Рет қаралды 32,880
Rais John Magufuli siku ya Jumanne alikutana na kufanya mkutano na wadau mbalimbali wa madini mkutano ambao uliwashirikisha wakuu wa mikoa, mawaziri na wafanyabiashara wa kada mbalimbali za sekta hiyo.
Baada ya kusikiliza yote yaliyozungumzwa, Rais Magufuli akatoa hotuba yake akisisitiza kutazamwa vyema kwa msururu wa malipo kwenye sekta hiyo pia akataka kuimarishwa kwa ulinzi kwenye maeneo ya uchimbaji na kumtaka waziri wa madini, Dotto Biteko kuhakikisha kamera za CCTV zinafungwa ndani ya mwezi mmoja.