INNALILAHI WAINNA ILAYHI RAJIUNI ACT WAFIKWA NA MSIBA MZITO OMO ASHIRIKI MSIBANI

  Рет қаралды 4,000

Tifu Tv

Tifu Tv

Күн бұрын

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, Leo Jumanne Agosti 13, 2024 amejumuika pamoja na Viongozi, Masheikh, Wananchi na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Maziko ya Marehemu, Bw. Sadra Hassan Juma, huko Wete- Mtemani, na Kangagani, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Marehemu Bw. Sadra, ambaye ni Mstaafu wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC), na pia Baba wa Mmoja wa Wasaidizi wa Mheshimiwa Othman, alifariki-dunia mapema Jana Agosti 12, huko katika Hospitali ya Mzena, Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Marehemu amesaliwa katika Msikiti wa Ijumaa wa Mwitani Wete, katika Sala ambayo imeongozwa na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa la Zanzibar, Sheikh Jamal Mohamed Abeid; kabla ya kupelekwa Kijijini kwao Kangagani, pia Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwaajili ya Hatua za Mwisho za Maziko.
Viongozi mbali mbali wa Serikali, Siasa, Dini na Jamii wamehudhuria Maziko hayo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Wete, Mhe. Dokta Hamad Omar Bakar na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa wa Kichama Wete, Ndugu Juma Khamis Ali (kabakaba).
Awali kabla ya Maziko hayo, Mheshimiwa Othman amefika na kutoa, Mkono wa Pole kwa Ndugu na Jamaa huko Nyumbani kwa Marehemu, Kifumbikai Wilaya ya Wete, ambapo pia amewatakia Wanafamilia nyoyo za subra, hasa katika Kipindi hiki cha Msiba, huku akiwanasihi waendelee kuishi kwa umoja na mashirikiano, kama wakati ule ambao Mzee wao alipokuwa-hai.
Katika Tah-zia hiyo, Mheshimiwa Othman ameambatana na Mke wake, Mama Zainab Kombo Shaib.
Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi, Amiin!
Innalillahi Waina Ilayhi Raajiun!

Пікірлер: 9
@HamisMberwa
@HamisMberwa 2 ай бұрын
Innalilahi waina ilaihi rajiuu Allahumma Ghfirlahum warahamahu waskana Filjanna Tangulia Mzee Sadra
@SuleimanMuhamed-it8bj
@SuleimanMuhamed-it8bj 2 ай бұрын
Innalillah wainna ilayhi rajouna
@Allybinamour
@Allybinamour 2 ай бұрын
إنا لله وإنا إليه راجعون
@FatmaAmour-y1t
@FatmaAmour-y1t 2 ай бұрын
Innalillah wainnailayhi raajiun ALLAH amsemehe makosa yake aamiyn
@fatmaabdalla2707
@fatmaabdalla2707 2 ай бұрын
Innalillahi wainna ilayhi raajiun, Tunamuomba Allah amsamehe makosa yake na amfanyie wepesi ktk safari yake
@ArRahman-ih1pi
@ArRahman-ih1pi 2 ай бұрын
😢 hakika sote ni wa Allah na kwake tutarejea😢Allah amsamehe makosa yake 🙏
@ShauriAli-o5y
@ShauriAli-o5y 2 ай бұрын
Kilala kheri katika MAISHA Yako ya barzakh
@chikujuma18
@chikujuma18 2 ай бұрын
Inalilaahi wainalilah rajighun mola ampe khauli thabiti ndugu yetu mbele yake nyuma yetu
@omarhamadomar8832
@omarhamadomar8832 2 ай бұрын
Allah amlaze mahala pema peponi
DCMA Taarab & Kidumbaki Ensemble
29:34
Dhow Countries Music Academy
Рет қаралды 86 М.
哈哈大家为了进去也是想尽办法!#火影忍者 #佐助 #家庭
00:33
火影忍者一家
Рет қаралды 131 МЛН
Кәсіпқой бокс | Жәнібек Әлімханұлы - Андрей Михайлович
48:57
Это было очень близко...
00:10
Аришнев
Рет қаралды 6 МЛН
ITAKUTOA MACHOZI: MFANYA KAZI WA NDANI AMNYONGA MTOTO WA MIEZI 6/UCHAWI
25:46
DCMA Kidumbak Group
6:31
Dhow Countries Music Academy
Рет қаралды 18 М.
RAIS MWINYI AMLIZA MZEE WA MIAKA 62 ZANZIBAR
3:34
Tifu Tv
Рет қаралды 1,8 М.
KIMENUKA ZANZIBAR SINGA AMWAMBIA RAIS MWINYI MANENO HAYA
7:14
SHEIKH WALID AKIMKARIBISHA SHEIKH OTHMAN MAALIM KWA AINA YA KIPEKEE
40:58
哈哈大家为了进去也是想尽办法!#火影忍者 #佐助 #家庭
00:33
火影忍者一家
Рет қаралды 131 МЛН