Рет қаралды 6,721
Uchaguzi mkuu wa 1975 ulivyomuweka Aboud Jumbe madarakani Usiku wa Ijumaa ya Oktoba 24, 1975, ikiwa ni siku mbili kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 26, Rais wa Tanu, Mwalimu Julius Nyerere alilihutubia Taifa kwa njia ya redio na kuahidi kuwa ataendelea kuitumikia Tanzania na watu wake kwa kipindi kingine cha miaka mitano kama wananchi wengi wangempigia kura katika Uchaguzi Mkuu huo.
Na kwa upande wa Zanzibar, Aboud Jumbe ambaye aliingia madarakani Aprili 1972 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Abeid Amani Karume kilichotokea Ijumaa Aprili 7, 1972, uchaguzi huu wa Oktoba 1975 ulikuwa wa kwanza kwake na ndiyo ulimuweka madarakani.