Salama Na DR TULIA SE6 EP50 | BULYAGA 1976 PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

  Рет қаралды 32,954

YahStoneTown

YahStoneTown

Жыл бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Tulia Ackson ni jina kubwa kati ya majina makubwa kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kwa sisi kuweza kulipata jina kubwa na kukubali kuja kuketi kwenye kiti chetu chakavu ilikua ni BARAKA sana. Ila ukiachana na kwamba ni jina kubwa ila yeye ni binadamu, tena wa kawaida tu. Ni Mama, ni mke, ni Dada, ni Binti kwa Mama yake na ni Mbunge kwa wana Mbeya mjini lakini pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wadhifa ambao baada ya uchaguzi wa 2020 alirudi bungeni kama Naibu Spika ila baada ya aliyekua Spika kujiuzulu Dr Tulia aliona fursa ya yeye kuvaa viatu hivyo na wabunge nao walimpa kura zao zote za kuridhia Mwana Dada huyu AWAONGOZE.
Baada ya uchaguzi wa 2020 na yeye alirudi bungeni kama MBUNGE kamili, si tunakumbuka baada ya 2015 alienda bungeni kama Mbunge wa kuteuliwa ila mwaka 2020 aliamua kwenda kugombea jimbo la Mbeya mjini ambako Gwiji wa Bongo Flava Kaka yangu Joseph Mbilinyi aka Sugu alikua ndo Mbunge wake? Sugu alikaa kule kwa miaka 10 ilikua ni moja ya ngome za wapinzani ambazo walikua wanajivunia nazo, kwa Dr Tulia kuamua kwenda kugombea pale iliwafanya watu wengi watake kufuatilia mchuano huo mkali ambao mwisho wa siku Dr Tulia aliibuka kidedea. Na haya yalikua ni moja ya maswali ambayo nilikua na hamu ya kumuuliza na kwa urefu alinijibu tu vizuri sana.
Sasa nchi yetu inaongozwa na Rais mwanamke kwa mara ya KWANZA toka tulipopata uhuru wetu mwaka 1961, na hii haikuja kwa kupangwa ila baada ya kutokea ambalo Mwenyezi alikua ameliandika, na hata hili la kuwa na Spika Mwanamke (ingawa huko nyuma Mama Anne Makinda alishawahi kuwa) nalo halikua limepangwa maana Spika tayari tulikua naye baada ya Uchaguzi wa 2020. So suala la kuwa na Rais mwanamke na Spika mwanamke bila ya shaka linalipa Taifa letu utofauti na HESHIMA flani hivi ambao mataifa mengi yanavutiwa nayo.
So kwake yeye nini hasa kimebadilika? Yaani kutoka kuwa Naibu mpaka sasa Spika? Ilikua easy kwake kuichukua nafasi hiyo baada ya kuwepo na nafasi hiyo? Alifikiria mara mbili?
Kwa maongezi yetu haya pia nimegundua Dr Tulia alikua hapendi kabisa siasa, yeye aliyapenda zaidi maisha yake ya kuwa Lecturer pale Chuo Kikuu, alipenda zaidi kuandika na kusoma na kujifunza. Alikua akiwaona wana Siasa kama watu flani ambao pengine wanajiona tofauti na watu wengine, pengine wanajiona wa MUHIMU sana. Je na yeye sasa? Akiwa nao kule bungeni wanaishi vipi? Sasa pia kama Kiongozi wa mhimili huo wa NCHI nini zaidi kimebadilika? Nini zaidi kigumu?
Maongezi yetu yalianzia nyuma kiasi na mbele pia yakafika, pia humu tumeongelea Tulia Trust na vitu ambavyo inafanya ili kuwafikia wale ambao wana uhitaji. Na sasa amekua naye MWANASIASA, nini kimebadilika? Msemo wa Siasa ni mchezo mchafu, kwake yeye una maana gani?
Yangu matumaini uta enjoy na kujifunza jambo kutoka kwa Kiongozi huyu ambaye pia ni Dada yetu.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪KZbin Link bit.ly/KZbinSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 76
@drmdee
@drmdee Жыл бұрын
Naomb salama ukianza kuwahoj Hawa uwe unaulizia historia zao walipozaliwa,waliposoma na maisha yao
@davidwillson4894
@davidwillson4894 Жыл бұрын
Dr Tuli, you are smart, jeeembe letu la Mbeya
@mohamedismail2662
@mohamedismail2662 Жыл бұрын
Akili kubwa ambayo bado naona haijatumika vzur tunaitumia kisiasa zaidi Mungu akubariki Dr Tulia nakuona mbali sana endelea ivyo ivyo
@ramadhanomar8346
@ramadhanomar8346 Жыл бұрын
km na wew umesoma HKL KM MAMA TULIA ACKOSON LIKES HAPA. HUWAGA TUNAONGEA
@noeljuvenalmunishi75
@noeljuvenalmunishi75 Жыл бұрын
Beauty, Brain and confidence (BBC) in one person @Dr Tulia Ackson...
@dostovan5142
@dostovan5142 Жыл бұрын
Beauty is questionable
@skteller5039
@skteller5039 Жыл бұрын
😂minus one B tafadhali
@hopxzbahati1078
@hopxzbahati1078 Жыл бұрын
As a member of the Comment Reading Association (CRA), I’m only here to read comments. Please keep the comments short and simple. We do appreciate your typing effort. Also please watch your spelling. Thank you and have a great day!
@pastorteddywaziri5754
@pastorteddywaziri5754 Жыл бұрын
😂😂😂🙌🙌🙌
@Felister100
@Felister100 Жыл бұрын
😂😂😂
@seinabelimi2296
@seinabelimi2296 Жыл бұрын
Naam kwanza ss wanaume tutambue thamani ya mwanamke ktk maisha yetu mfano tu hai kitendo cha mwanamke kazi ya kulea mimba miez 9 heka heka anayopitia mwanamke hata uuze dunia na vilivyomo huwez katu kumlipa hapo bado kwenda leba kwa uchungu na kuzaa na kunyonyesha mtoto hv una kipi cha kumlipa mwanamke huyo zaid ya kumfanyia ihisani mapenz huruma na upole kwao kitendo cha mwanamke kuweka kiumbe tumbon ni hekima ya Mwenyezi Mungu wanawake wanaweza tuwaheshimu na kuwapa elimu ya kutosha ya dini na dunia na tuwathamini tuliingia ktk kupitia tupu zao na humo humo ndo njia ya ss kutokea namuomba mola wangu awalinde na kila baya na kila shari na kila hasad tupate kufaulu ktk huu mgongo wa dunia✍✍
@edwinmandela5658
@edwinmandela5658 Жыл бұрын
ko ulitaka wote tunyonyeshe mngekula nini
@mwaminitindwa7131
@mwaminitindwa7131 Жыл бұрын
Mwenyezi mungu akubariki sana kwa hekma hizo, no wachache sana wanaotambua thamani ya mwanamke
@seinabelimi2296
@seinabelimi2296 Жыл бұрын
@@mwaminitindwa7131 shukrani kipenz cha Allah ikiwa unatambua kuna Allah bs utatambua kuna viumbe vya Allah☝️
@nassornassor9678
@nassornassor9678 Жыл бұрын
Talent women big up nimefurahi umetofautisha kazi na siasa umependa kazi kuliko siasa that good 👍
@mzizirashid709
@mzizirashid709 Жыл бұрын
Huyu Mama Yupo Vizurii Jaman Anavyojibu Maswaliii Huchoki Kumsikiliza Yaani Hadi Rahaaa 🥰 Tanzania inawatu Jaman Vichwaa Haswaaaa
@gertrudegwarasa632
@gertrudegwarasa632 2 ай бұрын
Here I am Mama. Nilisoma HKL pia🤝🥰
@mimmyjijimmy5235
@mimmyjijimmy5235 Жыл бұрын
Tunamuomba Halima Mdee nadhan itapendeza sana
@jescalaurenti4970
@jescalaurenti4970 Жыл бұрын
She's my role model and my mentor@ Mh Tulia ..... As a youth we should have mentors who inspire us on chasing our dreams en goals.. Big up mom... 💪 Let's start dreaming big as the upcoming leaders.
@januaryrashid8844
@januaryrashid8844 Жыл бұрын
Speaker ( Akson) Mama uko vzr saaana,unajibu maswali kwa confidence ya juu saana, Salama asant kwa kumleta speaker
@G.r.e.a.t.I.Q
@G.r.e.a.t.I.Q Жыл бұрын
Kibonge Salamaaaa!👋👋
@ilhamsalum6815
@ilhamsalum6815 Жыл бұрын
Msuko wa ki Zanzibari kabisa # chana la ndizi 🥰 umependez sis SALAMA
@gladnesskombe1664
@gladnesskombe1664 Жыл бұрын
Nimefurahi sana kumuona huyu jemedari wetu wa uongozi Mungu amlinde awe na maisha marefu ya baraka tele
@seinabelimi2296
@seinabelimi2296 Жыл бұрын
maisha lazima kutafakar huko ndo kufaulu ktk kila lko ktk maisha kuchukua muda wako na kulifanyia kaz huko ndo kunazalika hekima busara na utu ni muhimu mno maishan mwetu mola atusimamie atutangulie sote ktk hilo ndo msingi wa maisha yetu✍✍
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 Жыл бұрын
Yaani da Salama umependeza sana haki ya mzungu tena wala sikutanii
@mussachabonga9595
@mussachabonga9595 Жыл бұрын
Sister Salama big up, this my super woman, fantastic interview 2023
@rommelmauma8081
@rommelmauma8081 Жыл бұрын
Zamani, kazi zilijigawa sana, kijinsia, kulingana na nguvu za misuli yetu. Leo hii, kazi hazitegemei nguvu ya misuli. Teknolojia ya mashini imetuokoa na utegemezi wa misuli; *tunategemea ubongo*! Na uwezo wa ubongo *transcends the gender divide*, japo mila za *kikabila* bado nyingi *work at the advantages of the boys and at the disadvantages if the girls*.
@ashooraashoora1180
@ashooraashoora1180 Жыл бұрын
Tumefrah kweli Allah akuongoze katika Khery duniani na kesho akhera
@aminaomary5567
@aminaomary5567 Жыл бұрын
Salama safi sana,kualika viongozi,mimi binafsi naomba umwalike Mh.Majaliwa
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 Жыл бұрын
Napenda anavyojibu Mheshimiwa Tulia.
@stellah3844
@stellah3844 Жыл бұрын
Dr Tulia 💞💞💞💞💞💞
@abuujuhayfa4321
@abuujuhayfa4321 Жыл бұрын
Big up kwa muheshimiwa 🤝
@yusufmohamed8874
@yusufmohamed8874 Жыл бұрын
Salama umetisha sana
@hansmwasakyeni3038
@hansmwasakyeni3038 Жыл бұрын
Bunge saizi lina spika kwakweli! Dada namuelewa sana saizi!
@jasmineedamu6089
@jasmineedamu6089 Жыл бұрын
Salama na tulia 💕
@tanzaniamycountry9308
@tanzaniamycountry9308 Жыл бұрын
Kumbe waheshimiwa kama Hawa inawezekana kuja mezan eh? Sasa niombe umwalike mama yetu uvunje rekod kabisa😊
@MandrivaShinnyFirstMedia
@MandrivaShinnyFirstMedia Жыл бұрын
Always good job salama
@amrimtiti9054
@amrimtiti9054 Жыл бұрын
Namkubali sana spika wa bunge letu na nawish kama ningekutuna nae siku moja
@yahyahamad1802
@yahyahamad1802 Жыл бұрын
salama mlete dada Sofia mjema
@nahyialetomia9284
@nahyialetomia9284 Жыл бұрын
Goal 3 in the Millennium development goals - promote gender equality and empower women
@massawemrlowprice3949
@massawemrlowprice3949 Жыл бұрын
Namba 3
@KamodiTV
@KamodiTV Жыл бұрын
Kamodi star ✴️
@maryamtanzania9743
@maryamtanzania9743 Жыл бұрын
Salamama umenenepa umependeza
@mzizirashid709
@mzizirashid709 Жыл бұрын
Anayefuata Ni Mr Polepole 🥰
@tausonsamwel8736
@tausonsamwel8736 Жыл бұрын
Bulyaga my home from Tukuyu (took you)
@buberwadeus3158
@buberwadeus3158 Жыл бұрын
👏👏👏
@msowamhokole7714
@msowamhokole7714 Жыл бұрын
Mlete konde ama mengi ya kutujibu maana katrend sana
@stevewanga957
@stevewanga957 Жыл бұрын
from🇶🇦🇶🇦 2ko locked
@assumaninadja315
@assumaninadja315 Жыл бұрын
Natamani nimuone Diamond kwenye hio meza please
@bedabenson6576
@bedabenson6576 Жыл бұрын
Lete Mgunda
@kilamiko8299
@kilamiko8299 Жыл бұрын
Hata kuchunga ng'ombe huwezi kusoma utalisha mazao ya watu ama mifugo kupotea hahah
@sheikhmuharammwaita
@sheikhmuharammwaita Жыл бұрын
Mashallah, umenenepa salama
@jaymwinyi6957
@jaymwinyi6957 Жыл бұрын
Mashaallah 👏 tabarakallah Tena sana 🤣mashavu mashavu
@marygregory7566
@marygregory7566 Жыл бұрын
Nimejifunza umuhimu kutafakari
@Johnsonkayila
@Johnsonkayila Жыл бұрын
Salama fanya ufanyavyo umlete Mh Khasim Majaliwa;alafu baada yake Mlete Mzee Mwinyi Rais wa Zanzibar
@kakakuona57
@kakakuona57 Жыл бұрын
Spika,je unaridhika kuongoza bunge lenye wabunge wa chama chako TU?
@donnietommie8444
@donnietommie8444 Жыл бұрын
#SalamaNaDrLeaky
@michaellagwen8198
@michaellagwen8198 Жыл бұрын
Huu msuko wa Salama unaitwaje mwenzenu Mpaka nimewaza kwa sauti
@dostovan5142
@dostovan5142 Жыл бұрын
Kwende kazi
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 Жыл бұрын
Salama na juma lokole 😝please please please please
@johnsahani4182
@johnsahani4182 Жыл бұрын
Mlete na ndugai
@mountaincoffee7
@mountaincoffee7 Жыл бұрын
Mlete ayo tz
@semsimbazisemsimbazi2866
@semsimbazisemsimbazi2866 Жыл бұрын
Tuleteeni mzee Mwinyi jamani....
@dostovan5142
@dostovan5142 Жыл бұрын
Hapana
@raiyansaleh9255
@raiyansaleh9255 Жыл бұрын
Milard ayo mlete
@ahmedahzab9439
@ahmedahzab9439 Жыл бұрын
Ndani ya dakika 9 nzima wa kuongea pumba ukiachia kukosea Matamshi licha yakua ni gwiji wakusema.👌🏽
@edwardmwakanolo1259
@edwardmwakanolo1259 Жыл бұрын
Mama mwenye Jimbo lake..Mbozyo mwenyewe,mama asiye na makuu,kimbilio la wengi,mfuta machozi wa Wanambeya,mama piga kazi ,mama mwenye HEKIMA,mama bingwa ,Jimbo la Mbeya limetulia na Dr.Tulia
@victornjwango9683
@victornjwango9683 Жыл бұрын
Mlete njwango b
@athumanimtengo3350
@athumanimtengo3350 Жыл бұрын
Napenda sana uelewa wa Huyu mama, namkubali katika hilo suala kwa kweli..ana akili mno na navutiwa kumsikiliza 🙏🙏🙏🙏🙏
@Nyimbozainjil
@Nyimbozainjil Жыл бұрын
Mbeya for TULIA Ackson
@paulsibu5770
@paulsibu5770 Жыл бұрын
Mlete Mama Samia Kiongozi Shupavu.
@fadhilshafi2947
@fadhilshafi2947 Жыл бұрын
she's smart
@hendrycomonsiwenga1128
@hendrycomonsiwenga1128 Жыл бұрын
Nimefurai kumuona Mhe, Dk. Tulia Akson ( Spika Wa Bunge La Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania ) Hongera umeongea point ☝️🤣
@samsonmwakikuti5318
@samsonmwakikuti5318 Жыл бұрын
Unastahili nafasi hiyo,si bahati tu!!
Iron Chin ✅ Isaih made this look too easy
00:13
Power Slap
Рет қаралды 35 МЛН
Now THIS is entertainment! 🤣
00:59
America's Got Talent
Рет қаралды 40 МЛН
Llegó al techo 😱
00:37
Juan De Dios Pantoja
Рет қаралды 53 МЛН
EXCLUSIVE: NYUMBA ZA ZARI SOUTH AFRICA, MAGARI NA MAISHA
14:47
Millard Ayo
Рет қаралды 1,3 МЛН
"They Are Stealing My Culture!" Bassem Youssef On Netflix's 'Cleopatra' Casting
9:24
Piers Morgan Uncensored
Рет қаралды 3,9 МЛН
Моя Жена Босс!
0:40
Petya English
Рет қаралды 8 МЛН
The cat chose the right one 🥰🥳😸
0:32
Ben Meryem
Рет қаралды 27 МЛН
Best Toilet Gadgets and #Hacks you must try!!💩💩
0:49
Poly Holy Yow
Рет қаралды 10 МЛН