Salama Na MAJIZZO SE6 EP17 | MPIMAJI PART 2 | SendTip MPESA LIPA NO 5578460

  Рет қаралды 83,794

YahStoneTown

YahStoneTown

Күн бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
MPIMAJI
Francis Ciza that’s the name, anastahili heshima yake kwa ujasiri mkubwa ambao ameuonyesha kabla hajafika hapa alipo leo. Njia yake kwa mujibu wa haya maongezi yetu ilikua ya kulazimisha sana na yeye hakuwahi kukata tamaa, au tuseme neno au wazo la kukata tamaa halijawahi kuwa mawazoni mwake.
Majay ndo jina la umaarufu wake, Dj Majay au RDJ Majay au Majizzo moja ya ma Dj walokua wakiunda kundi la ‘Kwa Fujo DJ’s’ akiwa pamoja na Abubakar Sadique na ma Dj wengine wakati huo. Jinsi gani walikutana na nini kiliwafanya wawe na umoja huo? Tulimuuliza Majay kwenye maongezi haya na akaniambia waliona kitu ambacho hakuna mtu mwengine alikiona wakati huo na kweli kilifanya kazi.
Nini sasa kilisababisha umoja wao kuvunjika? Nini special kwake ambacho anadhani kinamfanya aendelee kuwa mwenye mafanikio na relevant kuliko wenzake? Huku sasa anatuelezea rasilimali yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu, ya KUTOKATA TAMAA. Ambayo ndo imemfanya yeye anendelee kubaki kuwa nahodha wa boti yake ambayo imeweza kupambana na dhurba nyingi za baharini na nchi kavu lakini bado inaendelea na safari.
Majay alianza kutafuta kwake kama fundi nguo, wengi tunawaita fundi cherehani, anatuambia mtaani kwake kulikua na MC mmoja wa harusi ambaye yeye ndo alikua anamshonea nguo zake na siku ambayo alimchukua Majay kwenye moja ya kazi zake ndo siku ambayo maisha ya Majay YALIBADILIKA.
Sasa ni CEO wa moja ya Radio zenye nguvu hapa Tanzania na mpambanaji ambaye anahakikisha vijana na mziki wetu wa kizazi kipya unazidi kwenda mbali, yeye ni mtu ambaye anawavutia vijana wengi kwa kuwapa matumaini kwamba kuna siku mazuri yatakuja tu, at least hiyo ndo vibe ambayo mimi naipata kwake. Ashakataliwa sana. Ashakosea sana, ashafungiwa milango sana, ashakimbiwa sana na marafiki ambao walikua hawaamini kwenye ndoto yake na amesha anza upya mara kadhaa kwa kuamini kwamba kama aliweza kukipata mwanzo, basi inawezekana kukipata tena, na hivyo ndo jinsi ambavyo ilikua na inaendelea kuwa mpaka leo hii.
Kama unahitaji inspiration au mtu wa kumtazama ndoto zake ili na wewe uweze kuzitimiza za kwako basi Francis Ciza anaweza kukusadia sana.
Tafadhali enjoy mazungumzo yetu haya ambayo yamejaa safari ndefu ya kuanzia kwenye kupima watu viuno na kifua mpaka kuwapangia watu burudani isiyochosha.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪KZbin Link bit.ly/KZbinS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 164
@NassTwin
@NassTwin 2 жыл бұрын
Aisee sijawah kumsiliza majizzo aiesee huyu jamaa ni mtu sana na mpambanaji sana. Kama tupo pamoja gonga like nyingi kwa kumsupport jamaa
@deusdedit789
@deusdedit789 2 жыл бұрын
Dah aisee nimejifunza sana sana TANZANIA ni nchi pekee ambayo mtu akifanikiwa watu wanawaza uchawi madawa bila kuangalia mahali tulikopita. Ooo Lord help us. I must work so hard mpaka siku moja nifanikiwe niitwe kwenye interview
@bahatirngulika4493
@bahatirngulika4493 2 жыл бұрын
Aiseee kumbe Tanzania iko na wanaume wenye true love,yani haumii aliyoyapitia yeye ila anaumia juu ya maumivu ya mwanamke wake!!! Aiseeee be blessed Majizo na awatunze
@tanzaniatourismboard8395
@tanzaniatourismboard8395 2 жыл бұрын
Naendelea Kujifunza Kila Siku, MAISHA Ni Mapambano na Hakuna Kukubali Kukata Tamaa. GOD Bless You MAJIZZO...Thank You Salama J
@fefenailsandmakeup1353
@fefenailsandmakeup1353 2 жыл бұрын
Majizo ana vingi ila sio mtu anaweza kujieleza sana...! All in all hongera ❤
@addeypentacos9014
@addeypentacos9014 2 жыл бұрын
This guy has a golden heart. Imagine he isn't bothered with his own personal lowest moments in his life and career but he is touched with his woman .we always complains about Tanzanians men not being gentleman but he stands as one trophy to proud of.
@elizabethhonere2931
@elizabethhonere2931 2 жыл бұрын
Majizo Mungu amekupa wisdom kubwa sanahata Eliza anayo mmekutana wa kufanana
@2116-n
@2116-n 2 жыл бұрын
Majizzo SALUTE Sana Kaka, nimegundua una IQ kubwa Sana ya maisha
@jofrasful
@jofrasful Жыл бұрын
A real-life journey with a determined heart and vision. Congrats Majizzo.
@hildaminja5148
@hildaminja5148 2 жыл бұрын
NATAMANI VIJANA wote wangefuatilia na kusikiliza hii show. Salama uko vizuri sana.Hongera Francis /MAJIZO
@gastonchonya7790
@gastonchonya7790 2 жыл бұрын
Dada mm nafuatilia
@nsazabahizirehema7897
@nsazabahizirehema7897 2 жыл бұрын
Nime fatiliya kwa umakini part 1 and 2 Asante sana kunakitu nime jifuza Allah akupe mwisho mwema na aendeley kukubariki wewe na mkeo na family kwa ujumula🙏🙏Salama ubarikiwe from 🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮🇧🇮
@damaskinkela2265
@damaskinkela2265 2 жыл бұрын
Like from 257
@namsamson3443
@namsamson3443 2 жыл бұрын
Huyu kijana ni mtu mzuri sana. Mungu aendelee kukubariki wewe pamoja na familia yako.
@johnlihawa4145
@johnlihawa4145 Жыл бұрын
The man with a big heart .......... Nimejifunza mengi sana.... Acha Mungu amshinishe aisee he deserves that
@mariamkibindo1741
@mariamkibindo1741 Жыл бұрын
💯🤝
@rithamarrow5716
@rithamarrow5716 2 жыл бұрын
Mwanaume yoyote mwenye huruma ni mwanaume ambae anajielewa sana. Majizzo ni mwema pia ni muaminifu Mungu amtunze na kumbarik pamoja na familia yake
@salomewandya7257
@salomewandya7257 2 жыл бұрын
Kabisaaa 💯
@janemuhumba5823
@janemuhumba5823 2 жыл бұрын
💯💯💯
@rossarutasha9391
@rossarutasha9391 2 жыл бұрын
Mungu akubariki sana Majjizo kumbe wewe ni mwaminifu na unampenda kiukweli mke wako mubarikiwe ktk maisha yenu
@aaaaaah290
@aaaaaah290 2 жыл бұрын
KAONA/KASIKIA LA MKE TUU 😀😀😀
@christiannyamamba9089
@christiannyamamba9089 2 жыл бұрын
Hivi vitu vinainspire sana vijana na kupitia hizi interview watu wanabadilisha maisha yao na kufungua ukurasa mpya hongera sana Salama unafanya kitu kizuri sana
@marianajohn5415
@marianajohn5415 2 жыл бұрын
Lulu unapendwa mama! Huyu ni mwanaume 🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻🙌🏻
@tunudachitalks6575
@tunudachitalks6575 2 жыл бұрын
Majizo you have inspired me so much....i know am not there yet but in shaa Allah will be there by God's grace. Salama Nakupenda sanaaa keep up the Good work 👏❤
@azinarashidi5204
@azinarashidi5204 2 жыл бұрын
Interview nzur san Mashaa Allah Mungu akujaalie baba kaka uzidi kufanikiwa zaidi ya hapo na akutunzie familia n kizaz chako Ameen,,,
@rayanndizeyes3161
@rayanndizeyes3161 2 жыл бұрын
Najikuta na lia sana Majizzo unaupendo Mungu akubariki sana nauzidi kumutuza mukewako
@hadijajumanne5493
@hadijajumanne5493 2 жыл бұрын
Unaweza ukawaambia na bado wakakuona huna mana,unaishi na watu vizuri wenzio wanakung'ong'a Kisogo bora uachane nao uwe na 50 zako tu
@Juxton
@Juxton 2 жыл бұрын
Majizzo needed 2 more episodes.
@جميلهخميس-ط5ث
@جميلهخميس-ط5ث 2 жыл бұрын
Dah kaka Anamapenzi ya dhati Huyu Mungu awasimamie hadi mzikane😭😭🙏🙏
@zuuqueenhilson3135
@zuuqueenhilson3135 2 жыл бұрын
Nice majiz umenifunz mengi mmoja wak kam unampnd mtu mpend hat awe kweny mazingiz yapi
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 жыл бұрын
Very inspirational... Majizzo is so smart. 6:55 - 7:20 📌📌📌 Keep up the good work Ace Jay...👏👏👏
@fauziayusuf235
@fauziayusuf235 2 жыл бұрын
Best interview ever........am officially a fan of majizzo❤️❤️
@zawadisalum5684
@zawadisalum5684 2 жыл бұрын
Huyu jamaa n very humble aisee he and lulu they deserve each other indeed
@HusseinSalumu-o1e
@HusseinSalumu-o1e 9 ай бұрын
Ni bonge la entervew so poa maisha safari unatakiwa uwe mmbishi nakukubali sana majizo forshizo mi binafsi sijaona dj kama wewe Tanzania nzima Yani uwezo binafsi ndio uliokufikisha hapo ulipo much respect my bro
@aminiismail3371
@aminiismail3371 2 жыл бұрын
Salama tunamuomba Kondeboy hapa please
@franknsato6373
@franknsato6373 2 жыл бұрын
Very inspirational story, hope this will motivate a lot of youth towards their life destiny, personally I'm much inspired and encouraged by your efforts, big up foxy
@abduly.snootie
@abduly.snootie 2 жыл бұрын
Aseee, BONGE MOJA LA INTERVIEW S/O TO SALAMA, KWA HILI PINDI LA KIBABE, BIG UP CHAMP MAJIZZO.✨👑💪🏾👊🏾✊🏾 🎥🎬🎞️📽️🔥🔥🔥🔥🔥
@evamday2896
@evamday2896 2 жыл бұрын
Asante sana mwenye kipindi hiki nimejifunza mengi kwa Majj
@mwalimualiaminialiamini8623
@mwalimualiaminialiamini8623 2 жыл бұрын
Nimeielewa sana hii hili ufanikiwe ni razima ujihamini kwanza wewe 🙌🙌🙌🙌
@abdulpires9091
@abdulpires9091 2 жыл бұрын
Big up na harus yko cz ata mm nimeanza kufikiria kuowa!👍
@mohamedrajab358
@mohamedrajab358 2 жыл бұрын
Nimejifunza Sana Acha niendelee kupambana mungu akupe nguvu ya kutuletea watu Wa kutueleimisha za kutufungua
@sakinamixpambe2602
@sakinamixpambe2602 2 жыл бұрын
Nimekupenda bure maj hasa hapo kwenye watoto mashallah
@prettypretty9745
@prettypretty9745 2 жыл бұрын
Interview nzuri Sana sijui kwanini nimechelewa kuiangalia majizzo ni mwanaume wa kupigiwa mfanoooo
@johnkabadi8732
@johnkabadi8732 2 жыл бұрын
Sema yule mwanamke mange anatakiwa kutafutwa na kufyatwa anapotosha Sana jamii
@khadijangozi4324
@khadijangozi4324 2 жыл бұрын
Naomba uniambie lulu ametajwa wapi
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Жыл бұрын
@@khadijangozi4324 Eliza hukulisikia jina lk
@editatairo9667
@editatairo9667 2 жыл бұрын
Inspiration kama hizi ndio tunatakiwa kusikiliza na sio zile za motivation speakers za kuchanganya akili
@ch-tvonlinegr8125
@ch-tvonlinegr8125 2 жыл бұрын
Realy
@khadijahali4837
@khadijahali4837 Жыл бұрын
🤣🤣
@flexturnertv8585
@flexturnertv8585 2 жыл бұрын
Salama we need Fred vunjabei if possible
@watsonmwanjelwa4535
@watsonmwanjelwa4535 2 жыл бұрын
we need this kind of staff salama na. great job
@yusufurahabiamu6052
@yusufurahabiamu6052 2 жыл бұрын
nimeipenda story Mungu ambariki sana
@daudgrayson8534
@daudgrayson8534 2 жыл бұрын
I like this interview nilikuwa simfahau majizo now kdg nimepata picha kuhusu yeye ni mtu wa aina gani
@yvetteuwase2740
@yvetteuwase2740 2 жыл бұрын
Tunawapenda papa G na maman G🥰🥰🥰🥰🥰🥰
@JustArkon
@JustArkon 2 жыл бұрын
Big fan of the show. Salute from Nairobi
@julietdawa5518
@julietdawa5518 Жыл бұрын
From Kenya 🇰🇪 this is very inspirational
@salumuseif3324
@salumuseif3324 2 жыл бұрын
Majizo kama ruge namkubali uyu boss
@rsautoservice984
@rsautoservice984 2 жыл бұрын
Interview smart Sana jabir.. Mardam mm nipenda Sana .majizo yangu hardworking person..
@agricolamirinde6111
@agricolamirinde6111 2 жыл бұрын
it's a very good interview am truly inspired but salama please mda hautoshi aise like alikuwa na vingi ila inabidi akarishe
@evajames2514
@evajames2514 2 жыл бұрын
Nilikuwa nakuckiaga tu ckujua ww ni mtu mzuri na unahuruma na kujali.kaka mzuri sn and Smart
@hahmadhabibu2076
@hahmadhabibu2076 2 жыл бұрын
This man is genius...
@CHITUS
@CHITUS 2 жыл бұрын
This guy is so smart 🔥
@fatmaahamadabass8080
@fatmaahamadabass8080 Жыл бұрын
Hayo ndio mapenzi tena mapenzi ya Samani sana Mashallah
@AfiSoul103
@AfiSoul103 2 жыл бұрын
Nimeipenda sana ya Kiheshima
@mutumbisalash923
@mutumbisalash923 2 жыл бұрын
Mzazi wa E F.M kwa maongezi ya ki smart, kizazi kipya kwa jina yake CIZA? mwana wetu wa Tanganyika. Kutoka hapa ubeljiji, nikitoa pongezi ya dhati kwako mtangazaji bingwa SALAMA JABBIR. Ndoto yangu ni ya kukutana na wewe na Kunihoji hapo; mkasi au kwangu inshaALLAH
@xw6427
@xw6427 2 жыл бұрын
One of the best interviews
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 2 жыл бұрын
Mashallah, mimi namkubali sana Majizo,barikiwa sana brother 🙏
@rosemofuga8101
@rosemofuga8101 2 жыл бұрын
Waoooooo, Hongera sana Baba G
@lilianjulius917
@lilianjulius917 2 жыл бұрын
Intelligent one,tunamuomba na Idris Sultan
@veeJesus
@veeJesus 2 жыл бұрын
Tayar alishakuja hapa
@lilianjulius917
@lilianjulius917 2 жыл бұрын
Ooooh ngoja nisearch
@elizabethmwakalinga5271
@elizabethmwakalinga5271 2 жыл бұрын
Endelea kubarikiwa Majizzo,umenijenga sana
@melkizedeckelsonmbise4424
@melkizedeckelsonmbise4424 8 ай бұрын
Safi,,natamani hii meza angekaa Ruge nae ateme madini.
@fredrickpeter8051
@fredrickpeter8051 2 жыл бұрын
Salama,umeuliza maswali mengi,mbona hujauliza why E FM,kwann aliita e fm???that's my qn
@sheshem5453
@sheshem5453 2 жыл бұрын
Asante Salama! Bro Majei.. Mungu azidi kukubariki...
@maggiepeter8936
@maggiepeter8936 2 жыл бұрын
Salute #Majizzo........Lulu she got a really hubby
@carlosmzena548
@carlosmzena548 2 жыл бұрын
That's the face of business my dear he's not who you think he is
@harysonnyobuya9601
@harysonnyobuya9601 2 жыл бұрын
Ece Jay. Unajua kuuframe swali right to point. Hongera Sana 🙌
@othumanlorenzo260
@othumanlorenzo260 2 жыл бұрын
Angekuwa mwanasheria ingekuwa hatari katika x examinations
@lawizeentertainment5021
@lawizeentertainment5021 2 жыл бұрын
Hakuna kukata tamaa big up bro Majizzo
@estermwakafwila9890
@estermwakafwila9890 2 жыл бұрын
Hustler😊❤️
@susancharles1660
@susancharles1660 2 жыл бұрын
Huyu kaka ni smart sana👏🏽👏🏽👏🏽
@Agatee01
@Agatee01 2 жыл бұрын
Yes, I will be there In Jesus name
@sumahililuis85
@sumahililuis85 2 жыл бұрын
Naomba link ya interview ya salama na ommy dimpoz pl
@happinessjohn607
@happinessjohn607 Жыл бұрын
Yupo vizuri
@aminanamoyo83
@aminanamoyo83 2 жыл бұрын
Thanks ❤
@alinagwemwaselela9053
@alinagwemwaselela9053 2 жыл бұрын
Was waiting for this aisee...Najifunza SAAANA.
@vanjizzle122
@vanjizzle122 2 жыл бұрын
Am the first and Broo Your my Menter 🍸🇹🇿One Day I will be there I be to be 🍸🇹🇿
@ApipaTV
@ApipaTV 2 жыл бұрын
Asante Salama Nakupenda unafanya kazi nzuri
@zainabubakari4156
@zainabubakari4156 2 жыл бұрын
Nakukubali Sana Kk Ma..J
@mbechajumaa7966
@mbechajumaa7966 2 жыл бұрын
Namkubali San kaka majizo yani ntaishi na vitendo vyak
@charlesbakari7265
@charlesbakari7265 2 жыл бұрын
Majjizo umeniinspire Sana
@mtaalamwamambo2099
@mtaalamwamambo2099 2 жыл бұрын
Akili nyingi hiii🔥🔥
@mrfashion1687
@mrfashion1687 2 жыл бұрын
Nasubiri SALAMA NA ADAMU MCHOMVU
@saidalssa3409
@saidalssa3409 2 жыл бұрын
Great work salama keep it up
@irenengatia4289
@irenengatia4289 2 жыл бұрын
The show is 🔥🔥🔥
@homan_nkwama
@homan_nkwama 2 жыл бұрын
Salama ...! Mwenzio FARASI!?
@sarajoseph4253
@sarajoseph4253 2 жыл бұрын
Good interview
@dedsecmalis2005
@dedsecmalis2005 2 жыл бұрын
Endelea kubarikiwa bro 💪🏿
@Kanyaga_leatherIndustry
@Kanyaga_leatherIndustry Жыл бұрын
Kama uamini kwenye nguvu ya utafutaji lazima ufikirie mafanikio ya mtu yanatokana na kuuza madawa au mchawi.
@deboraezekiel784
@deboraezekiel784 2 жыл бұрын
Daaaa nimejifunza
@kolokokoloko9276
@kolokokoloko9276 2 жыл бұрын
Muulize uyo majizzo "" kwa Nini baadhi ya wasanii nyimbo zao hazipigwi Efm ?
@nsajigwamwanjati5119
@nsajigwamwanjati5119 2 жыл бұрын
Salama tuletee Gwajima
@leaherasto929
@leaherasto929 2 жыл бұрын
Apo kwa Elizabeth pamenigusa Sana Mungu awaweke
@niriacatering172
@niriacatering172 2 жыл бұрын
Asanteni Sana
@selemanimuhanga4018
@selemanimuhanga4018 2 жыл бұрын
Hii show Kali Sana! Big Up Yahstone
@hadijajumanne5493
@hadijajumanne5493 2 жыл бұрын
Na hasa watanzania waķiona mtu anamaendeleo wanakuwa na chuki yani majay yuko na point
@azikamujulius3530
@azikamujulius3530 2 жыл бұрын
Daah Jamaa kapambana sana asee
@hadijajumanne5493
@hadijajumanne5493 2 жыл бұрын
Kama wanakuja kukamata gaidi wabongo duuh
@mamukinyogoli5549
@mamukinyogoli5549 2 жыл бұрын
Majizo unafanana na waziri simbachawene
@mussamsella8560
@mussamsella8560 2 жыл бұрын
Maisha ni kupambana bila kukata tamaa huku ukiwa na subira
@shukurubashiry9117
@shukurubashiry9117 2 жыл бұрын
Nimejufunza kitu kutoka kwa majizo kwenye maisha no kukata tamaa halafu usiogope kufanya kitu ambacho unacho
@richardcastromzena5136
@richardcastromzena5136 2 жыл бұрын
0:51 1:40 5:14 5:39 6:34 7:04 7:38 23:57
@winifridambilinyi8043
@winifridambilinyi8043 2 жыл бұрын
Nice interview🥰
Citizen TV Live
Citizen TV Kenya
Рет қаралды 45 М.
НАШЛА ДЕНЬГИ🙀@VERONIKAborsch
00:38
МишАня
Рет қаралды 2,6 МЛН
Когда отец одевает ребёнка @JaySharon
00:16
История одного вокалиста
Рет қаралды 14 МЛН
小蚂蚁会选到什么呢!#火影忍者 #佐助 #家庭
00:47
火影忍者一家
Рет қаралды 117 МЛН
DID A VAMPIRE BECOME A DOG FOR A HUMAN? 😳😳😳
00:56
Thilakan In Nerechowe - Old Episode  | Manorama News
25:13
Manorama News
Рет қаралды 2,9 МЛН
Salama Na MwanaFA Ep 10 | KARAMA Part 2
27:20
YahStoneTown
Рет қаралды 110 М.
НАШЛА ДЕНЬГИ🙀@VERONIKAborsch
00:38
МишАня
Рет қаралды 2,6 МЛН