Meena Ally Afunguka Yote, Kujiunga Clouds, Familia Na Maisha Yake | SALAMA NA MEENA PART 1

  Рет қаралды 85,273

YahStoneTown

YahStoneTown

2 жыл бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
MARASHI YA KARAFUU…
Jina lake halisi ni Muhaymeena Ally na kwa kifupi aliona Meena litamfaa sana na si Amina kama watu wengi wanavyodhani. Mzaliwa halisi wa Zanzibar na ni mtoto wa Stone Town kabisa. Kutoka alikozaliwa Meena na nilipozaliwa mimi si mbali kabisa, kwao Malindi karibu kabisa na bandarini na mimi kwetu ni Kiponda, wakati Meena anazaliwa mwaka 1993 mimi nilikua darasa la sita, msichana kabisa na pengine nilishaanza kuandikiana barua na kichimvi na kina Murad 🤣.
Mimi na yeye tumefahamiana hapa Dar es Salaam lakini, sina hakika kama wazazi wetu wanajua maana bado sijamuuliza Mama yangu ila nna hakika wa asilimia 99 kwamba Kaka zangu (ambao wengi wao ni wavuvi) wanawajua wazazi wake na pengine shangazi na wajomba zake, mtaa ambao Meena kazaliwa ndo njia wanayopita kwenda Pwani so uhakika huo nnao kwa asilimia hizo. Lately mimi na yeye tumekua karibu, uzanzibari pengine unachangia kwa kiasi kidogo ila binafsi zaidi ni kwasababu na admiration ya kazi zetu kwa kila mmoja wetu. Wakati Meena anakuja EATV mimi sikumbuki vizuri na nadhani zilikua ndo siku zangu za mwisho mwisho kuwa muajiriwa pale au pengine nlikua tayari nlikua nafanya mambo yangu pembeni kwa kupitia Mkasi TV.
Nilifurahia kila sekunde ya maongezi yetu haya kwasababu nilikua naongea na Rafiki yangu na ki ukweli ilikua inatakiwa yafanyike siku nyingi tu ila kama unavyojua, sisi binadamu tunapanga mambo yetu ila Mwenyezi Mungu ndo hutupa nguvu na wasaa wa kutufanya tuyatekeleze kwahiyo wakati huu ndo ulikua wakati sahihi.
Kama mwezi umepita Meena alipata mitihani kwenye mitandao ya kijamii baada iliyokua inalazimishwa iwe video yake akiwa anafanya ngono kutambaa mitandaoni. Kama Dada ilinishtua mara ya kwanza na uzuri ni yeye mwenyewe ndo alinitumia, ukimuangalia yule Dada kwa pembeni unaweza kudhani ni yeye ingawa kama unamfahamu Meena kwa ukaribu basi utajua kabisa yule si yeye. Mtihani ulikua mkubwa, mtihani wa kuwaelezea binadamu ambao baadhi yao walikua wanataka yule awe yeye nao walikuwepo lakini walikua hawataki kuamini nao pia tulikua wengi tu. Mawe mengi yalirushwa na ilihitaji Meena awe kwenye ubora wake, kuto panic na kufanya yote yaliyokua yanatakiwa kufuatwa ki SHERIA na mengine tuiachie Mamlaka inayohusika ambao naamini bado wanaendelea na kumtafuta aliyeanzisha uvumi ule na yangu imani watampata ili awe mfano kwa wengine.
Sina hakika sana na nasema hivi kwasababu kwa mtu mwenye imani na akili timamu hawezi kufanya unyama kama huu kwa mtu mwengine ambae hana ubaya nae. Madhara yanayokuja na shutuma kama hizi ni makubwa sana, ki akili na ki utu na ki biashara. Athari zake zinaweza kuwa za muda mrefu kuliko wengi wanavyo dhania.
Humu nilimuelewa vizuri, utulivu wake kwenye kujibu maswali na jinsi alivyokua amejibeba, mmoja anaweza kuangalia kwa kujifunza kutoka kwake, Meena ana kila kitu ambacho kinaweza kikamfanya yeye aweze kutimiza ndoto zake, kuwa chochote kile ambacho atapewa au atapata nafasi ya kukifanya, kuanzia kwenye filamu mpaka yote yale ambayo anatamani kuyafanya na anaweza kuyafanya kwa asilimia 100, ambayo sina shaka atayapa na pengine zaidi.
Humu tunamzungumzia Marehemu Bibi yake ambaye kifo chake kilimuathiri kwa kiasi kikubwa na jinsi ambavyo alijikwamua kutoka kwenye wimbi hilo la msongo. Maelewano yake na wazazi wake ni kitu cha kumfanya mtu ajifunze kutoka kwake, najua si kila mmoja wetu ana mahusiano ya aina hii na wazazi wake ila kwa kuskiliza naamini utapata ujumbe flani. Heshima na kujituma kwake anapokua anafanya kazi pia itaiskia humu, kujitoa kwake na jinsi anavyoangalia na kujifunza mengi kwa kuwasoma watu na nafasi zao kunamfanya aweze kufika mbali, na yangu matumaini nnayoyaona mimi kwake basi na yeye anayaona hivyo na zaidi. Kazi yetu sisi ni ku enjoy tu kwa kuangalia safari yake ya kikazi na kushuhudia mafanikio yake tele yajayo In Shaa Allah.
Enjoy hii session kama ambavyo umekua uki enjoy na kujifunza mengi kutoka kwa wengi waliopita na wengi wajao. Mungu katubariki na watu wengi wa aina hii ambao wako mbele yetu, maisha yao ni darasa tosha kwetu sote. Ni vyema yale tutakayo yapenda tukayaweka na sisi katika maisha yetu ili tufike mbali zaidi.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪KZbin Link bit.ly/KZbinSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 98
@bongotvonline4883
@bongotvonline4883 2 жыл бұрын
Unajua SALAMA wewe ni shida sana, sina la kusema kuhus wewe. Ila kwa wanaoelewa wanajua kazi ilivyo kumhoji MTANGAZAJI MWENZIO. All the best Salama.
@saidmohamed4619
@saidmohamed4619 2 жыл бұрын
Aisee leo nimeenjoy sana...two kids from Zanzibar in one place...hapo ni matani ya kikwetu tu...
@drwebangila
@drwebangila 2 жыл бұрын
Navutiwa sana Meena. Looks smart and intelligent. Kila la kheri Salama na Meena. Naamini Mkiungana Nchi itasimama.
@Kevin_davi
@Kevin_davi 2 жыл бұрын
Salama naomba hichi kipindi cha salama na kirudi kwenye channel ya East Africa television kama ilivyokuwa hapo awali sisi wanyonge hatuna pesa ya kununua dstv bei yao ikoo juu sana
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 2 жыл бұрын
Salama ''tuna omba Mlete bikilala! na mzee kikalala 😘na muwandishiw wao' wa kombolela 🔥🔥
@Wachuoni
@Wachuoni 2 жыл бұрын
I think this kind of Interview suits you better, naifananisha hii na Zuhura Yunus, imejaa upendo, utani, uhuru, ucheshi, hisia za ukweli kabisa kutoka moyoni. na kwa hii pekee nimependa sana vionjo vya lugha za Mina ... kama "Dada Judi acheke", .... it was great 👍.... keep it up !
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 жыл бұрын
I love the way Meena answers the questions... 👌💚
@antonymwaniki6248
@antonymwaniki6248 Жыл бұрын
I really like Meena's voice.
@badalichauchau6983
@badalichauchau6983 2 жыл бұрын
Nampenda sana huyu dada kwasababu hajawahi kuzungumza maneno ya ovyo
@iammichaellukindo
@iammichaellukindo 2 жыл бұрын
Nimefanya kazi na meena EATV na Clouds lakini baada ya kumsikiliza hapa nahisi kama sasa ndio nimemjua angalao. And hongera Meena. I know what happened to you EATV. Mungu amekupa nafasi keep Going
@odrianinicolaus5353
@odrianinicolaus5353 2 жыл бұрын
Tuletee, Yule Mbunge Kishimba wa Bungeni au Mhe.Msukuma Salama
@stevennyondo2215
@stevennyondo2215 Жыл бұрын
Kwenye lafudhi nakubali huyu dada. First time namuona nlijua chuga girl.
@rodrickmataba8999
@rodrickmataba8999 2 жыл бұрын
Habari, Hujambo...😀😀😀 leo hii salamu hatujaipata
@mongai001
@mongai001 2 жыл бұрын
To be honest this young lady she always make me laugh peace and love
@bish_daddiyao
@bish_daddiyao 2 жыл бұрын
Nice interview.. Bring Zuchu I have been Searching for Long🙌🏾🇰🇪💕
@mkaapwekekariakoo6417
@mkaapwekekariakoo6417 2 жыл бұрын
asante sana Salama.... natamani siku moja uingie mtaani utuletee mtu ambaye si maarufu lakini, ambaye ataweza kufanya usaili nawe. hata kama si kumfanya maarufu lakini itakuwa pia namna ya kuhamasisha watu kuwa kile wanaamini. Kazi nzuri sana, ni lini utajihoji hahahaaa
@mohamednaaman188
@mohamednaaman188 2 жыл бұрын
Masha Allah interview nzuri #Zanzibar 🔥
@saumusalimuhassan2499
@saumusalimuhassan2499 2 жыл бұрын
Nakukubali sana Meena
@user-gi1ez6fc1y
@user-gi1ez6fc1y 2 жыл бұрын
Can't wait salama na Millady
@bobanthony1326
@bobanthony1326 2 жыл бұрын
Quite funny; had a good laugh.
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 жыл бұрын
Ace jay keep up the good work...👌💚
@neemapetro8188
@neemapetro8188 2 жыл бұрын
I love mena jmn uwii❤️❤️❤️❤️
@zhaujiakashindi6617
@zhaujiakashindi6617 2 жыл бұрын
Nawapenda sana…❤️❤️
@yetromtambulo3452
@yetromtambulo3452 Жыл бұрын
Keep it up
@chiticollemans
@chiticollemans 2 жыл бұрын
Please bring Ghalib (GSM) and Flaviana Matata
@victormwakipesile6990
@victormwakipesile6990 2 жыл бұрын
Tunaomba ya Dina marious
@janethsuleiman2445
@janethsuleiman2445 2 жыл бұрын
Nimecheka sana
@lastsimbatv1497
@lastsimbatv1497 2 жыл бұрын
U kill it salama i love u mwaaaah beautiful
@alphonsinedusabe3590
@alphonsinedusabe3590 2 жыл бұрын
🤣🤣🤣 jmni meena wew 💥😍
@alphredinaalphonce7043
@alphredinaalphonce7043 2 жыл бұрын
💕🥰
@didahbebe3866
@didahbebe3866 Жыл бұрын
I really like the answers za meena and she's so smart ma sha allah
@davidnchoji
@davidnchoji 2 жыл бұрын
I love you Da Salama, am here just for you and that beautiful Lady Meena❤️🙌🏽
@princessbim6096
@princessbim6096 2 жыл бұрын
Salama naa zuchu ndo umeificha shoga yngu
@rosegideon336
@rosegideon336 Жыл бұрын
Mfike Mbali.
@mtanzaniahalisimungunimwem673
@mtanzaniahalisimungunimwem673 2 жыл бұрын
Nawapenda sana wote jamani
@dilipdab3714
@dilipdab3714 2 жыл бұрын
Kweli.leo.munachoweyaa
@el-chicosfootballdevelopme7411
@el-chicosfootballdevelopme7411 2 жыл бұрын
Iyo lafudh anayoigiza ni ya joti si ya kizanzibari. Wazanzibari hawaongei hvo.
@mariagodfrey2028
@mariagodfrey2028 2 жыл бұрын
😀😀😀😀😀
@chardoAmos4476
@chardoAmos4476 2 жыл бұрын
Mimi naomba ufanye interview na milard ayo please
@shahabdul1126
@shahabdul1126 2 жыл бұрын
when will you upload Salama na Zuchu? we need it here
@tofikijafary8470
@tofikijafary8470 Жыл бұрын
Mmm
@ayeeshasuleiman8826
@ayeeshasuleiman8826 2 жыл бұрын
Hahaaa nimefurah
@mohamedhamad2374
@mohamedhamad2374 7 ай бұрын
Sister salama mambo nimefatilia mahojiano unayofa nya naona unafanya na watu ambao ni maarufu vipi wasio kuwa maaarufu
@fahadfahmy
@fahadfahmy 2 жыл бұрын
Wazenji united.
@alantonio855
@alantonio855 2 жыл бұрын
Mwijaku next time
@ishakafaki3501
@ishakafaki3501 2 жыл бұрын
Rangi nyekundu Kwa asie onaa nikumwambia afinge macho then awashe tochi machoni mwake then utamwambia hiyoo ndio rangi nyekundu
@santruninichamy4974
@santruninichamy4974 2 жыл бұрын
Umetishaaa... We kichwa
@loysirikwa5052
@loysirikwa5052 2 жыл бұрын
Upload Salama na Adam Mchomvu
@dilipdab3714
@dilipdab3714 2 жыл бұрын
Ww.meena. salam.leo.munanichekesha.kweli
@meky9404
@meky9404 2 жыл бұрын
tunamwomba na msuvaaaa
@fortunathabarabara8471
@fortunathabarabara8471 2 жыл бұрын
salama na wema sepetu
@bjzee1981
@bjzee1981 2 жыл бұрын
Karo za chooni sio round but ni oval
@bjzee1981
@bjzee1981 2 жыл бұрын
Kumbe tuko wengi. Na ndio kilicho nifanya nijue lugha nyingi.
@shedyali964
@shedyali964 2 жыл бұрын
Samahan salama darajan hamuna round kuna nondo na harufu mbaya
@user-eo7ug2tg9r
@user-eo7ug2tg9r 2 жыл бұрын
My love meenaally😍😍😍😍
@sabraridhwan2858
@sabraridhwan2858 2 жыл бұрын
Salama badilisha nguo hizo kila Siku nyeusi kama upo msibani
@salumbabu
@salumbabu 2 жыл бұрын
Acha makasiriko,,, 😁😁😁😁
@abdullahhamed2197
@abdullahhamed2197 2 жыл бұрын
Tunaomba ya salah wa GSM
@kharounngavason8012
@kharounngavason8012 2 жыл бұрын
Kwa MEENA tena ufika hapo
@tamrikznz7583
@tamrikznz7583 2 жыл бұрын
Nyinyi Wapemba Mnaitwa Huku Kwenu.
@dilipdab3714
@dilipdab3714 2 жыл бұрын
Sie.hivyo.vilikuwa.ndio.yeyetu.vifundo.vya.miwaa.salama.na.meena.lakini.sahivi.kifundo.kinalipwaa
@lareineminah1353
@lareineminah1353 2 жыл бұрын
Salama na zuchu lini?
@hamedabashir9
@hamedabashir9 2 жыл бұрын
Tunaomba ya zuchu
@ycb_yakoub3584
@ycb_yakoub3584 Жыл бұрын
Swala la kurithi lafuzi hii ni kawaida kwa wamwambaoo asilimia 75% wapo hivo
@talazain1017
@talazain1017 2 жыл бұрын
Binafsi
@fatumahilaly9911
@fatumahilaly9911 2 жыл бұрын
SALAMA KIPENZI MBONA YA ZUCHU HUJAIPOSTI JAMANI IPOSTI BASI JAMANI🥺
@keifatuke99
@keifatuke99 2 жыл бұрын
Nimeosubiri ya Zuchu mpaka nimechoka
@dilipdab3714
@dilipdab3714 2 жыл бұрын
Salama.lakini.hapo.zamani.kama.hujaokotoa.vifundo.forodhani.bc.hakuzaliwa.zeji.itakuwa
@razackkalanje5049
@razackkalanje5049 2 жыл бұрын
wekeni ya zuchu
@oscarmwakibinga1142
@oscarmwakibinga1142 2 жыл бұрын
Aliezaliwa haoni kwani anajua rangi ya damu?
@oyay2821
@oyay2821 2 жыл бұрын
Haya maneno ya kuzungu kama inferior, insight au relate waTz wanafahamu?
@kdloon2030
@kdloon2030 2 жыл бұрын
Tueleze wewe mzungu
@tuesdaymeli8458
@tuesdaymeli8458 2 жыл бұрын
😄😄😄😄😄😄😄😄 hawa wote mm nawapenda
@razackkalanje5049
@razackkalanje5049 2 жыл бұрын
Tuwekeeni ya zuchu
@dilipdab3714
@dilipdab3714 2 жыл бұрын
Wanaokota.vifundo.sio.miwaa
@saidahmed9688
@saidahmed9688 Жыл бұрын
meena tunakupenda
@dilipdab3714
@dilipdab3714 2 жыл бұрын
Kifundo.chamuwaa
@barikilangoy4737
@barikilangoy4737 2 жыл бұрын
Utuletee na diwani wa mama ashura
@jrsaid4270
@jrsaid4270 Жыл бұрын
We kijana acha masihara 🤣🤣
@barikilangoy4737
@barikilangoy4737 Жыл бұрын
@@jrsaid4270 sio masihara naona kama zinaendana tufanye kama hii episode 1 afu ya diwani wa ashura episode 2
@jrsaid4270
@jrsaid4270 Жыл бұрын
@@barikilangoy4737 🤣🤣🤣🤣 Mr Pimbi he!? 🤣🤣
@josephmuchiri3180
@josephmuchiri3180 2 жыл бұрын
Mbona sasa anachekacheka
@mwanaidikhatibu4726
@mwanaidikhatibu4726 2 жыл бұрын
Tunamumba dinaa marios
@Boaz22
@Boaz22 2 жыл бұрын
Alisikiaje baada yakuhusishwa kwenye video ya Ngono???😩
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 жыл бұрын
Part 2 kajieleza.
@jean-Robert
@jean-Robert 2 жыл бұрын
Tunaitaji interview yako na zuchu aipo youtube kwanini?
@ashurantandu1799
@ashurantandu1799 2 жыл бұрын
Kuongea kingereza ndo kupotezana mada
@fahadfahmy
@fahadfahmy 2 жыл бұрын
Kiswahili fasaha
@faizadiriye1384
@faizadiriye1384 2 жыл бұрын
Salama mbona humuweka zuchu
@bjzee1981
@bjzee1981 2 жыл бұрын
Hiyo hata sio kichekesho. Bora mgombea urais wa Kenya wajakoya
@mwanajumamohammed6327
@mwanajumamohammed6327 2 жыл бұрын
Meena ni mtoto wa master j ama mm ndio sijui
@fathimaf1048
@fathimaf1048 2 жыл бұрын
Hapana dear meena ni mtu wa Zanzibar na Master j ni mtu wa kilimanjaro wapo kikazi
@mwanajumamohammed6327
@mwanajumamohammed6327 2 жыл бұрын
Asante dear...sikuona ubaya kuuliza...maana sijui na misio Mtanzania...ni mkenya na pia cko Kenya niko safar
@mtanzaniahalisimungunimwem673
@mtanzaniahalisimungunimwem673 2 жыл бұрын
@@mwanajumamohammed6327 mhhhh
@kingkinye1419
@kingkinye1419 2 жыл бұрын
Singeli hii Kali sanakzbin.info/www/bejne/hKbceqpmlLCkeNU
@christopherpeter3112
@christopherpeter3112 2 жыл бұрын
Zuchu lini
когда повзрослела // EVA mash
00:40
EVA mash
Рет қаралды 4,2 МЛН
Salama Na RIYAMA Ep 32 | UTAKWENDA UTARUDI Part 1
34:34
YahStoneTown
Рет қаралды 178 М.
BSS 2022 SE13EP03 SALAMA JABIR FULL SHOW
1:32:37
BongoStarSearch
Рет қаралды 27 М.
POR QUEEE DIVERTIDA MENTE 2 !!! #SHORTS
0:15
Figuritalo
Рет қаралды 23 МЛН
🤣МАЛО КУПИТЬ ЛОШАДЬ
0:18
Бутылочка
Рет қаралды 5 МЛН
Слепой парень помог раскрыть тайну 😱
0:45
Фильмы I Сериалы
Рет қаралды 1,7 МЛН
Sigma Girl Past #sigma #funny #comedy
0:20
CRAZY GREAPA
Рет қаралды 4,6 МЛН