MV MWANZA HAPA KAZI TU YAFIKIA ASILIMIA 96 KUANZA SAFARI ZAKE AFRIKA MASHARIKI HIVI KARIBUNI

  Рет қаралды 5,691

GSengo

GSengo

Күн бұрын

NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Meli Mpya ya kubeba Abiria na Mizigo ya MV Mwanza hapa kazi tu, kwa mara ya nyingine imefanya safari ya majaribio ya kiufundi katika Ziwa Victoria.
Mara baada ya majaribio ya siku 3, Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa anaongoza zoezi la ukaguzi wa Mv Mwanza Hapa Kazi Tu, iliyoondoka katika Bandari ya Mwanza Kusini ikiwa na jopo la wadau, wakiwemo Wahandisi, Wakandarasi, Wandishi wa Habari pamoja na Wataalam waliokuwa wakiijenga meli hiyo.
Eric Hamisi ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini na hapa anaeleza zaidi ni yapi yaliyosalia kwa ujenzi wa meli hiyo ili kuanza safari zake.
Meneja Mradi wa Ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza hapa kazi tu Vitus Mapunda amesema majaribio hayo ni ishara ya kukamilika kwa Ujenzi wa Meli hiyo, nao wakiwa na dhamana ya kuilinda na kuitunza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya huduma za Meli MSCL Meja Jenerali Mstaafu John Mbungo amesema Watanzania wanapaswa kuona fahari kubwa ya ushiriki wao katika Ujenzi wa Meli hiyo.
Wakazi wa Jiji la Mwanza wameipongeza Serikali kwa kukamilisha Ujenzi wa Meli hiyo.
Meli ya MV. Mwanza hapa kazi tu yenye uwezo wa kubeba Abiria 1,200, Tani 400 za Mizigo, si chini ya Magari Madogo 28 na Malori Matatu unatarajiwa kukamilika ndani ya Mwaka huu ambapo Ujenzi wake ulianza Mwaka 2019 ukitekelezwa na Mkandarasi kutoka Korea ya Kusini zikishirikiana na Suma JKT ya Tanzania, Mradi huo umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 127 za Kitanzania.

Пікірлер: 6
@HJ-wf2vi
@HJ-wf2vi 3 ай бұрын
Yaani 50b zaidi ya kilichokadiriwa khaaaaaah
@ramaaman4020
@ramaaman4020 Ай бұрын
Very good
@khamissaleh921
@khamissaleh921 Ай бұрын
Imefeli mbona haijaanza kazi mpaka leo July 😊
@SAADAOTHMAN-tn7ur
@SAADAOTHMAN-tn7ur 4 ай бұрын
Kazi mzuri
@khamissaleh921
@khamissaleh921 Ай бұрын
Mbona tuko july kimya nini sababu?
@khamissaleh921
@khamissaleh921 Ай бұрын
Mbona kimya kulikoni haijaanza ?
Tanzania set to export power to Zambia
2:12
CGTN Africa
Рет қаралды 15 М.
这三姐弟太会藏了!#小丑#天使#路飞#家庭#搞笑
00:24
家庭搞笑日记
Рет қаралды 92 МЛН
wow so cute 🥰
00:20
dednahype
Рет қаралды 31 МЛН
КАКУЮ ДВЕРЬ ВЫБРАТЬ? 😂 #Shorts
00:45
НУБАСТЕР
Рет қаралды 3,5 МЛН
Blue Food VS Red Food Emoji Mukbang
00:33
MOOMOO STUDIO [무무 스튜디오]
Рет қаралды 19 МЛН
IFAHAMU MV.VICTORIA  ILIVYOKUWA NA SASA INAVYORUDI KATIKA UPYA WAKE
10:39
KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI -MSCL
Рет қаралды 40 М.
TAZAMA UZURI WA MV.MWANZA  ITAKAPO KAMILIKA..
6:07
KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI -MSCL
Рет қаралды 41 М.
KARIBU MWANZA: Jionee kisiwa kiitwacho "SAA NANE"
6:59
Millard Ayo
Рет қаралды 64 М.
BMG TV: Mapya yaibuka sakata la Kisiwa, Mlima kuuzwa Mwanza
17:40
BMG ONLINE TV
Рет қаралды 31 М.
这三姐弟太会藏了!#小丑#天使#路飞#家庭#搞笑
00:24
家庭搞笑日记
Рет қаралды 92 МЛН