Nimefurahi sana kutufungua ufahamu, ninapata tabu sana kupata soko la kuku wa kienyeji, nakuwa na kuku lakini soko ndiyo tatizo, je unautalamu wa soko?asante Dada Mungu akubariki. Naitwa Mary Z. Gyumi
@NoaUbongoTz6 жыл бұрын
Habari, Mary. Je, kabla hujaanzisha biashara yako ya kuku wa kienyeji, ulifanya utafiti wa soko hapo unapoishi? Je, ulifahamu kuwa kuna watu wanahitaji bidhaa yako ya kuku wa kienyeji? Haya ni maswali mawili ambayo ulitakiwa kujiuliza kabla hujaanza biashara yako. Ndio, unaweza kuwa na bidhaa lakini je, ni wangapi wanaihitaji? Tunakushauri urudi tena sokoni na ufanye utafiti wako kwa ufanisi zaidi ili ufahamu ni wangapi na nani wanahitaji bidhaa yako. Rudi na utazame video zetu ya namba 3 na 4 ili kufahamu jinsi ya kufanya utafiti huu.