TAARIFA NYINGINE KUBWA HII HAPA IMETUFIKIA LEO KUTOKA MWANZA KUHUSU DARAJA LA MAGUFULI

  Рет қаралды 11,240

ICON TV TZ

ICON TV TZ

Ай бұрын

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kutekeleza mradi wa Ujenzi wa daraja la JPM (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa KM 3.2 linalojengwa na mkandarasi China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa gharama ya zaidi ya Tshs. Bilioni 716.
Hayo ameyasema leo juni 10, 2024 alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa daraja la kigongo - Busisi ambapo amesema chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Mwanza, ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 88.2 na akatumia wasaa huo kuwapongeza kwa kazi nzuri.
"Nimeona kazi nzuri mnayoifanya, ninawapongeza sana na ninatoa wito kuendelea kusimamia vizuri na kwa kasi ile ile ili mradi huu ukamilike kwa wakati ifikapo disemba 30 mwaka huu".
Mtanda ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kujenga daraja hilo kwa kasi kwani Rais Samia amelikuta likiwa chini ya asilimia 40 kiujenzi na hata malipo ya fedha lakini ndani ya miaka mitatu limeendelezwa bila kusimama na kwamba sasa wananchi wataondolewa adha ya msongamano kwenye vivuko.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutatoa fursa kwa mikoa ya Kanda ya ziwa na nchi za jirani kuwa na hakika wa kufika kwa urahisi vilevile utasaidia kupunguza msongamano w magari kwenye vivuko vinavyotumika sasa na kwamba utarahisisha suala la usafiri kwa ujumla.
Mwakilishi wa Meneja wa TANROAD Mkoa huo Mhandisi Richard Ruyango amesema awali ujenzi wa daraja hilo linalogharimu ulioanza mwaka 2020 ulitarajiwa kukamilika mwezi februari mwaka huu lakini kutokana na sababu mbalimbali mkandarasi huyo aliongezewa muda.
"Hatujaona mpango wa kujenga mzani upande wa Sengerema hivyo tunaomba ujengwe ili kulinda daraja letu maana uwekezaju huu ni lazima ulindwe kwa kuweka ukomo wa uzito wa magari kupita ili lidumu muda mrefu." Mhe. Hamis Tabasam, Mbunge wa Sengerema.

Пікірлер: 25
@omzedstationary932
@omzedstationary932 27 күн бұрын
"VIVAA...TZ VIVAA".
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ 27 күн бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@LuckymusyokiLuckymusyoki
@LuckymusyokiLuckymusyoki Ай бұрын
Shida iko wapi pesa hakuna ama ,mm naona hivo daraja hadi Leo bado mnaongelelea wapuuzi nyinyi,mnakula pesa za watanzania ,mnafaa kunyongwa
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@MohamedRashid-py7ro
@MohamedRashid-py7ro Ай бұрын
Kuna madaraja nchi mengi tu jamekatika na sehemu nyingi tu nchi kunaitaji madaraja bora mbona hao watanzania mnao wasifia hapo hatuwaoni kujenga je navifaa vya ujenzi vya kisasa wanavyo au kusema tuna mainjinia vitendo hakuna
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@user-gv8yn9lg1i
@user-gv8yn9lg1i Ай бұрын
Sawa, mama anajitahidi, je ninyi mmezidi maneno tu.
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@user-gv8yn9lg1i
@user-gv8yn9lg1i Ай бұрын
Maneno mengi, utendaji kidogo, hilo daraja angekuwepo Jpm lingekuwa tayari.
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@user-gv8yn9lg1i
@user-gv8yn9lg1i Ай бұрын
@@ICONTVTZ 🙏
@user-gv8yn9lg1i
@user-gv8yn9lg1i Ай бұрын
@@ICONTVTZ hapo sawa
@amirjuma9395
@amirjuma9395 Ай бұрын
Analazimisha aonekane kwenye TV kwakweli mnafikiri sisi watanzania ni wajinga hatujui kuchambua mambo? Kiukweli speed ya kumaliza ujenzi ipo chini sana magufuli angekuepo tushasahau izo porojo zenu miradi yote inaenda mwendo wa kinyonga hata soko la tandale bado kariakoo bado treni bado
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@mussachichajr
@mussachichajr 28 күн бұрын
Shigongo nani kakuambia tunataka daraja kutoka dar kuja zanzibar
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ 28 күн бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@MohammedJaizan-yf5yt
@MohammedJaizan-yf5yt Ай бұрын
SI ajabu ukasikia hata hiyo trh 30 ikawa bado . Hakuna miradi ya hovyo kama miradi ya mza . SI kweli kufanya miradi wenyewe hiyo ni kama kutwanga maji kwenye kinu
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@saidabdallah2649
@saidabdallah2649 Ай бұрын
Hakuna mbunge hapo unaongelea mezani wkt kabla na baada mizani kote zipo..mi nilijua ulinzi wa mazingira na kuwa mataa ili liwe kivutio unaleta story zingine bdo wabunge wetu sana
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@mawazoaliselemani
@mawazoaliselemani Ай бұрын
Hawa wakuu wa mikoa mingine mboni magumashii mizani ya nini?
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
@SelijusiMalambo-rh6sf
@SelijusiMalambo-rh6sf Ай бұрын
Wezi wakubwa tabasamu hajuwi kusoma wajinga ww siumesomea makalatasi mnajua nini chamaana nimiongoni mwawasomi WA pumbavu
@ICONTVTZ
@ICONTVTZ Ай бұрын
Asante Kwa Kutufuatilia
БАБУШКИН КОМПОТ В СОЛО
00:23
⚡️КАН АНДРЕЙ⚡️
Рет қаралды 16 МЛН
New model rc bird unboxing and testing
00:10
Ruhul Shorts
Рет қаралды 26 МЛН
Mama vs Son vs Daddy 😭🤣
00:13
DADDYSON SHOW
Рет қаралды 39 МЛН
Ronaldinho Gaucho Goals That SHOCKED The World
7:01
iLance7i
Рет қаралды 8 МЛН
KIVUMBI! MBOWE AMKATAA RAIS SAMIA AWALIPUA WAZANZIBARI
8:35
Yuhai media
Рет қаралды 30 М.