Рет қаралды 10,146
Kamishina wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamishina Awadhi Haji amewatahadhari wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mkononi vinavyosababisha uvunjifu wa amani.Kamishina Awadhi alikuwa anazungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Mkongo Wilayani Namtumbo kufuatia watu wanne kuuawa kutokana na mgogoro wa wakulima na wafugaji.Amesema kitendo kilichotokea kiwe cha mwanzo na mwisho na kwamba jeshi la Polisi litafanya operesheni ya kuwasaka wote watakaojihusisha na vitendo hivyo.Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha wote waliohusika katika mauaji hayo wanasakwa,kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.