BINTI ZANGU WAMELALA 'MUENDELEE KUTUOMBEA MKE WANGU YUPO HOSPITALI' BABA WA WALIOFARIKI KWA MOTO

  Рет қаралды 14,074

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

Baba wa familia iliyotokea mauaji ya watu watatu katika Mtaa wa Segu Bwawani kata ya Nala, wilayani Dodoma Mjini, Robert Mugema ameomba Serikali kuimarisha ulinzi kwenye eneo hilo kwa kuwa wakati wa tukio kuna baadhi ya majirani nyumba zao zilifungwa milango kwa makufuli.
Septemba 16,2024 katika nyumba yake waliuawa watu watatu ambao ni Milcah Robert (12), aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika Shule ya Msingi ya Chilohoni pamoja na Mkazi wa Mailimbili jijini Dodoma Fatuma Mohamed (20) na kisha miili yao kuchomwa moto.
Katika tukio hilo pia binti aliyekuwa akifanya kazi katika nyumba hiyo, Makiwa Abdallah (16) aliuawa huku mama wa familia hiyo, Lusajo Mwasonge (40) akijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza leo jioni Septemba 18,2024 nyumbani kwake Segu Bwawani mara baada ya ibada ya kuaga mwili wa binti yake Milcah, Mugemu amesema yeye atakwenda mkoani Geita kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani lakini familia yake itabaki kwenye nyumba hiyo.

Пікірлер: 51
@MonicaMfinanga
@MonicaMfinanga 19 сағат бұрын
Umeongea vizuri sana Baba MUNGU azidi kukutia nguvu umejitahidi sana hujaropoka japo unauchungu mkubwa sana jamani pole na MUNGU akutie nguvu.
@CellineChengula
@CellineChengula 19 сағат бұрын
Mungu akutie nguvu Aiseee Endelea kumwamini Mungu hajawahi kumwacha MTU
@user-jn6ec7qv5p
@user-jn6ec7qv5p 3 сағат бұрын
Polee kaka angy kipenz Mungu azid kukutia nguvu katika kipindi hiki kigumu unachopitia
@claudiangowi9628
@claudiangowi9628 18 сағат бұрын
Pole Sana, najua maumivu uliyonayo ni makali Sana Mungu akutie nguvu 🙏😢😢😢😢 mwenyezi Mungu awapumzishe Kwa Amani wote waliopoteza maisha
@CristinLyanga
@CristinLyanga 8 сағат бұрын
Pole sana my broo.
@gladnessfinda7534
@gladnessfinda7534 6 сағат бұрын
Mungu aendelee kukupa ujasiri na uvumilivu ndugu. Mungu aendelee kukufunika katika ukuu wake. Mungu aendelee kumponya mama yetu Amen.
@ritapiusnicolaus7068
@ritapiusnicolaus7068 19 сағат бұрын
Pole sana BABA 💔😭😭😭😭
@stephaniemmuya8382
@stephaniemmuya8382 18 сағат бұрын
Mungu akuongoze na akutie nguvu ktk mapito unayoyapitia
@AlHamra-k4u
@AlHamra-k4u 13 сағат бұрын
Pole Sana baba angu Mwenyezi Mungu akupe nguvu akupe subra na uvumilivu
@user-fr7to6iy2h
@user-fr7to6iy2h Сағат бұрын
Mungu akawe faraja kwako pole sana jambo hili nigumu mno tunamuombea mama Mungu amponye
@FatmasaidhamesaHamesa
@FatmasaidhamesaHamesa 19 сағат бұрын
Mungu atalipa haiwezi potea damu y mto
@salimamasanja4659
@salimamasanja4659 5 сағат бұрын
Pole sana tena sana,mungu akupe ujasiri
@asanterabisimon1347
@asanterabisimon1347 5 сағат бұрын
Pole sana mwanasingida mwenzangu mungu skutie nguvu
@MwanaHamis-y4e
@MwanaHamis-y4e 8 сағат бұрын
Pole sana maumivu ulinayo ni makali mno Mungu akutie nguvu ktk kipindi hiki kigumu niuchungu mno ulinao
@ChristinaOnditi-el3xo
@ChristinaOnditi-el3xo 6 сағат бұрын
Ndugu zangu,unapoona kuna mazingirz yeyote ambayo sio salama,pangisha nyumba kaishi mbali kabisa hata wilaya au mkoa mwingine. Hama. Usalama wako ni amani yetu sisi wote wenye nia njema na binadamu wenzetu,unaweza ukajikuta tu upo ndani ya chuki from no where.hama alafu muombe mungu huko uliko mwisho kila kitu kitakua sawa. Kuna baadhi wa binadamu wenzetu ukifungua moyo wake na wanyoka, unaweza ukakubali kuishi pori lenye nyoka ukajua kujilinda kuliko kuishi na huyo binadamu, maana nikiangalia naona hapo kuna chuki iliingia, hadi milango ya baadhi ya majirani kufungiwa kufuli?.so 😭
@twiseghekisilu8845
@twiseghekisilu8845 11 сағат бұрын
Pole Sana kaka Mungu awe faraja kwenu!
@MariamKhalid-ub9jj
@MariamKhalid-ub9jj 3 сағат бұрын
Mungu akutie nguvu...katika huu wakati mgumu😢
@gloryleonard1563
@gloryleonard1563 10 сағат бұрын
Ee Mungu mtie nguvu huyu baba watoto wamekatishwa ndoto zao, Mungu wewe pekee ndiyo unajua mponye huyo mama maana wewe ndiyo mponyaji wetu.
@NeemaDamas-c3q
@NeemaDamas-c3q 17 сағат бұрын
Pole Baba mungu akutie nguvu .
@zamalisaide3209
@zamalisaide3209 4 сағат бұрын
Pole kaka angu mwenyezi mungu akupe subbra
@HalimaKassim-yz3we
@HalimaKassim-yz3we 9 сағат бұрын
Jamani dunia inaenda wapiii Tanzania inaelekea wapi😢😢😢😢😢😢😢masikini poleni sana
@Rosina-q2j
@Rosina-q2j 18 сағат бұрын
Pole sana kaka Mungu akutie nguvu
@user-bm2tr7sn9e
@user-bm2tr7sn9e 7 сағат бұрын
Mungu akutie nguvu baba
@Christinachidyaka
@Christinachidyaka Сағат бұрын
Pole sana najua unamaumivu makubwa sana lakini amini mungu yunawe
@Christinachidyaka
@Christinachidyaka Сағат бұрын
Mungu atawlinda na mungu atamponya mke wako
@VeronicaMukandara
@VeronicaMukandara 4 сағат бұрын
Pole sana mwl .
@HappinessBarua
@HappinessBarua 4 сағат бұрын
Bwana Yesu wewe wajua.😢😢😢
@alleyjuniourtz
@alleyjuniourtz Сағат бұрын
Pole sana Ndugu 😢
@ZuhuraZiota
@ZuhuraZiota 7 сағат бұрын
Pole sana baba
@OmanOman-dd5qk
@OmanOman-dd5qk 14 сағат бұрын
Pole sana kaka ipo siku mungu atalipa tu
@mpefu_4936
@mpefu_4936 8 сағат бұрын
Poleni sana sana mungu yupo kweli
@meckmussa1840
@meckmussa1840 19 сағат бұрын
Mungu yupo
@rashdiyange7758
@rashdiyange7758 8 сағат бұрын
Uyu jamaaa mwazo nilikua najua alistote 😂 pole ndugu yangu
@HyacintaGugu
@HyacintaGugu 6 сағат бұрын
Wanafanana sana
@MultiBice
@MultiBice 2 сағат бұрын
Pole saana baba
@farajasallah2338
@farajasallah2338 8 сағат бұрын
Dunia ngumu hii, pole sana
@FatumaMohamedi-t6t
@FatumaMohamedi-t6t 3 сағат бұрын
Jaman Mungu ww unajua na utatenda .
@ThomasMmary-r7w
@ThomasMmary-r7w 2 минут бұрын
Poreni wafiwa
@teller_julio
@teller_julio 5 сағат бұрын
Kwa kweli huyu baba ni jasiri sanaa
@LaurentMatigili
@LaurentMatigili 7 сағат бұрын
Mungu wa mbinguni akupe nguvu na ujasiri kama Simba..,😢😢
@HopeChriss
@HopeChriss 13 сағат бұрын
Mwenyez MUNGU NI MWINGI WA REHEMA AMPONYE UYO MAMA AWATAJE AO MASHETANI WALIO FANYA IVYO
@jumahili8121
@jumahili8121 10 сағат бұрын
Za saa hizi. Hii habari sijaelewa chanzo chake. Naomba ufafanuzi
@salama1113
@salama1113 9 сағат бұрын
Pole kaka kwamsiba mzito jamani😢😢😢
@lizzynkifu4179
@lizzynkifu4179 2 сағат бұрын
Yan sijui tunaelekea wapi kila ukifungua mitandaoni ni habar za kutisha tu TUOMBE MUNGU atusaidie jaman
@BesterSigalla
@BesterSigalla 11 сағат бұрын
Duuu dunia hii pole bb
@gracebwimbo1889
@gracebwimbo1889 18 сағат бұрын
WANADAMU WAKATILI WAMEKUWA WAKITOA UHAI WA WENZAO BILA HOFU YA MUNGU
@TunauzaSimu-fn2ff
@TunauzaSimu-fn2ff 8 сағат бұрын
Mama Samia nchi imekuwa ya mauwaji hata wtt wadogo wasio na dhambi kwa MW MUNGU WETU. YA RABBI
@joycemkeka3769
@joycemkeka3769 6 сағат бұрын
Hakika inatisha na inavunja moyo yani nimachozi yauchungu kila siku Mungu tusaidie
@delsonandrea5223
@delsonandrea5223 4 сағат бұрын
Kwa mtu mwenye akili timama hawezi kufanya tukio llt la kutisha vijana wavuta bangi unakua wanahusika kwenye matukio makubwa,, nawachukia wavuta bangi ,, unakuta mtaan wapo wanajulikana alafu mnawalea tu matokeo yake ndo hayo sasa.
@fatumaathumani9977
@fatumaathumani9977 Сағат бұрын
Dodoma matukio yamexidi jamani alafu kupp kimya kama hamna kilich tokea
@nishaabdula5015
@nishaabdula5015 10 сағат бұрын
Ngumu sn i kuipokea
Angry Sigma Dog 🤣🤣 Aayush #momson #memes #funny #comedy
00:16
ASquare Crew
Рет қаралды 50 МЛН
Girl, dig gently, or it will leak out soon.#funny #cute #comedy
00:17
Funny daughter's daily life
Рет қаралды 28 МЛН
Teaching a Toddler Household Habits: Diaper Disposal & Potty Training #shorts
00:16
Dad gives best memory keeper
01:00
Justin Flom
Рет қаралды 25 МЛН
BREAKING: MEYA JACOB AFIKISHWA MAHAKAMANI
1:21
Millard Ayo
Рет қаралды 3,9 М.
Angry Sigma Dog 🤣🤣 Aayush #momson #memes #funny #comedy
00:16
ASquare Crew
Рет қаралды 50 МЛН