Рет қаралды 4,947
Bwana Maulid Mshangama Haji aliajiriwa katika Utumishi wa Serikali mara aliporejea kutoka masomoni Makerere na akajikuta katika msukosuko baada ya kupingana na Kamishna Mkuu wa Utawala miongoni mwa Maofisa wa Kikoloni wa Kiingereza Zanzibar. Raghba za ujananchi zilimpelekea kuingia kwenye siasa akiunga mkono chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na akawa mmoja miongoni mwa mawaziri vijana kwenye serikali ya mwanzo iliyokuja kupinduliwa Januari 1964. Ismail Jussa anatupitisha kwenye kurasa za kitabu chake "Sowing the Wind: Zanzibar and Pemba Before the Revolution."