Рет қаралды 1,682
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi anayoifanya inasababisha atukanwe lakini anajifanya chura kutowasikiliza ili atimize mipango yake.
“Mchechu fanya kazi yako najua utalaumiwa lakini hiyo ndiyo kazi niliyokupa simama ifanye mimi kazi niliyopewa na Watanzania nimesimama naifanya na mnashuhudia matusi ninayotukanwa mpuuzi, hana maana, huyu bibi yaani mambo tele lakini najigeuza chura,” amesema Rais Samia leo Juni 11 2024 Ikulu ya Dar es Salaam kwenye hafla ya kukabidhi gawio kwa Serikali kutoka kwenye mashirika ya umma na binafsi ambayo Serikali ina hisa zake.