Salama Na DR TULIA SE6 EP50 | BULYAGA 1976 PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

  Рет қаралды 17,211

YahStoneTown

YahStoneTown

Күн бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Tulia Ackson ni jina kubwa kati ya majina makubwa kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na kwa sisi kuweza kulipata jina kubwa na kukubali kuja kuketi kwenye kiti chetu chakavu ilikua ni BARAKA sana. Ila ukiachana na kwamba ni jina kubwa ila yeye ni binadamu, tena wa kawaida tu. Ni Mama, ni mke, ni Dada, ni Binti kwa Mama yake na ni Mbunge kwa wana Mbeya mjini lakini pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wadhifa ambao baada ya uchaguzi wa 2020 alirudi bungeni kama Naibu Spika ila baada ya aliyekua Spika kujiuzulu Dr Tulia aliona fursa ya yeye kuvaa viatu hivyo na wabunge nao walimpa kura zao zote za kuridhia Mwana Dada huyu AWAONGOZE.
Baada ya uchaguzi wa 2020 na yeye alirudi bungeni kama MBUNGE kamili, si tunakumbuka baada ya 2015 alienda bungeni kama Mbunge wa kuteuliwa ila mwaka 2020 aliamua kwenda kugombea jimbo la Mbeya mjini ambako Gwiji wa Bongo Flava Kaka yangu Joseph Mbilinyi aka Sugu alikua ndo Mbunge wake? Sugu alikaa kule kwa miaka 10 ilikua ni moja ya ngome za wapinzani ambazo walikua wanajivunia nazo, kwa Dr Tulia kuamua kwenda kugombea pale iliwafanya watu wengi watake kufuatilia mchuano huo mkali ambao mwisho wa siku Dr Tulia aliibuka kidedea. Na haya yalikua ni moja ya maswali ambayo nilikua na hamu ya kumuuliza na kwa urefu alinijibu tu vizuri sana.
Sasa nchi yetu inaongozwa na Rais mwanamke kwa mara ya KWANZA toka tulipopata uhuru wetu mwaka 1961, na hii haikuja kwa kupangwa ila baada ya kutokea ambalo Mwenyezi alikua ameliandika, na hata hili la kuwa na Spika Mwanamke (ingawa huko nyuma Mama Anne Makinda alishawahi kuwa) nalo halikua limepangwa maana Spika tayari tulikua naye baada ya Uchaguzi wa 2020. So suala la kuwa na Rais mwanamke na Spika mwanamke bila ya shaka linalipa Taifa letu utofauti na HESHIMA flani hivi ambao mataifa mengi yanavutiwa nayo.
So kwake yeye nini hasa kimebadilika? Yaani kutoka kuwa Naibu mpaka sasa Spika? Ilikua easy kwake kuichukua nafasi hiyo baada ya kuwepo na nafasi hiyo? Alifikiria mara mbili?
Kwa maongezi yetu haya pia nimegundua Dr Tulia alikua hapendi kabisa siasa, yeye aliyapenda zaidi maisha yake ya kuwa Lecturer pale Chuo Kikuu, alipenda zaidi kuandika na kusoma na kujifunza. Alikua akiwaona wana Siasa kama watu flani ambao pengine wanajiona tofauti na watu wengine, pengine wanajiona wa MUHIMU sana. Je na yeye sasa? Akiwa nao kule bungeni wanaishi vipi? Sasa pia kama Kiongozi wa mhimili huo wa NCHI nini zaidi kimebadilika? Nini zaidi kigumu?
Maongezi yetu yalianzia nyuma kiasi na mbele pia yakafika, pia humu tumeongelea Tulia Trust na vitu ambavyo inafanya ili kuwafikia wale ambao wana uhitaji. Na sasa amekua naye MWANASIASA, nini kimebadilika? Msemo wa Siasa ni mchezo mchafu, kwake yeye una maana gani?
Yangu matumaini uta enjoy na kujifunza jambo kutoka kwa Kiongozi huyu ambaye pia ni Dada yetu.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪KZbin Link bit.ly/KZbinSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 37
@amirymdee4259
@amirymdee4259 Жыл бұрын
***Nilichofurahishwa hapo ***Doctor Tulia kachapa Kiswahili tu hongera sana bibi****
@mbwanaseif404
@mbwanaseif404 Жыл бұрын
The best interview hongera Salama na hongera Dr Tulia
@seinabelimi2296
@seinabelimi2296 Жыл бұрын
ukweli humueka mtu huru na huyu dada ni mwema na msafi wa niya na anajituma anajuwa wajibu wake kwann mm mbunge nina wajibu gan km mbunge km spika siasa inataka nn raia ni wanahitajia nn anajitambua mno mola amsimamie Ammyn🤲
@darvie7653
@darvie7653 Жыл бұрын
Hongera sana mheshimiwa ,hongera sana dada salama. ⚖️🥂
@mohamedismail2662
@mohamedismail2662 Жыл бұрын
Doctor Tulia kachapa Kiswahili tu watumwa wa lugha za watu bila shaka mmejifunza kitu hapa
@adkajisi4536
@adkajisi4536 Жыл бұрын
You know what, so as ,maybe
@musabarnabas7628
@musabarnabas7628 Жыл бұрын
Na ukimsikia anaongea Kiingereza utapenda. Kimenyookaaaa. Sa msikilize Lema akitoa mchango. Viingereza viingiii halafu havijanyookaa. Nampenda sana Lema ila kwa hili huwa ananikwaza. Mtu mwingine namkubali kwa hili ni Hayati Rais Mkapa. Kiingereza chake kilinyookaaa na kiswahili pia kilinyooka. Akiongea Kiswahili hachomekei kiingereza. Na akiongea Kiingereza utapenda. Wanasiasa wote kama kioo cha jamii wajitahidi katika hili. KiswaKinge kimepitwa na wakati; ni ishara ya kukosa umahiri katika lugha.
@msafirikilongo7429
@msafirikilongo7429 Жыл бұрын
Congratulations h/ Tulia we love u mamaa!!
@gatimarwa7525
@gatimarwa7525 Жыл бұрын
Tuliosoma Loleza m-like apa tumetoa spika bwana na anareflect maisha tuliyoyaishi loleza....say ayeeeee
@samsonmwakikuti5318
@samsonmwakikuti5318 Жыл бұрын
Uko vizuri sana , unajibu hoja kikamilifu madam!
@rehemarwanda6039
@rehemarwanda6039 Жыл бұрын
I love Dr Tulia.....♥️
@bernadetamodest6170
@bernadetamodest6170 Жыл бұрын
We love Dr Tulia👍
@cosmasj3597
@cosmasj3597 Жыл бұрын
Tusaidie kumleta Padre Dr. Charles Kitima
@mr.yahzadochuno7914
@mr.yahzadochuno7914 Жыл бұрын
I love tulia na kweli ametulia
@essanfesto3049
@essanfesto3049 Жыл бұрын
Hongera sana dada
@mzizirashid709
@mzizirashid709 Жыл бұрын
Babu zetu walikuwa Wanakula Majani Mengi Muheshimiwa Mengine Hamuyatakagi 🤣🤣🤣😍😍😍
@mozasaid3869
@mozasaid3869 Жыл бұрын
Spika Tulia Jackson 💪💪💪❤❤❤
@rosenamilia4140
@rosenamilia4140 Жыл бұрын
Salama Jabir,poker MAONO toka kwa Mh.Spika Tulia Acksson,SALAMA MARATHON.Iliyobaki ni wewe kuyatendea haki maono hayo.
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 Жыл бұрын
Good talking Dr Tulia
@christinaabel4236
@christinaabel4236 Жыл бұрын
Nampenda Sana dada tulia.! Mungu akulinde dada!!
@johnmwandu2116
@johnmwandu2116 Жыл бұрын
11:56-12:30, 😂😂, hiyo sehemu mheshimiwa umenichekesha Sana, hao ni waheshimiwa wa zamani waliona hakuna mwingne wakuwatoa, wanataka kusalimiwa kwa kuinamisha kichwa
@mshanatheblacksmith
@mshanatheblacksmith Жыл бұрын
Yaani huyu mama yupo vyema full Kiswahili speaking hata neno moja la kingereza hamna mzalendo kweli😂
@buberwadeus3158
@buberwadeus3158 Жыл бұрын
👏👏👏
@christinaabel4236
@christinaabel4236 Жыл бұрын
Nakupenda Sasa dada Tulia Mungu akulinde
@sadamhsn7078
@sadamhsn7078 Жыл бұрын
aaaa mamaa uyoooo
@mkaapwekekariakoo6417
@mkaapwekekariakoo6417 Жыл бұрын
KinolewachoHukata,😊😊
@didakalaule7840
@didakalaule7840 Жыл бұрын
🥰🥰🥰
@jumawaziri8501
@jumawaziri8501 Жыл бұрын
@salama, kwani siku hizi kipindi hakina chakula au samaki samaki wameingia mitini ???
@ahazinelson6351
@ahazinelson6351 Жыл бұрын
Viongozi hawali kila mahali
@justinendizeye714
@justinendizeye714 Жыл бұрын
This is a big woman de Tilia💪💪👌
@bernadetamodest6170
@bernadetamodest6170 Жыл бұрын
Salama mbona siku hzi hamna chakula? Wagen jaman
@alhmdulilah1187
@alhmdulilah1187 Жыл бұрын
Kwanini salama unavaa nguo nyeus tu kila mahojiano yako
@mashoo6781
@mashoo6781 Жыл бұрын
Fanya mpango umlete Dizasta vina
@dsimtoe7141
@dsimtoe7141 Жыл бұрын
Hongera salama
@fauziasultanikilewa7602
@fauziasultanikilewa7602 Жыл бұрын
Sodo😂😂😂
@hadijagere
@hadijagere Жыл бұрын
Mi nilikuwa najuwa Dr tulia ni mwanaume😁
@georgedaniel4962
@georgedaniel4962 Жыл бұрын
Hahahaha pole.
Smart Sigma Kid #funny #sigma #comedy
00:26
CRAZY GREAPA
Рет қаралды 20 МЛН
路飞太过分了,自己游泳。#海贼王#路飞
00:28
路飞与唐舞桐
Рет қаралды 15 МЛН
Опасность фирменной зарядки Apple
00:57
SuperCrastan
Рет қаралды 8 МЛН
Cool Items! New Gadgets, Smart Appliances 🌟 By 123 GO! House
00:18
123 GO! HOUSE
Рет қаралды 17 МЛН
Salama Na WANA SE6 EP75|  PART 1 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460
24:30
Salama Na Masoud Kipanya
52:05
YahStoneTown
Рет қаралды 13 М.
Intimacy // Honest Tea Talk | Season 1 Episode 14 (Season 1 Finale)
27:48
Summer shower by Secret Vlog
0:17
Secret Vlog
Рет қаралды 9 МЛН
😬 Мам Дай Хлеб 🍞 #shorts
0:38
AOneCool
Рет қаралды 1,5 МЛН
НИЧЕГО СЛОЖНОГО
0:21
KINO KAIF
Рет қаралды 3 МЛН