Waziri Magufuli achukua fomu kuomba Kuteuliwa Kugombea Urais kupitia CCM

  Рет қаралды 304,122

Grann Chaco

Grann Chaco

Күн бұрын

Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alisaini kitabu kabla ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu ndiye aliyemkabidhi fomu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Safari ya chama cha mapinduzi ya kupata mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao imeendelea kushika kasi baada ya makada sita wa chama hicho kuchukua fomu hii leo tarehe 04.06.2015 na kufanya jumla ya makada 11 wa chama hicho kujitokeza ndani ya siku mbili tangu zoezi hilo lifunguliwe rasmi june tatu mwaka huu.
Miongoni mwa waliojitokeza kuchukua fomu hii leo ni pamoja na waziri mkuu mstaafu awamu ya tisa Mhe Edward Lowassa mbunge wa jimbo la Monduli ambaye amejinadi kuwa hana mpango wa kushindwa na amechoka na siasa za matusi na tuhuma na kudai kuwa hiyo sio demokrasia kwa viongozi wenye nia ya kweli ya kulikomboa taifa.
Mwingine ni aliyewahi kuwa waziri mkuu wa awamu ya nane Fredrick Sumaye ambaye amebainisha kuwa endapo atapata ridhaa ya chama hicho ya kuwania urais na kushinda atahakikisha anatokomeza kabisa tatizo sugu la rushwa kwa kuunda vyombo maalum ikiwemo mahakama ya wala rushwa huku akitumia rasilimali za asili zilizoko nchini kuinua uchumi wa watanzania.
Kada mwingine aliyejitokeza ni John Pombe Magufuli ambaye hivi sasa ni waziri wa ujenzi lakini pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na ndani ya CCM kwa ufanisi wa hali ya juu ambaye yeye ametamba kipaumbele chake cha kwanza ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya chama cha mapinduzi.
Makada wengine waliojitokeza ni makamu wa rais Dk Mohamed Gharib Bilal, balozi Ali Karume na mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro Amos Siyatenzi huku makada wengine zaidi wakitarajiwa kujitokeza katika muda ambao chama hicho kimeweka kuanzia june 3 mpaka jully 2.

Пікірлер: 155
Detik-detik Presiden Turki Tiba di Istana Bogor
19:02
KOMPASTV JATENG
Рет қаралды 7 М.
REAL OR CAKE? (Part 9) #shorts
00:23
PANDA BOI
Рет қаралды 81 МЛН
Yaliyopamba kampeni za Dkt John  Magufuli katika Safari ya Ikulu
12:33
MUHIDIN MICHUZI
Рет қаралды 327 М.
Full video Dr. Magufuli alivyotangazwa mshindi wa Urais 2015
9:16
Lowassa bungeni1 3
4:43
Edward Lowassa
Рет қаралды 254 М.
HUYU NI MHE JOHN POMBE MAGUFULI 14 Nov 2013
13:38
Ikulu Tanzania
Рет қаралды 306 М.