Рет қаралды 42
“Tangu tufanye mabadiliko ya Sheria ya Madini mwaka 2017 na baadaye ikafanyiwa marejeo mwaka 2019, katika utekelezaji wa mabadiliko hayo, Serikali imeweka takwa la kikanuni na kiutaratibu kwamba hakuna mchimbaji mkubwa anayepata leseni kubwa (Special Mining License - SML) na kwenda kuuza nje ya nchi kama malighafi ni lazima aje na mpango wa kuyaongezea thamani hapa hapa nchini”
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa wakati akifunga mafunzo ya Siku tatu ya uongezaji thamani madini ya vito kwa nadharia na vitendo kupitia mradi wa Pamoja Initiative yaliyoandaliwa na Chama cha Tanzania Women in Mining and Mineral Industry (TWIMMI). Mafunzo yaliyofanyika katika kituo cha Madini na Jiosayansi African Minerals and Geosciences Centre (AMGC) jijini Dar es Salaam.