Рет қаралды 3,759
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Profesa Mohamed Janabi ametoa rai kwa wananchi kuacha matumizi makubwa ya sukari ambapo amesema kuwa sukari haijawahi kumuacha mtu salama na kwamba miaka 300 iliyopita hapa Duniani kulikuwa hakuna kitu kinachoitwa sukari.
Profesa Janabi alikuwa anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Mtakanini Kata ya Msindo wilayani Namtumbo.