Wafanyabiashara wafunga maduka wakimshtumu meneja TRA Handeni

  Рет қаралды 4,616

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

Wafanyabiashara wa maduka ya jumla na rejareja wilayani Handeni mkoani Tanga wamefunga maduka yao kutwa nzima wakidai kutolewa lugha za vitisho na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wilayani hapa, wakati wanapofika ofisini kwake.
Wakizungumza kwenye mkutano na kamati ya ulinzi na usalama katika kikao kilichofanyika viwanja vya Handeni Square, wafanyabiashara hao wamesema shida kubwa wanayokutana nayo TRA, ni lugha za vitisho kutoka kwa meneja na makadirio ya kodi ambayo si rafiki kwao.
Akijibu shutuma hizo, Meneja wa TRA wilayani Handeni, Venance Ephraim amesema changamoto iliyopelekea hali hiyo ni wafanyabiashara wengi kukosa elimu ya kodi na waliowengi hawataki kutoa risiti.

Пікірлер: 8
@modestwenceslaus9
@modestwenceslaus9 7 ай бұрын
Safi sana mkuu wa Wilaya kwa maelekezo yako mazuri maana huyo meneja akiambiwa akafanye hiyo Biashara na Mfanyabiashara akawe meneja wa TRA ukweli huyo meneja atashindwa na mfanyabiashara ataimudu vizuri hiyo kazi ya Umeneja.
@EdwiniMushumbusi
@EdwiniMushumbusi 7 ай бұрын
Wanakosea sana kuajiri mtu ambaye hajawahi uchuuzi
@kilogreekachananawatuwasio4054
@kilogreekachananawatuwasio4054 7 ай бұрын
Huyu kashapitiwa na makonda??? kama Risiti sasa maduka yote wafunge kwa Risiti mbona Aifanani hiyo mkuu wa TRA 😂😂 5:34
@WilsonGilbert-ut5fg
@WilsonGilbert-ut5fg 7 ай бұрын
Kiufupi meneja aondolewe hapo wilayani sababu sio rafiki na wafanya biashara sheria afate mkondo
@hurumalunda2490
@hurumalunda2490 3 ай бұрын
Nisikilizenii watanzania TRA sio tatizo tatizo ni wawekezaji wa kihindi na kichina ndio wameharibu biashara tunashindwa kusimamia bei kwa sababu Yao wawekezaji Hadi wateja wamekuwa na kiburi kutokana na uhorela wa bei zao kibiashara
@HamidaKondo-z1s
@HamidaKondo-z1s 7 ай бұрын
Muongo huyu meneja anaonesha amachoka kazi sasa naitwe makonda aje amnyooshe
@bishopjohnolenaata5581
@bishopjohnolenaata5581 7 ай бұрын
Mnatuwekea taarifa nusu mbona hivyo
@josephfrancis9943
@josephfrancis9943 7 ай бұрын
Mchawi samia mwaka huu niko kote tunaonewa wamekopa nchi inadaiwa ndo mana wanatukandamiza mm nko manyara huku tumepigwa kod kubwa sana tena uku porin samia hafai kuwa rais
UTATA KIFO CHA MTU HANDENI/AKUTWA CHUMBANI NA VIDONGE/ NDUGU WAZUNGUMZA
3:21
Cool Parenting Gadget Against Mosquitos! 🦟👶 #gen
00:21
TheSoul Music Family
Рет қаралды 32 МЛН
Kimeumana Handeni Wazee wazuia mradi wa barabara hadi wafanye Tambiko
2:56
DRAMA AT D.C.I GACHAGUA ARRIVING [GACHAGUA SURMONED BY DCI]
7:12
WAMUCHEMBE JUNIOR REALITY VIBES
Рет қаралды 48 М.
sakata lamsikiti wa kidato handeni
1:53
Ust Nurdin Hemed
Рет қаралды 2 М.