Ujumbe wa mwaka mpya 2025 kutoka kwa Katibu Mkuu wa UN

  Рет қаралды 93

Habari za UN

Habari za UN

Күн бұрын

#HabarizaUN #UmojawaMataifa #Kiswahili #2025
Kwa mwaka mzima wa 2024, imekuwa vigumu kupata matumaini.
Vita vimesababisha maumivu makubwa, machungu na ukimbizi.
Ukosefu wa usawa na mgawanyiko vinaongezeka - na kuchochea mvutano na kukosa imani.
Na leo naweza kuripoti rasmi kuwa tumevumilia muongo wa joto kali.
Miaka 10 yenye joto zaidi ni katika miaka 10 iliyopita ikiwemo 2024.
Huku ni kuvurugika kwa tabianchi - mbele ya macho yetu. Lazima tuondoke kwenye mwelekeo huu wa uharibifu - na hatuna muda wa kupoteza.
Mwaka 2025, nchi lazima zielekeze dunia katika njia salama kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi na kuunga mkono mpito kuelekea mustakabali wa nishati salama.
Ni muhimu - na inawezekana. Hata katika siku za kiza zaidi, nimeona matumaini yakichochea mabadiliko.
Naona matumaini kwa wanaharakati - vijana na wazee - wakipaza sauti zao kwa maendeleo.
Naona matumaini kwa mashujaa wa kibinadamu wakivuka vikwazo na kusaidia watu walio hatarini zaidi.
Naona matumaini kwa nchi zinazoendelea zikipambana kusaka haki ya kifedha na tabianchi.
Naona matumaini kwa wanasayanasi na wagunduzi wakichukua hatua tofauti kwa ajili ya ubinadamu.
Na niliona matumaini mapya Septemba, viongozi wa dunia walipokutana na kupitisha Mkataba wa Zama Zijazo.
Mkataba ni hatua mpya ya kusongesha amani kwa kuzuia kusambaa kwa silaha.
Kurekebisha mfumo wa fedha duniani ili usaidie na kuwasilisha mataifa yote.
Kushinikiza fursa zaidi kwa wanawake na vijana.
Kushinikiza kuweka kanuni ili teknolojia iweke mbele watu na haki zaidi badala ya mchakato wa takwimu usiodhibitiwa.
Na kila mara, kuzingatia maadili na kanuni za haki za binadamu, sheria ya kimataifa na Chata ya Umoja wa Mataifa. Hakuna hakikisho la kilicho mbele ya 2025.
Lakini naahidi kushikamana na wale wote wanaosongesha mustakabali wenye amani zaidi, usawa, tulivu na afya kwa wote.
Kwa pamoja, tunaweza kufanya 2025 kuwa mwanzo mpya.
Si kama dunia iliyogawanyika. Bali mataifa yaliyoungana.

Пікірлер
Kituo cha Tanzania kinachojengea uwezo walinda amani wa UN
5:27
Habari za UN
Рет қаралды 4,1 М.
How did Turkey change Somalia's fate?
23:42
TVNET X
Рет қаралды 690 М.
Какой я клей? | CLEX #shorts
0:59
CLEX
Рет қаралды 1,9 МЛН
요즘유행 찍는법
0:34
오마이비키 OMV
Рет қаралды 12 МЛН
LOST TECHNOLOGIES: Mysteries of Vanished Civilizations
2:03:29
Lifeder Edu
Рет қаралды 8 МЛН
Young Lionel Messi Was Actually INSANE
14:20
VSP7 FOOTBALL
Рет қаралды 462 М.
Kauli baada ya Marekani kujiondoa WHO na lulu Bahrain
13:37
Habari za UN
Рет қаралды 300
Deedat's Funniest Response To Girl's Question On Hijab
6:51
ASIAN MUSLIMS
Рет қаралды 369 М.