Рет қаралды 17
Habel Chidawali- Dodoma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mpango ametoa maagizo matatu kwa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF likiwemo la kuongeza minara katika maeneo yote nchini.
Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo April 25,2024 wakati akizindua jengo la UCSAF Jijini Dodoma ambapo ameagiza pia mfuko huo kuwashirikisha wadau wengine katika kutafuta fedha.
Agizo lingine alilotoa Dk Mpango kwa UCSAF ni kuwataka waongeze vifaa vya mawasiliano mashuleni licha ya kukiri kuwa walishatoa vifaa kwa shule 1121 ikiwemo kompyuta.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameagiza Wizara ya fedha kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi ili wananchi wengi zaidi waweze kumiliki simu janja lakini viongozi wafanye kazi kwa kujali muda zaidi.