MAAJABU YA JIWE LA GINGILI UKILISEMESHA LINAKUJIBU

  Рет қаралды 2,561

Super News TV

Super News TV

Күн бұрын

Tanzania kuna mambo makubwa ambayo wengi hawayafahamu. Karibu, Tukiwa Mkoa wa Simiyu - Wilaya ya Meatu Jimbo la Kisesa - Mwandoya - Kijiji cha Igobe - Mtaa wa Mwagingili ambako kuna jiwe maarufu la Gingili lenye miujiza, Mr. Super News alifanikiwa kufika kwenye jiwe hilo.
Baada ya kupata taarifa ya mlima wenye Jiwe kubwa lenye miujiza, yaani ukilisemesha linakujibu kwa kutikisika. Kwa mujibu wa Maelezo ya wenyeji wa eneo hilo walisema Jiwe hilo limekuwa likitumiwa na watu kutoka maeneo mbalimbali kupigia Lamuli kwa ajili ya kujua na kutatua shida zao.
Najua unatamani kufahamu historia ya Jiwe hilo la Gingili, iko hivi Gingili alikuwa ni Mtemi wa eneo hilo baadae alifariki na akazikwa. Katika hali isiyo ya kawaida kwenye kaburi lake ndipo lilipo ibuka jiwe kubwa, jiwe hilo lika hama kwa kuviringita kutoka sehemu ya Kaburi mpaka hapa lilipo sasa.
Jamii ya watu wanao ishi hapo wakapeana taarifa kuwa Gingili ameamka na amehama kutoka kwenye Kaburi lake na kusogea pembeni kidogo.
Kwa Imani zao wakazi wa eneo hilo wakaona kwa sababau alikuwa mtemi, kutokana na taratibu zao za kimira ndipo wakaanza kulitumia jiwe hilo kuomba ili matatizo yao yaweze kutatuliwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya wenyeji walisema kweli matatizo yao huwa yanatatuliwa. Mr. Super News baada ya kufika mpaka kwenye Jiwe hilo alishuhudia mambo mengi watu wakiendelea kuliomba jiwe liwasaidie kujua na kutatua shida zao. Enjoy to watch Super News TV subscribe our Channel for more videos.

Пікірлер: 3
Maajabu ya Daraja la Mungu na Simulizi ya Kusisimua ya Nyerere na Warusi
14:50
escape in roblox in real life
00:13
Kan Andrey
Рет қаралды 35 МЛН