Рет қаралды 8,475
Goma. Mapigano mazito yanayoendelea kati ya kundi la M23 na vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yamesababisha vifo vya watu 25 huku 375 wakirjeruhiwa katika mrushiano wa risasi kati ya pande hizo.
Al Jazeera imeripoti kuwa watu hao walifariki na wengine kujeruhiwa kwenye mapigano yaliyotokea kuanzia jana Jumatatu hadi leo Jumanne Januari 28,2025 huku hospitali zilizopo Mji wa Goma zikirajwa kuelemewa na majeruhi wa mapigano hayo.
Jana Jumatatu Umoja wa Mataifa ambao uliishutumu Rwanda kuwafadhiri wapiganaji wa kundi la M23 kufanya uvamizi huo, ulisema waasi hao wameshauzingira Mji wa Goma nchini DRC.
Kuutwaa Mji wa Goma ni pigo kwa Serikali ya Rais Felix Tshisekedi kufuatia mapigano yaliyodumu kwa miezi kadhaa kati ya M23 na askari wa Jeshi la nchi hiyo FARDC, huku Mji wa Goma ukiwa kitovu cha biashara katika Miji iliyopo mashariki mwa DRC.
Waziri wa Maendeleo ya Vijijini wa DRC, Muhindo Nzangi amethibitisha leo kuwa waasi hao wameshauteka Mji wa Goma kwa asilimia zaidi ya 80, huku akidai kuwa vikosi vya Jeshi la Rwanda vimeweka kambi katika maeneo mengine ya mji huo.
Katika mkutano na vyombo vya habari nchini humo, Nzangi ameueleza Umoja wa Mataifa kuwa hospitali katika mji huo zimeanza kuelemewa kutokana na ongezeko la majeruhi wa mapigano hayo huku miili mingine ikionekana kuwepo katika mitaa ya mji huo.
“Hadi sasa kuna mamia ya watu waliojeruhiwa katika hospitali eneo la Goma, wengi wao wamelazwa wakiuguza majeraha ya risasi walizopigwa na waasi hao,” amesema Adelheid Marschang, ambaye ni Mratibu wa Shughuli za Dharura wa kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) nchini DRC.
Amesema kati yao watu 17 wamefariki jana mjini Goma huku sita wakifariki kuanzia leo asubuhi kwenye mapigano hayo na kuongeza kuwa watu 367 wamejeruhiwa katika mapigano hayo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la kutetea haki za watoto la Save the Children nchini DRC, Greg Ramm, amesema: “Tumekuwa tukipokea ripoti kuwa kuna wakati mitaa inatulia lakini baada ya muda kidogo zinasikika risasi kila mahali,”
Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayotoa huduma za kibinadamu nchini humo, Jens Laerke, amesema pamoja na mirindimo ya risasi, mitaani kunaonekana uwepo wa miili ya watu chini wakidhaniwa kuwa nao wamefariki.
Kutokana na mapigano hayo, huduma za kibinadamu ikiwemo za mpango w Chakula zimesitishwa kwa muda katika Mji wa Goma huku hofu ya u