Рет қаралды 10
Wasichana zaidi ya mia moja ambao wanatarajia kujiunga na elimu ya juu na kati wamepatiwa elimu ya kujitambua ikiwemo afya ya uzazi pamoja na matumizi sahihi ya mitandao ili kuepuka vitendo vya udhalilishaji
Wasichana hao ambao wanatoka mazingira hatarishi na wanafadhiliwa na shirika la Camfed wamesema elimu hiyo itasaidia namna yakuripoti matukio ya ukatili ikiwemo wakingono pindi yanapotokea wakiwa chuoni.
Mratibu wa Camfed mkoa wa Iringa, Neema Msemwa amesema kuwa wameona vyema kuwapa elimu ya afya ya uzazi ili kujiepusha na vishawishi visivyofaa wawapo chuoni
Kwa upande wake Christopher Jacob ambaye ni muuguzi mkunga hospitali ya kilolo Ameshauri vijana wakike kuacha matumizi ya dawa za kuzuia mimba zikiwemo P2 bila kufahamu athari zake, kutokana na baadhi ya dawa hizo kusababisha changamoto za kiafya ikiwemo saratani na ugumba.
#nurufm
#nurudigital