Sizonje - Mrisho Mpoto ft Banana Zorro (Official Video)

  Рет қаралды 1,067,960

MrishoMpoto

MrishoMpoto

Күн бұрын

Nyimbo Mpya ya Mwaka 2016, Sizonje.
[Kibwagizo - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
[Bridge - Banana Zorro]
Tulikaa barazani, tukasikia kelele
Kelele toka ndani, mtu anaruka dirishani
Sizonje, karibu nyumbani kwetu
Uone maajabu ya nyumba yetu
[Verse 1 - Mrisho Mpoto]
Karibu sana Sizonje, hii ndo nyumba yetu,
Tulipoficha mundu za kupondea wezi,
Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya?
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne,
Vitatu havifunguki, kimoja hakina mlango,
Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili,
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea,
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni,
Huna haja ya kwenda kule, kumejaa mafundi wa kupika
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako
Wanashangaa mbona ghafla
Samahani sana mgeni
Wapishi wameniomba kwamba
Nikuulize tena kwa kukuomba kwamba
Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje
Sizonje chumba hiki naomba usiingie
Ukimaliza nitakwambia kwanini
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa
Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa
“USIYEMTAKA KAJA”
Hatukuwahi kuelewa maana yake
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia
[Chorus - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
[Verse 2 - Mrisho Mpoto]
Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto
Na kamwe mtoto hawezi kuungua
Kwa kiazi kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi
Njoo huku uone Sizonje
Si unajua, harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue?
Sawa, Sizonje, huu hapa ni ua
Lile pale ni shimo la taka
Na kile pale ni choo
Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi
Wanaoishi humu ndani hawajawahi kutupa taka
Wala kwenda chooni
Kama ukiwa makini
Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu
Wengi ni vijana, wana bahasha za khaki mikononi
“KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?”
Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje
Kuna watoto, wazee na kina mama
Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele
Ninavyosikia, ila sina uhakika
Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao
Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki
Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni
Uone maajabu mengine ya nyumba hii
Sizonje, ukiona tembo anaringa
Ujue mvua zinakaribia
[Chorus - Banana Zorro]
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu

Пікірлер: 422
@davisnyandindi4917
@davisnyandindi4917 Ай бұрын
2025 huu mwaka tunategemea sana nyimbo zako,,, ganga like nying km mpo pamoja na mimi
@kombakomba7922
@kombakomba7922 3 жыл бұрын
Nyumba ni nchi,kwa nje inatafsirika na kuonekana ni maskini ila ndani ina utajiri mkubwaa,ila inaibiwa na manyemera wanaopita njia za panya kuiba rasilimali zetu, pia undugunization kwenye ajira ni tatizo,afya za kina mama na watoto,uchumi,rushwa na uwajibikaji ila sizonje ushafika umekomesha hayo yote. Hongera sana sana Mrisho na hongera kwa Sizonje.
@Richplumbing11
@Richplumbing11 3 жыл бұрын
Leo ndio nimeielewa atari sana uyu jamaa
@tengezashemisea1787
@tengezashemisea1787 2 жыл бұрын
Hongera mrisho, ila bado mwendo hujaumaliza endelea kuwa kumbusha wenye dhamana , hakika bado tunakuhitaji.
@alvinmuthui
@alvinmuthui 2 жыл бұрын
Elenzea zaidi tafadhali
@المهلهلالحراصي
@المهلهلالحراصي 2 жыл бұрын
duuuuuuh kumbe ndo nimejua leo hii maana ya wimbo huu
@bonfacemark9048
@bonfacemark9048 2 жыл бұрын
Asante kwa tafsiri yako ndugu from 🇰🇪 🙏
@mariammalendeja370
@mariammalendeja370 Жыл бұрын
nyimbo hii ulimuimbia maghufuli nae akaskia sauti yako akawaadhibu wadhalimu hadi wakaanza kupitia mlangoni r.i.p maghufuli tutakukumbuka milele
@VictorMligo-t9c
@VictorMligo-t9c 11 ай бұрын
Ila mpoto I nyimbo nimekuja kuelewa leo trh 5-3-2024😂😂😂
@Gbril45
@Gbril45 11 ай бұрын
Inamaanishi nini kwani? Mimi bado naangaika
@SalvatoryKayinga
@SalvatoryKayinga Ай бұрын
Hongera kijana
@FanuelJoel
@FanuelJoel 25 күн бұрын
Mm cjaelewa bado
@stephanokigosi656
@stephanokigosi656 3 жыл бұрын
huu wimbo ulikuwa special to MAGUFULI..Rest in paradise our icon 🕯🕯😭😭
@allyhussein516
@allyhussein516 5 жыл бұрын
Bila akili ya ziada kwa mrisho mpoto hutoki na kitu njooni tuungane jaman gonga like hapa kama umeikubali hii
@upendorealestateagentintan190
@upendorealestateagentintan190 Жыл бұрын
Mjomba Tanzania imekumiss sana. Tunaamini bado unatupenda yapo mengi tunahitaji utusemee hasa ktk wakati huu.
@SalvatoryKayinga
@SalvatoryKayinga Ай бұрын
Tangu apewe kipande cha keki saut haitoki tena
@jodasonudavis1131
@jodasonudavis1131 8 жыл бұрын
MLANGO UPO WANAPITA MADIRISHANI.... ..kwamba Kuna utaratibu wa kufikia jambo fulani Ila watu hutumia njia za mkato(rushwa) kupata jambo hilo.....SHIMO HALITUPWI TAKA WALA HAWAENDI CHOO... maana yake Kuna mfumo wa watu kustaafu Lakini Kuna watu hawaachii nyazifa na pia kuna kazi fulani hivi zimekuwa za koo fulani wanarithishana kutoka kwa baba then mtoto hatimae mjukuu mfano(benki kuu) na hivyo kusababisha vilio vya vijana wengi wasomi kuzunguka na bahasha kwa kutafuta ajira na ajira hamna.......This is the best literature song I ever meet. Good work for this guy
@martinnsuhuje4391
@martinnsuhuje4391 8 жыл бұрын
Asante kwa kufafanua kidogo nadhan umesoma kiswahili vzr
@jodasonudavis1131
@jodasonudavis1131 8 жыл бұрын
Sikuachwa nyuma sana katika fasihi
@davidomemu471
@davidomemu471 8 жыл бұрын
Nakubaliana nawe Jodasonu kabisa, the best oral lit, of modern time, big up MPOTO.
@khadijambuta4360
@khadijambuta4360 7 жыл бұрын
Jodasonu Davis yani huko benk kuu ndio ucseme watu wapitishana tu msemo wao hpa kaz tu
@doreenmalesi6039
@doreenmalesi6039 6 жыл бұрын
Asante kwa kunifafanulia
@patrinraura1397
@patrinraura1397 3 ай бұрын
Hakika huyu ni Artist❤ mbobevu na gwiji la Mashahiri yaliyosheheni Ujumbe mzito kwa Jamii Ni style ya Wimbo usio na Vionjo vya Tamaduni za nje Wimbo huu umebeba maisha yetu kupitia mila,desturi na Tamaduni zetu Hongera Msanii Mwamba Mrisho Mpoto
@jimmyfredmwanswaswa4562
@jimmyfredmwanswaswa4562 3 жыл бұрын
Tutolee nyimbo nyingine nzuri kama hii Mrisho! Asante kwa kutufundisha Kiswahili na utunzi! Mashairi Yako natamani watoto wetu wayasome shuleni!
@phillies846
@phillies846 8 жыл бұрын
Mrisho mwalimu wako wa kiswahili alikuwa anapata shida saana kwa kukosolewa na wewe 🙏🏽 amen
@merryn4891
@merryn4891 6 жыл бұрын
😀😀😀😀
@ssur5797
@ssur5797 6 жыл бұрын
Nampnda mpka bac huyu kaka mola ampe umri mrefu wenye kheri ishllh
@catenzeki678
@catenzeki678 5 жыл бұрын
@S Sur AMINA
@solangeramadhani4038
@solangeramadhani4038 Жыл бұрын
Duuuh miaka nenda miaka rudi leo ssa ndonimeelewa maan ya huu winbo
@josephseleman7780
@josephseleman7780 4 жыл бұрын
Kama unamkubari mrisho mpoto gonga like hapa
@kenneth.m.siwale9699
@kenneth.m.siwale9699 6 жыл бұрын
Mjomba Mpoto utaniwia radhi kwakweki mjomba uliwahi kuniliza enzi za awamu ya nne ya Mzee wetu Dr. wa Ukweli wa Msoga, niliwahi kulia na kucheza sana pala LUGOBA!ulikuwa wimbo Adela,na Sasa hivi SIZONJE huu si tu ni wimbo ni FASIHI KALI!!!!. Wewe kweli ni aina ya akina Shaban Robart
@mhonamisaomar7011
@mhonamisaomar7011 8 жыл бұрын
ukiisikiliza mankini itailewa 2..hongera. mjomba coz umenifanya ninitulie xanaa kukusikiliza Na kufafanua..wakuache jomba..nakusikiliza. mwana Kenya nikiwa saudia nimetua mankini..
@kenneth.m.siwale9699
@kenneth.m.siwale9699 6 жыл бұрын
Pamoja na hayo mjomba Mpoto,leo hii nikiwa natokea kwenye kilele cha sherehe ya kilele cha miaka mia moja ya vita kuu ya Dunia ya kwanza! Mjomba Mpoto nimelazimika kutumia au kuiba jumbe zako hizi kwa mapenzi na ujumbe sahihi kwa wakati mwafaka hasa hapa kwetu Zambia!
@rosenamilia4140
@rosenamilia4140 2 жыл бұрын
Sizonje ni jina la HAYATI JOHN POMBE MAGUFULI,alilopewa na Ndugu yetu msanii Mrisho Mpoto.Nyumba ktk wimbo huu ni IKULU YA RAIS MAGOGONI Dar es Salaam.
@JoshuaLyalukilo
@JoshuaLyalukilo Ай бұрын
Wimbo huo ni wazamani mno hata kabla ya huyo magufuli hajajitambua kabisa
@Yana_queen1
@Yana_queen1 Ай бұрын
@@JoshuaLyalukiloAliutoa wakati magufuli ndo kaingia madarakani…nyumba ina vyumba 4 means awamu nne Usiyemtaka kaja (Magu km Magu)
@thedoctor8301
@thedoctor8301 8 жыл бұрын
SIKU ZOTE MWENYE HEKIMA HANUKI MDOMO NA MWENYE AKILI HASEMI NDANI YA MAJI.... HESHIMA KWAKO MR MPOTO NATAMANI NIJIFUNZE ZAIDI TOKA KWAKO.
@msafirisalehe563
@msafirisalehe563 8 жыл бұрын
Kama umesoma sana vitabu vya Hayati Shabani Robert,hakika hutokuwa na kazi kubwa ya kumuelewa Mpoto.
@nyabisemaro2095
@nyabisemaro2095 7 жыл бұрын
Mrisho Unajitahidi sanaaaa kusema kweli nazipenda nyimbo zakooo hasa Sizonje,kitendawili,nikipata nauli,Waiteee nk
@bakarikimea4711
@bakarikimea4711 2 ай бұрын
Ila huyu mzee phana nasikilizaga nyimbozake lakn hii mh katumia methali tupu aisee safisana
@ezrambilinyi6788
@ezrambilinyi6788 3 жыл бұрын
Mhhh ngoja niseme ukweli tuuu. Ni miaka 3 now nasikiliza nyimbo za huyu jamaaa cjawai elewa anae elewa anielekezeee
@Catherinemichael1995
@Catherinemichael1995 3 жыл бұрын
Amemaanisha kuwa nchi inaonekana masikin wakati ndani yake inautajir tena amemaanisha sheria ipo lkn watu wanatumia njia ya mkato ameelezea mambo mengi
@eusebiusjmikongoti6625
@eusebiusjmikongoti6625 8 жыл бұрын
Nakukukubali sana mtaalamu Mjomba, kazi zako huwa zina nipa shida kuzielewa lakini huwa nakuelewa taratibu. Ninahisi hakuna kazi niliyowahi kukuelewa kwa 100% maana kila nikirudia kusikia wimbo fulani huwa naongeza kitu fulani kutoka humo! Wewe ni Shaaban Robert wa pili kwakweli, yapasa nawe uandike kitabu cha KUSADIKIKA kama mzee Shaaban, sijui utakiita SIZONJE....., au NYUMBA YETU!
@DoubleDlyrics-v7k
@DoubleDlyrics-v7k Жыл бұрын
Dah!!na mkubali sana mrisho miaka 7 imepita nasikia wimbo huu ila leo ndo mmeelewa sahihi ya wimbo huu
@mwangacharles8474
@mwangacharles8474 8 жыл бұрын
Kaka hongera sana kaka, nimeielewa sana nyimbo hiii, hasa choo kipo lakini hakitumikiiii. Unatisha kaka.
@Nairobipicturesstudios
@Nairobipicturesstudios 3 жыл бұрын
Alaaah! Mrisho wanidekua kwa mishororo na ushairi wako kila tungo lanijenga ajabu. mie nasoma sana fan wako mpya hapa toka Kenya.
@mabudaissere2295
@mabudaissere2295 11 ай бұрын
Ana kiazi cha moto mdomoni ataimbaje sasa
@abukiczan6600
@abukiczan6600 8 жыл бұрын
Mwenye akili ndogo hawezi elewa nyimbo zako but wewe ni zaidi ya msaniu hapa afrika na natamani siku nikukumbatie kwa furaha. U are the best mjomba
@fatmafetty4117
@fatmafetty4117 5 жыл бұрын
Sizonje naipenda mnoo sichoki kuiangalia wallah love u bro mrisho ❤️❤️❤️❤️❤️ kazi nzur sanaaaa👌👌👌👌👌👌
@fatmafetty4117
@fatmafetty4117 5 жыл бұрын
@@rashidikufinyu444 pouwa
@johnambrose7223
@johnambrose7223 Жыл бұрын
Siku hizi mrisho mpoto haimbi tena
@valentinesyekeye6846
@valentinesyekeye6846 2 ай бұрын
Asali ni tamu mkuu
@bwakilamychanel5951
@bwakilamychanel5951 5 жыл бұрын
sizonje hii ndiyo nyumba yetu ingia uyaone hapa anaizungumzia tz yetu jinsi watu wanavyopenda rushwa na kurisishana madaraka na wakat kila mtu ana haki
@johannesshornest4916
@johannesshornest4916 9 жыл бұрын
we unayesema amealibu au angemuonesha sizonje auna uelewa kumbuka wimbo uu ni fumbo akikuonyesha sizonje utaelewa yeye mpoto anatupa mtiani tumjue sizonje ni nani kua mwelewa sio unakulupuka kuongea tu au unadhani mpoto ni sawa na wale wa mpenzi nakupenda
@bitaetenge3989
@bitaetenge3989 8 жыл бұрын
Johanness Hornest Mbona hote mnabaki jujuhu majela yamejengwa lakini wafisadi wakubwa ambao wangefaha watupwe na kuozea huko kama kinyesi kinavyo hozea chohoni awatupwi huko. Wasomi wanaho maliza awapewi kazi wanashinda waki zunguka mahogisini lakini awapati milango. Sizonje niserekali na nyumba ni inchi. Sio Tanzania tu Africa yote.
@rumbikamachumu3292
@rumbikamachumu3292 9 жыл бұрын
one of the best video and nice message to Tanzanian. kazi nzuri Mjomba endelea kuelimisha ,kufundisha na kukosoa jamii
@ernestshaha1932
@ernestshaha1932 5 жыл бұрын
Huu wimbo nimeusikiza Mara 7 sai Mjomba juu wimbo unamafundisho saana
@saidbarawa9096
@saidbarawa9096 5 ай бұрын
Mrisho shujaa shujaa shujaa,saluti kwako,mimi ni mkenya anaefurahia kazi yako nzuri mungu akubariki
@barackolgeno1076
@barackolgeno1076 8 жыл бұрын
this guy is marvellous... your Tanzanian fan from Australia
@samwelmkondo10
@samwelmkondo10 7 жыл бұрын
We are together
@augustinomkongwa5444
@augustinomkongwa5444 5 жыл бұрын
Usiyemtaka kaja, sizonje huyu huenda akawa ni JPM aka Jembe aka Chuma cha Pua, siyo lazima niwe sahihi kumtambua Sizonje kwenye ghani hii ya Mrisho
@FredySokolo
@FredySokolo 8 ай бұрын
Kiongozzzz unajua sana ,sasa sijajua umesoma kiswahili sana au mimi ndio btplms
@zulferabour607
@zulferabour607 5 жыл бұрын
Wakati leo nasom kiswahil ....mwalim wanv kantolea mfano wa mwanafasihi anaetumja lugh y fasihi kufikish ujumb ktm jamii....ndipo akntajia huu wimbo ....hap nmeelewa kwann mrisho umeamua kutmia lugha hii....hongera sana
@silassambia876
@silassambia876 4 жыл бұрын
My all time Tanzanian Artist..love from🇰🇪
@abdulhalim5950
@abdulhalim5950 8 жыл бұрын
nyimbo kamuimbia MAGUFULI kama anamgahamisha kua nchi ya Tanzania ina maajabu mfano vijana wamesoma ila hakuna ajira. aliposema. " watu huja na bahasha za kaki na kuhoji kama hamtupi taka shimoni. Pia kamfahamisha kua wahalifu waliokuwemo nchini hawaadhibiwi. mfano akiposema- " watu wa nyumba hii hawaendi chooni wala jalalani kutupa taka shimoni
@husseinhassainlugeje6042
@husseinhassainlugeje6042 7 жыл бұрын
Asante
@eliyadigasson6679
@eliyadigasson6679 5 жыл бұрын
Vr good
@salumkanju1732
@salumkanju1732 8 жыл бұрын
daah kwa sisi tuliosoma arts aisee mzee mpoto unatisha baba angu.....nakutamani san katik matumizi ya lugha na hasa lugha ya picha kikubwa zaidi ni hiyo nyumba yaudongo lakin ndani noouma!! bila shaka watanzania waliotazama video hii wamejifunza kitu, binafsi sanaa yako sio tu kiburudisho kwangu maana najifunza mengi san na ni miongoni mwa mhimili wa utamaduni wa nchi yetu! unaimba kwa kusoma upepo unavyovuma ila ulituomba nauli ili uwende kwa mjomba na je sizonje ni naniiiiiii?
@JosephatJuma-dj5tq
@JosephatJuma-dj5tq 8 ай бұрын
Mjomba hapa Kenya unapendwa kakangu
@Franko-zd6hc
@Franko-zd6hc 3 жыл бұрын
Huu ni usanii wa hali ya juu.Utumiaji wa kejeli ilikupeana ujumbe flani.
@rashidhassankadege1455
@rashidhassankadege1455 4 жыл бұрын
Yaani nyumba yetu kwa nje ni mbaya sana nayakizamani mno ila ukiingia ndani ndo utajua uzuri wake najinsi ilivonakshiwa kwa mapambo ya gharama na ustaarabu uliotukuka
@ramadhanboi6485
@ramadhanboi6485 4 жыл бұрын
Imemaaanisha mbuga za wajama na dhahabu tulizonazo na maziwa
@ramadhanboi6485
@ramadhanboi6485 4 жыл бұрын
Imemaaanisha mbuga za wajama na dhahabu tulizonazo na maziwa
@isackyakobo7829
@isackyakobo7829 4 жыл бұрын
Asante sizonje, Kwa sasa wenye nyumba tunalala vyumban piah, Magufuli Oyeeee! Bahasha za kaki tu ndo bado ila karbu tena 2020, ulitatue na hlo! Kwa sasa hawapt madrishan tena,
@richardjuma7708
@richardjuma7708 4 жыл бұрын
Hatari sana
@williammwajeka3347
@williammwajeka3347 9 жыл бұрын
"Najua, wimbo mbaya haufai kumbelezea mtoto, Na kamwe mtt hawez kuungua kwa kiaz kilichokua kweny kiganja cha mama yake mzazi, Njoo huk uone sizonje Siunajua, harufu ya uzaz haiish mpk mtt akue? Haa haa haa daahh mpoto unaandk xn, hongr xn kwa uandsh Mzur, nazkubal xn nyimbo zko ✋✋✋✋
@IrineKimaro
@IrineKimaro 8 ай бұрын
Mjomba tumemiss mashairi yako, come back legend
@davidomemu471
@davidomemu471 8 жыл бұрын
Mjomba, kwa kweli nyumba za Africa mashariki zina mambo na maajabu, zaidi hapa Kenya.
@emmanuelmsambya5293
@emmanuelmsambya5293 9 ай бұрын
Hii nyimbo iliimbwa na watu wenye IQ kubwa
@enockjohn332
@enockjohn332 9 жыл бұрын
mtoto hawezi kubembelezwa kwa wimbo mbaya,na mtoto aungui na kiazi kilchopo kwenye kiganja cha mama yake,nimekusoma mjomba
@lightnessmruma9740
@lightnessmruma9740 9 жыл бұрын
nmeelewa kidogo,anamkaribisha maguful ikulu(nchi yetu)....asiye mtaka kaja hahaha I like this ....japo mafumbo n mnge
@ivanmutwol
@ivanmutwol 4 ай бұрын
A true Patriot, maisha marefu
@SostenesMasawa-ls1eo
@SostenesMasawa-ls1eo 4 ай бұрын
2024 eeeeeh 🔥 "MASTERPIECE"
@edwinpepela1205
@edwinpepela1205 6 жыл бұрын
Shairi,malumbano.african setting, traditional and meaning,economical failure.Kiasi hakiwezi mchoma mwana kikiwa kikanjani Cha mama.pili mtoto hajakuwa Hadi harufu Cha babake kiishe.Hehe if you not an African don't try to pea in that setting.You will meet with stonishment.always remember that.
@aminagoliama8668
@aminagoliama8668 9 жыл бұрын
Weng ni vijan na wanabahasha za kaki mikonon daaaaah nimeelewa sana nakupend sasa mpot ii ndo nyumb yetu TZ ingia uyaone Kile ni choo wanaoish hawajawai kukitumia mean hospital zipo ila wanaenda nje hahahahahahaha 😍💞💕😘💜👏👏👏
@marwa2862
@marwa2862 2 жыл бұрын
2022 kama Bado unamkubali Mrisho gonga Like . Much Love from Kenya. 🤔Humu ndimo tulimoficha Mundu za kubondea wezi!!!! Na jumba hiki Usiingiye kamwe🤔
@anitaphilip2070
@anitaphilip2070 9 жыл бұрын
upenda Wangu nimependa kilakitu wanao sema sinzuri wajaribu nawao tuona zao zitakuaje
@ibrahimzuberi1029
@ibrahimzuberi1029 8 жыл бұрын
yan nimeskiliza zaid ya 10 tym sijaeleza zaid ya bahasha za kaki2...daaah shkaaaaamooooo burazaaaaa
@kedmondkepha7707
@kedmondkepha7707 6 жыл бұрын
Daaaaaaah mjomba ulisomea wapi kiswahili chako maana hayo mashairi yako hakuna anaeyaweza duuu big up sana mziki wako ni wa kibantu zaid
@wilhardjohn8287
@wilhardjohn8287 9 жыл бұрын
huyu hanscana ni director anayejielew pengine kuliko wote kwa sasa young but a real inspiration in music industry
@abbouramsey154
@abbouramsey154 9 жыл бұрын
Apo Godfather au nenene? bonge la kichupa straight to Urban top Ten
@nyabisemaro2095
@nyabisemaro2095 7 жыл бұрын
Wana fasihi tupo tunakuewaga sanaaaa Asante MWL wanguu wa kiswahili MWL MACHUMU, MWL Alexander na PRISCA Bila nyie mm nisingejuaaa ujumbe wa mpoto Mbarikiwe sanaaa
@amosnguvumali7869
@amosnguvumali7869 8 жыл бұрын
hahaha kwel mtoto hawez kuungua kwa kiaz kilichopo kwenye kiganja cha mama yake ahsante sana
@mwitaadah3649
@mwitaadah3649 4 жыл бұрын
Mjomba umetulia Sana. Tupe mashairi baba🔥
@mohdkhalifa8828
@mohdkhalifa8828 5 ай бұрын
Hekima kaka safi sana
@emmanuelpeter7371
@emmanuelpeter7371 9 жыл бұрын
Kaka mungu akujalie utufunze mengi kwakupitia nyimbo zako maan nakuelewa pale unapo tohoa maneno yalio sirin
@aliali189
@aliali189 9 жыл бұрын
napenda sana nyimbo za mlisho video kali sana
@Tutankhamun-s3n
@Tutankhamun-s3n Жыл бұрын
Nyimbo ngumu sana kuielewa inahitaji utulivu wa kutosha
@tiaschris7070
@tiaschris7070 8 жыл бұрын
aisehhh hii nyimbo ni hatari, xijui km ntakuja kuisikia nyimbo km hii tena
@mwalimmaroaibrah8051
@mwalimmaroaibrah8051 8 жыл бұрын
Dah! Kwakweli mashairi yamesimama sana. Hongera Mrisho kwa mashairi haya
@dorcasgitari8278
@dorcasgitari8278 8 жыл бұрын
Nimeingia nami nimeyaona maaaajabu ya nyumba yenu I say...great poetical pieces. Wengi waaalewa maaana ila kwa vile ina wachoma basi wanajifanya kutoelewa I say. He heeeeee.
@juniorlangen2648
@juniorlangen2648 3 жыл бұрын
Wewe ni mwalimu , kazi zote zako hujawahi kosea
@masirian06
@masirian06 3 жыл бұрын
nazipenda kazi zenu safi sana wanaTanzania... mwatufunza maadili mema ya upendo sis kama wakenya lakini wote tu waafrika na hivyo nafurahia kazi zetu,, hongera sana
@ibrahimjuma8577
@ibrahimjuma8577 9 жыл бұрын
hongera Mjomba mi huwa nakuelewa sanaa nice song babaa
@christopherkipeke7547
@christopherkipeke7547 8 жыл бұрын
Mlisho kwangu hata usipoimba, kitendo cha kukuona nahisi nguli na gwiji la sanaa anajambo analitoa
@alfredally1955
@alfredally1955 4 жыл бұрын
Tanzania inaonekana masikini ndani nitajiri hyo ndio jambo nimeona
@barick
@barick 8 жыл бұрын
Huyo mzee anavyo Lia na mimi nimelia mmh!sizonje
@iamjimba9775
@iamjimba9775 9 жыл бұрын
duuh! maishairiii nondo sana
@sirialemmy37
@sirialemmy37 9 жыл бұрын
hehehe yes yes mr
@kihanda2554
@kihanda2554 9 жыл бұрын
Long live Mrisho mpoto. Nimekuelewa vzr mnooo. Mfumbie mtoto mkubwa ang'amue
@hermanngaiza9327
@hermanngaiza9327 9 жыл бұрын
Kiukweli wimbo umetulia una ujumbe wa maana sana.ukionesha kwamba tuwe na nguvu na kupambana ahsante brother Mpoto
@leonardcharles3169
@leonardcharles3169 9 жыл бұрын
video ni nzuri, tuendelee kumpigia kura tuzo ya kola! wonderful video,
@sirialemmy37
@sirialemmy37 9 жыл бұрын
Yes Leonard!
@neykapoor5871
@neykapoor5871 2 жыл бұрын
Artist is more beautiful because one thing can bring different meaning and understanding as what it is in this song of. Sizonje salute mrisho mpoto
@Boazmosses8204
@Boazmosses8204 8 жыл бұрын
kwamba kwa nje inaonekana kkukuu lakn ndani imejaa vitu vya thamani😂😂😂😂tz hyo
@emmanuelpeter7371
@emmanuelpeter7371 9 жыл бұрын
na kinachonifuraisha sana kwako ni pale unapotohoa neno ;linanifikirisha kutafuta maan yake nn yaan hua unaniparaha sana na ninatumia akili kujua unamaan gani yuu ya usemi wako kuanzia mjomba hadi leo zizonjee daaah kweli hii ndo nyumba yetu ina milango lakin watu wanapitia madirishan tena ulinimaliza pale ulipo sema wagen wanalala chumban wenyej seblen daaah hii ndio nyumba yetu ni kweli kaka endelea kutohoaa
@sirialemmy37
@sirialemmy37 9 жыл бұрын
Emanuel Peterrrrrr kumbe wa2 wamo wa kuitafsi mafalsafa magumu? sikujua bwana. Amazing my country man!
@ephraimkagungu6050
@ephraimkagungu6050 9 жыл бұрын
Oooh Woookey Burhoney Wa Mponda Ha Hha Somehow Umenipa Idea
@hadijapazia8255
@hadijapazia8255 4 жыл бұрын
Naikubali xn hii ngoma🔥🔥🔥🔥👌🏻👌🏻👌🏻👌🏻
@cunada712
@cunada712 5 жыл бұрын
Mwanafasihi bora niliyemshuhudia maishani mwangu kwa sasa sijaona kama huyu🙌🙌
@vintankirikuu1103
@vintankirikuu1103 2 жыл бұрын
Mwngne madebe lidai just find Tanzanian artist
@saknamtaki8168
@saknamtaki8168 8 жыл бұрын
Nyimbo nzuli kweli uko posh kak kimziki nakupa respect
@muddysimba887
@muddysimba887 5 жыл бұрын
Yuliopo hapa 2020 tupia like
@ezekielbituro7969
@ezekielbituro7969 9 жыл бұрын
nimeilewa asee...mashairi yanaeleweka kiasi! HII NDO TANZANIA
@ibrahimwilliam8127
@ibrahimwilliam8127 9 жыл бұрын
MCHAWI WA VIDEO BONGO ONCE AGAIN #HANS MWENYE NJAA ZAKE NA HAWEZI KUKUKANA.. VIDEO KALI
@jovituskamugisha
@jovituskamugisha 9 жыл бұрын
Maudhui, mashairi, rekodi,... Nimeipenda. Ahsante sana Baba Mrisho Mpoto.
@NabakiZanzibar
@NabakiZanzibar 9 жыл бұрын
Natamani sana kuona hii video on MTV, Trace, ect. coz idea na shots zimetulia sana. Nashukuru sana kwa mashaili (Poetry) #MrishoMpoto kazi nzuri sana. Mungu akubariki, iposiku wataelewa tu.! @ThomGypsy #ThomGypsy
@kingimiwani3440
@kingimiwani3440 4 жыл бұрын
kiukweli hii nyimbo huwa ninaipenda . sana
@gospelman3720
@gospelman3720 3 жыл бұрын
Mmmmmmmh huu wimbo aliimbiwa JPM
@clementsanga
@clementsanga 9 жыл бұрын
bonge la kazi kaka na kwa upande wa video ipo poa ile mbaya.
@eliatalented7592
@eliatalented7592 5 жыл бұрын
Who else is still here in 2019
@antoinettetony3038
@antoinettetony3038 8 жыл бұрын
jameni ndugu zungu.samahani alie elewa, atueleweshe wimbo ulikua Una zumguzia nini, kwani mi apa sielewi
@christinewomanoffaith5479
@christinewomanoffaith5479 8 жыл бұрын
Antoinette Tony una mambo mengi sn anamkaribisha Rais ikulu(kwny hiyo nyumba) aone matatizo yaliyopo.... anaongelea tatizo la ajira kwa vijana(bshasha za khaki) anaongelea nchi ilivyo na vitu vya thamani(umeona ndani nyumba ni nzuri sn) nje mbaya ,watu wake wanaishi kwa shida...wanalala sebuleni.... milango ipo lkn wanaingilia dirishani,rushwa,njia za miato! ....nk
@ibrahimmakame5304
@ibrahimmakame5304 5 жыл бұрын
jamaa kaacha kuimba nyimbo za harakat utawala magu kavaa viatu mrisho mpoto
@MishenOnMission
@MishenOnMission 2 жыл бұрын
Mbona mrisho haimbi tena..
@hamidmpenja2489
@hamidmpenja2489 8 жыл бұрын
ishara ya muafrika ni kioo kimulikacho na kirudishacho taswira ya uafrika na tukajivunia kama waafrica,I salute brazza,napendaga sana mashairi yako!!!
@sonnymjeshi
@sonnymjeshi 8 жыл бұрын
adams boytz
Mrisho Mpoto - Waite ( Official Video HQ)
5:24
MrishoMpoto
Рет қаралды 820 М.
MKE WA BOSS ANAKUTAKA KAMA HIVI WEWE UNGEFANYAJE
14:33
Mweusi Family
Рет қаралды 298 М.
СИНИЙ ИНЕЙ УЖЕ ВЫШЕЛ!❄️
01:01
DO$HIK
Рет қаралды 3,3 МЛН
Try this prank with your friends 😂 @karina-kola
00:18
Andrey Grechka
Рет қаралды 9 МЛН
Леон киллер и Оля Полякова 😹
00:42
Канал Смеха
Рет қаралды 4,7 МЛН
ASKARI MZEMBE ALIVYO ANGUKA MBELE YA RAISI, UTACHEKA UFE
8:52
Mbengo Tv
Рет қаралды 548 М.
Banana Zoro - Zoba
7:43
Swahiliwood
Рет қаралды 1,4 МЛН
Young Lionel Messi Was Actually INSANE
14:20
VSP7 FOOTBALL
Рет қаралды 462 М.
BALAA LA MRISHO MPOTO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
11:17
MrishoMpoto
Рет қаралды 61 М.
ADORABLE Kid Drummer SHOCKS the AGT Judges!
6:30
Amazing Auditions
Рет қаралды 6 МЛН
STEVE NA NDARO WALIVO VURUGA NDOA UTACHEKA
16:04
Ndaro Tz
Рет қаралды 1,1 МЛН
Boko (Official Video) - Kilimanjaro Band Njenje
7:02
Kilimanjaro Band Njenje
Рет қаралды 206 М.
Nyasuba  - Odongo Swagg (Official Music Video) sms skiza 5439079 to 811
15:11