Рет қаралды 1,263
Marekani inaongeza kasi ya uwekezaji katika miradi mikubwa ya nishati jadidifu kama vyanzo vya umeme visivyochafua mazingira, yaani umeme rejeleshi kuendana na malengo ya taifa hilo.
Wamedhamiria kuachana na vyanzo visivyo rafiki wa mazingira ifikapo mwaka 2050 ambapo umeme jua na umeme wa upepo unachukua sehemu kubwa ya uwekezaji huo.
Mathalani katika jimbo la California, ambako kuna mwanga wa jua wa kutosha, mradi wa Westlands unaoendeshwa na sekta binafsi, unazalisha megawati 250 kutokana na jua.
Hassan Mhelela anaeleza zaidi alichokishuhudia...
#AzamNews #AzamTVUpdates #AzamTVHabari #USA