Рет қаралды 3,865
Wananchi wa Kitongoji cha Simbalivu wamekubali kujiandikisha ili waweze kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika 27/11/2024 ambapo watachagua mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa kitongoji na wajumbe ambapo Mkuu wa wilaya ameruhusu waendelee kuosomeka kata ya Chalangwa na Kijiji cha Itumba
Mpaka muda vituo vinafungwa wananchi zaidi ya mia mbili (200) wamejiandikisha kwenye daftari la mkazi la kitongoji na ikumbuke ni wastani wa masaa matatu tu yametumika kuandikisha idadi hiyo ya wananchi. Ni siku Mbili tu zimesalia kuhitimisha zoezi la uandikishaji hivyo bila shaka wananchi wa Itumba watatumia muda huo kuhakikisha wote wenye sifa wamejiandikisha