Papa Francis Akutana na Rais Samia, Waongea kwa Dakika 15, Wapeana Zawadi, Waweka Historia Mpya

  Рет қаралды 18,511

Jugo Media Network

Jugo Media Network

Күн бұрын

𝐖𝐄𝐙𝐄𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐓𝐔𝐌𝐄 𝐖𝐀 𝐉𝐔𝐆𝐎 𝐌𝐄𝐃𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐏𝐈𝐓𝐈𝐀 𝐌-𝐏𝐄𝐒𝐀 𝐋𝐈𝐏𝐀 𝐍𝐀𝐌𝐁𝐀 𝟓𝟎𝟓𝟒𝟔𝟑𝟓 𝐉𝐈𝐍𝐀 𝐉𝐔𝐆𝐎 𝐌𝐄𝐃𝐈𝐀 𝐍𝐄𝐓𝐖𝐎𝐑𝐊
Takwimu zinaonesha kwamba, Kanisa Katoliki nchini Tanzania linamiliki na kuendesha shule za awali 240, shule za msingi 147, shule za sekondari 244, vyuo vya ufundi, vyuo vikuu 5; taasisi za elimu ya 5 na vituo vya vyuo vikuu 2 ambavyo viko chini ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino, SAUT. Vyuo vyote hivi vina jumla ya wanafunzi 31, 000 pamoja na taasisi za afya ni 473, lengo likiwa ni kumhudumia mtu mzima: kiroho na kimwili. Kuna uhusiano mkubwa kati ya shule zinazomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki pamoja na dhamana ya Uinjilishaji wa kina inayovaliwa njuga na Mama Kanisa katika mapambazuko ya Uinjilishaji nchini Tanzania. Ili kutambua umuhimu huu, kuna haja kwanza kwa walimu, walezi na wanafunzi wenyewe kufahamu changamoto inayoletwa na Kanisa kwa wakati huu! Shule na taasisi za elimu ya juu pamoja na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na kuendeshwa na Kanisa Katoliki, vimekuwa ni vituo vya majiundo makini ya vijana: kiakili, kimaadili, kiroho na kiutu, kwa kuzingatia ubora na viwango vya kitaifa na kimataifa, ukweli ambao kamwe hauwezi kufumbiwa macho nchini Tanzania. Elimu bora inayotolewa na Kanisa inalenga kuwajengea wahitimu uwezo wa kujiamini na kumudu ushindani wa kitaifa na Kimataifa kwa kuwapatia: elimu, ujuzi na uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa Tanzania katika ujumla wake.
Rais Samia akipokea zawadi kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko
Rais Samia akipokea zawadi kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko
Imegota takribani miaka 12 tangu Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania alipotembelea mjini Vatican na kukutana na Baba Mtakatifu Benedikto XVI tarehe 19 Januari 2012. Katika mazungumzo ya dakika kumi na tano, viongozi hawa wawili waligusia kuhusu: Majadiliano ya kidini, amani katika eneo la Maziwa Makuu, Afya, Ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Ni katika muktadha wa kujenga na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Vatican, tarehe 12 Februari 2024, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Baadaye, Rais Samia amebahatika pia kukutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameambatana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa. Katika mazungumzo yao ya faragha yaliyodumu kwa takribani dakika ishirini na tano, wameridhika na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Vatican na Tanzania; mchango na dhamana ya Kanisa Katoliki katika ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu nchini Tanzania, hususan katika sekta ya: elimu, afya na ustawi wa jamii pamoja na changamoto ambazo Tanzania inapitia kwa sasa. Baadaye, wamejielekeza zaidi katika masuala ya kijamii nchini Tanzania; masuala ya kikanda na Kimataifa na umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa katika kujikita katika kudumisha amani ulimwenguni.
Rais Samia akimpatia zawadi Baba Mtakatifu Francisko
Rais Samia akimpatia zawadi Baba Mtakatifu Francisko
Rais Samia Suluhu Hassan katika ziara hii ya kitaifa, alikuwa ameambatana na Mama Evaline Malisa Ntenga, ambaye hivi karibuni amechaguliwa kuwa ni Mjumbe wa Bodi Umoja wa Wanawake Wakatoliki Duniani na Rais wa WUCWO Afrika, ambaye pia ni Mwenyekiti wa WAWATA, Taifa, nchini Tanzania. Prof. Deogratias Rutatora, Mwenyekiti Halmashauri ya walei, Taifa; Leonard Mapolu, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wakatoliki Wafanyakazi Tanzania, Taifa, VIWAWA; Dalmas Gregory, Mwenyekiti Halmashauri Walei, Jimbo Katoliki la Zanzibar pamoja na Theresia Seda, Mwenyekiti wa Utoto Mtakatifu, Jimbo kuu la Dar es Salaam.
Follow this link to join my WhatsApp group: chat.whatsapp....
Tumsifu Yesu Kristo, Napenda Kukushukuru kwa Kuwa Mdau Mpendwa wa Jugo Media. Tunapenda kukutaarifu kuwa Tumeandaa Group Maalum kwa Ajili ya Kupokea Taarifa Mbalimbali za Kanisa, Misa Live, Vipindi vya Kanisa nk kutoka Jugo Media. Kama ungependa Kuungana Nasi Tunaomba Ujiunge kwa Hiari Kupitia Link Hiyo Juu.
KAMA UNGEPENDA KUPATA TAARIFA KUHUSU KANISA KWA NJIA YA WHATSAPP TAFADHARI TUMA UJUMBE KWA WHATSAPP UKISEMA NIUNGE KISHA JINA LAKO KWENDA NAMBA +255757560764 au BONYEZA LINK HII wa.me/+2557575...) (SAVE HII NAMBA KWANZA, ANDIKA JUGO MEDIA)
KAMA UNA HABARI NA UNGEPENDA KUSHIRIKI PAMOJA NASI TAFADHARI WASILISHA KUPITIA WHATSAPP NO +255757560764 AU BONYEZA wa.me/+2557575...)
Tafadhali Subscribe, Like, Comment na Share tone hili la upendo kwa ndugu jamaa na marafiki.
𝐉𝐮𝐦𝐮𝐢𝐤𝐚 𝐧𝐚𝐬𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐦𝐢𝐭𝐚𝐧𝐝𝐚𝐨 𝐦𝐢𝐧𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐲𝐚 𝐊𝐢𝐣𝐚𝐦𝐢𝐢:
Instagram: / jugo_media
Facebook: / jugomedia2019
𝕄𝕒𝕨𝕒𝕤𝕚𝕝𝕚𝕒𝕟𝕠:
JUGO MEDIA,
Sokoine Drive, Posta
P. O. BOX 34014,
Dar es Salaam.
For Bookings and other Enquiries
Phone Number +255757560764/657790405
#jugomedia #kanisakatoliki #familiatakatifu #wawata #uwaka #viwawa #australia #unitedstates #canada #america

Пікірлер: 32
«Жат бауыр» телехикаясы І 26-бөлім
52:18
Qazaqstan TV / Қазақстан Ұлттық Арнасы
Рет қаралды 434 М.
24 Часа в БОУЛИНГЕ !
27:03
A4
Рет қаралды 7 МЛН
Papa Francis atembelea chimbuko la Uislamu
0:47
DW Kiswahili
Рет қаралды 86 М.
«Жат бауыр» телехикаясы І 26-бөлім
52:18
Qazaqstan TV / Қазақстан Ұлттық Арнасы
Рет қаралды 434 М.