Рет қаралды 4,855
Bodi ya wakurugenzi wa DMDP(Dar es salaam Metropolitan Development project ) ikiwa katika ziara ya siku 2 yaani tarehe 7 na 8 oktoba 20202 kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jiji la Dar es salaam), ambayo inasimamiwa moja kwa moja na ofisi ya Rais TAMISEMI,kupitia TARURA (Tanzania Rulal and Urban Road Agency), ambayo imepangwa kutekelezwa kwa awamu mbili yaani 2015/20 na 2020/25 katika Manispaa tatu yaani Temeke,Ilala na Kinondoni.
Miradi hiyo imeghalimu kiasi cha pesa zaidi ya billion 600 kwa manispaa zote, ikiwa miradi hiyo inatekelezwa kwa fedha za mkopo wa serikali kutoka benki ya dunia.
Bodi hiyo ilifanya ziara yake ya kwanza katika manispaa ya Temeke, tarehe 7 octoba 2020 kwa kukagua miradi mbalimbali ya miundo mbinu ya kijamii ikiwemo barabara, masoko, mifereji na vituo vya Afya.
Halmashauri ya manispaa ya Temeke wamenufaika na miradi hiyo kwa kupata masoko 3 yaliyokamilika na kuanza kutumika kati ya masoko 6 yaliyo katika mradi huo, ikiwemo soko kubwa la kisasa lilopo Kijichi pamoja na stendi ya mabasi kijichi, vilevile ujenzi wa barabara zinazowaunganisha wakazi wa eneo hilo ikwa ni pamoja na barabara ya Kijichi kwenda Toangoma yenye urefu wa kilomita 3.2 na barabara ya mwanamtoti yenye km 1.8.
Miradi mingine ni ujenzi wa mifereji ya maji ambayo itasaidia kuzuia mafuriko kwa wakazi walio maeneo ya mto kizinga ikiwemo ujenzi wa mfereji wa Kwashego ambao mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 70%.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa bodi ya ushauri TARURA, Injinia Frolian Kabaka amesema haya juu ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha bodi ilifika kukagua mradi wa kituo cha Afya cha buza, ambacho kimeshakamilika na kimeanza kutumika.
Miradi mingine inayohusisha manispaa ya Temeke ni pamoja na mradi wa ujenzi wa bonde la gerezani, maboresho ya miundombinu ya jamii kata ya kilakala na Keko, maboresho ya miundo mbinu ya jamii ya mtoni,ujenzi wa barabara za chang’ombe, mchicha , temeke na mbagala, maboresho ya miundo mbinu buza ambayo itaunganisha ukanda wa mbagala na ilala, lakini pia ununuzi wa magari 20 ya kubebea taka na makontena 65 ya kuhifadhia Taka.
Bodi imepanga kumalizia ziara zake kesho tarehe 8 ya mwezi oktoba kwa kukagua miradi ya manispaa ya Kinondoni na Ilala.