Рет қаралды 38
Ukombozi wa Afrika ni sehemu muhimu ya historia yetu, ni historia inayotuunganisha na kuelezea juhudi za kipekee za Waasisi wetu katika kupigania Uhuru na haki, kwa kutambua hilo Kituo cha Urithi wa Ukombozi, kinafanya kazi muhimu ya kudijiti nyaraka na kumbukumbu za ukombozi. Hii ni hatua muhimu katika kutunza na kuhifadhi historia yetu ya ukombozi, aidha itafungua milango ya elimu, ufahamu, na uelewa kwa vizazi vijavyo, na kuwapa fursa ya kujifunza na kuenzi mapambano ya ukombozi wa Afrika.