Рет қаралды 127,751
Timu ya taifa ya Zanzibar… #ZanzibarHeroes imeibuka na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2025 kwa kuichapa Burkina Faso mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa leo kwenye Dimba Gombani, Pemba.
Zanzibar walitangulia kupata bao dakika ya 41 kwa kisigino cha Ibrahim Hamad Hilika, kisha Burkina Faso wakachomo dakika ya 69 kupitia kwa Aboubacar Traore…. Lakini dakika za majeruhi, Hassan Ali Cheda akafunga la pili na la ushindi kwa Zanzibar.