TFRA YAKUTANA NA WADAU KUTATHMINI MPANGO WA MBOLEA YA RUZUKU

  Рет қаралды 131

MBOLEA TV

MBOLEA TV

Ай бұрын

Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imefanya mkutano na wazalishaji pamoja na wafanyabiashara wa mbolea nchini ili kutathmini mwenendo mzima wa tasnia ya mbolea hususani utekelezaji wa mpango wa utoaji wa mbolea za ruzuku katika msimu wa 2023/2024.
Katika mkutano huo wadau hao wa mbolea wamejadili masuala mbalimbali katika tasnia ya mbolea yakiwemo mafanikio yaliyopatikana katika msimu wa kilimo wa 2023/2024.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent amekiri kuridhishwa na utekelezaji wa Mpango wa Ruzuku ya Mbolea ulioanza kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita mwaka 2022/23.
Amesema matumizi ya mbolea kupitia utekelezaji wa mpango wa ruzuku yameongeza usambaji, uzalishaji na matumizi ya mbolea kutoka tani… 2021/22 na kufikia takribani tani… 2023/24 na hivyo kuongeza tija ya kilimo na upatikanaji wa chakula
Mkurugenzi Laurent ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na Waingizaji na Wazalishaji wa mbolea wa ndani ya nchi katika kikao kilichofanyika katika Ofisi za Mamlaka Jijini Dar Es Salaam.
Aidha, Mkurugenzi Laurent aliwashukuru wadau kwa namna wanavyounga mkono juhudi za Serikali katika kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea kwa kuanzisha mashamba ya mfano katika maeneo mbalimbali nchini na kutoa huduma ya kupima afya ya udongo kwa wakulima ili kuwawezesha kutumia mbolea kulingana na mahitaji ya undongo na zao lililolimwa.
Akitaja mafanikio mengine katika utekelezaji wa Mpango wa Ruzuku amesema mtandao wa usambazaji wa mbolea umeongezeka na mfumo wa kidijitali wa utoaji na uuzaji wa mbolea za ruzuku umeimarika na kuwezesha na kurahisha usambazaji nchini.
Akizungumzia kikao hicho, Claudia Kimako, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara na Masoko wa Itracom amesema ni kikao cha kawaida kinacholenga kutoa mwanga wa namna nzuri ya kuanza msimu kwa kuondoa changamoto zilizobainika katika msimu unaoisha na kubaini fursa kwa msimu unaofuata.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) Samuel Mshote amesema katika msimu wa 2024/2025 wataagiza na kuşambaza kwa wakulima jumla ya tani 150,000 za mbolea za kupandia na kukuzia yenye ruzuku ya Serikali.Katika msimu ujao Mshote ameongeza kuwa TFC itanza uwekezaji katika ujenga wa kiwanda cha kuchanganyia mbolea chenye uwezo wa kuchanganya tani 120 kwa Saa.
" Katika msimu ujao tutakarabati maghala ya kuhifadhi mbolea yaliyopo Mbeya, Makambako Tabora, Mwanza, Sumbawanga na Songea na kuwa ya kisasa", Alisema Mshote.
Kwa mujibu wa Mshote katika msimu ujao TFC itaongeza mtandao wa mawakala wa usambazaji kutoka mawakala 400 Mpaka 1000.

Пікірлер: 1
@redeemer06Newsalerttz
@redeemer06Newsalerttz Ай бұрын
TFRA Kazi iendelee😊
Despicable Me Fart Blaster
00:51
_vector_
Рет қаралды 28 МЛН
ЧУТЬ НЕ УТОНУЛ #shorts
00:27
Паша Осадчий
Рет қаралды 10 МЛН
Summer shower by Secret Vlog
00:17
Secret Vlog
Рет қаралды 11 МЛН
Fast and Furious: New Zealand 🚗
00:29
How Ridiculous
Рет қаралды 24 МЛН
LIVE : RAIS DKT. JOHN P. MAGUFULI AKIWA NJIANI KURUDI DAR ES SALAAM
5:25
TFRA YANADI FURSA UWEKEZAJI VIWANDA VYA NDANI VYA MBOLEA
4:37
Tabia 10 Muhimu za Mafanikio
30:39
Success Path Network
Рет қаралды 379 М.
Despicable Me Fart Blaster
00:51
_vector_
Рет қаралды 28 МЛН