Рет қаралды 8,879
Katika nyakati za vita baridi, ujasusi, uhasama na hujuma zilikua ni sehemu ya mchezo. Mafahali wawili wa dunia yaani Marekani na Shirikisho la Sovieti walihasimiana na uhasama huu ulisambaa na kuigawa dunia katikati.
Nchi nyingi ikiwemo Tanzania ziliamua kutofungamana na yeyote. Hii haikua kinga, bali uhasama uliendelea mpaka ndani ya nchi hizo.
Tanzania kuwa makao makuu ya ukombozi Afrika pamoja na ushawishi alioujenga Nyerere, ilifanya viunga vyake kuwa uwanja wa mapambano ya vita baridi.
Mashirika ya kijasusi yalipambana kushawishi, kutafuta taarifa na kusajili vijumbe. Mashaka na kutoaminiana ilikua ni maisha ya kila siku.
Mwaka 1965 lilitokea tukio Tanzania, tukio liloleta mvutano wa kidiplomasia, ilikuwa ni sehemu ndogo ya matukio yaliyosababishwa na uhasama wa vita baridi. Fuatilia Makala hii: