Tazama Misemo Ya Mchungaji Hananja Ilivyomvunja Mbavu Salama | SALAMA NA RICH BILIONEA PT 2

  Рет қаралды 268,181

YahStoneTown

YahStoneTown

Жыл бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Kipindi cha nyuma kidogo nilifanya lile ambalo huwa nafanya la kuwashirikisha rafiki zangu na team kuhusu list ya watu ambao wangependa kuwaona kwenye kiti chetu chakavu na sababu za kwanini hasa waje kwenye meza ile yenye kigae kwa juu maana tukisema tutaje majina tu bila ya sababu thabit za wao kuja pale tunaweza tukaondoa maana yenyewe ya kuwa na watu wenye story za kuvutia na kutufunza kama ambavyo tumekua tukifanya. Jina la mgeni wetu huyu lililetwa kwangu na Michael (Mx) Mlingwa na Ndugu yangu Elbogast Myaluko ndo alinipatia mawasiliano naye na kuanzia hapo mengine yamebaki kukhadithiwa kama hivi.
Sikua namfahamu Mchungaji Richard Hananja mpaka Michael alipo niambia nami nikachukua muda wangu wa kwenda kufanya ka research kangu kabla hajaja mezani, ambacho nilijifunza ni kwamba Mchungaji alikua ni mtu mashuhuri sana ambaye ana watu wengi sana pia wanao mskiliza. Ilinichukua takriban miezi miwili kuweza kumpata maana kila weekend (mara nyingi rekodi za kipindi huwa zinafanyika weekend) yeye huwa yuko safarini. Huitwa sana sehemu mbali mbali, na sasa Serikali nayo imekua ikimuita pia katika matamasha na mikutano mbalimbali. Kwahiyo mara utamsikia yuko Dodoma, mara Moshi, mara Iringa ilimradi yuko busy. Na wakati mwengine Jumapili yake inakua ya yeye kualikwa kwenye Makanisa mbalimbali ili akatoe neno, siku hizi yeye ameshastaafu kuhubiri kanisani na sasa zilizobaki ni hizo za mialiko maalum.
Kama kawaida mimi na wenzangu tulitaka kuanza kwa kumfahamu mgeni wetu maana kama nilivyokuambia hapo awali mimi sikua namfahamu zaidi tu ya kumuona kwenye mitandao akimwaga cheche, tulianzia kwenye kuzaliwa kwake na kukua kwake, mitihani mbalimbali ya ujana, bishara na kazi ambazo ashawahi fanya, na wakati naandika hii nimejifunza pia kuwa Mchungaji hana ambalo anaongeza chumvi maana baada ya sisi kufanya nae maongezi haya, nimeona ameenda sehemu tofauti tofauti na story yake haijawahi kubadilika.
Ujasiri wa ziada huhitajika ili tuweze kufanikiwa kwenye maisha yetu na pia kuwa kwenye mstari ili usiingie kwenye matatizo na vyombo vya sheria. Mchungaji ananiambia jinsi ambavyo alikua ana hustle kila kona, kusafiri bila ya kibali cha kuvuka mipaka ya nchi na boxing ambayo aliifanya kwenye kipindi flani kwenye maisha yake. Boxing imemuachia kovu ambalo kila siku linamkubusha mapambano ambayo ameshawahi kuyafanya kwenye maisha yake.
Boxing pia ndo ambayo imemfanya awe na discipline ya hali ya juu. Kwenye maisha yake ya sasa Mchungaji Hananja anatoa nafasi kwa kila aliye kata tamaa au ambae watu wamemkatia tamaa, yeye ndo huwachukua hao na kuwapa nafasi nyengine kwenye maisha yao, na amini usiamini wengi wao hunyooka na kuanza upya. Kwenye nyumba yake huko Madale Mchungaji anafanya mambo mengi ikiwa pamoja na kilimo na ufugaji. Swali langu lilianza kwa kutaka kujua hizo pesa za yeye kuweza kufanya mambo yote hayo, huwa zinatoka wapi?
Mchungaji Hananja ni MUME, na kwa mujibu wa maelezo yake, alichelewa saana kuoa na mkewe ni Rafiki yake wa kwanza. Yangu matumaini moja mbili tulizopiga humu zitakupeleka sehemu.
Tafadhali enjoy.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪KZbin Link bit.ly/KZbinSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 347
@gb-one6435
@gb-one6435 Жыл бұрын
Nimepata majibu ya mengi kupitia Interview hii kuhusu maisha, uchumi, Imani na mengine mengi 🤝💪
@noahmallango8223
@noahmallango8223 18 сағат бұрын
Ahsante sana baba mchungaji Hananja umetufungua kifikra namna ya kufikiri kwa mapana zaidi ili kupata ukombozi wa kiuchumi
@farajalongo4528
@farajalongo4528 Жыл бұрын
"Shetani haonei mtu asiyekuwa na akili." 🙌🤛
@rosemilingi7860
@rosemilingi7860 Жыл бұрын
Nikweli kbs
@renatuskanuthy5743
@renatuskanuthy5743 Жыл бұрын
umenifanya nicheke
@swahiliwithZita
@swahiliwithZita Жыл бұрын
Hii like 100 ni yangu natamani nilike Mara Mia Mia what an interview!
@user-tz4uy1rp6f
@user-tz4uy1rp6f 4 ай бұрын
Natamani sana vijana wote wangeisikiliza hii interview. Kwa kweli ni mafundisho muhimu kwao. Asante sana.
@eliasmtaki8518
@eliasmtaki8518 Жыл бұрын
Dada leo hakuna msosi wala juisi😊😊..ni nondo mwanzo mwisho. Nice interview..Mwamba sio wakuulizwa maswali meengi. Ni kumchokoza na kumwacha atambae
@reubensimon3556
@reubensimon3556 7 ай бұрын
🤣🤣🤣
@thomaskiponda6079
@thomaskiponda6079 7 ай бұрын
❤❤❤❤❤❤❤😂😂😂😂😂😂
@estergideon2039
@estergideon2039 5 ай бұрын
Amini😂😂😂
@farajalongo4528
@farajalongo4528 Жыл бұрын
"Umeletwa ili usaidie, siyo usaidiwe." 🙌🤛
@dorinitemba8074
@dorinitemba8074 Жыл бұрын
Hakuna kushindwa kwenye maisha,bado maisha yapo,maisha yamapambano yanakufanya uwe imara...asante Mchungaji Rich..
@sammarius2415
@sammarius2415 Жыл бұрын
Salama , ubarikiwe sana , kutuletea mtu na nusu , bonge la elimu , billionaire ni full package abarikiwe sana 🤝🤲
@peterkichochi7510
@peterkichochi7510 Жыл бұрын
JAMANI TUCHICHEENI BASATA WAMPE TUZO YA KUFAFANUA KUHUSU MTU NA DINI ALIYO TOKEA... THIS IS REALLY REALLY REALLY HARD TALK
@farajalongo4528
@farajalongo4528 Жыл бұрын
"Jambo la kwanza siyo maombi. Jambo la kwanza ni Ukombozi wa fikra." 🤛🙌
@September69able
@September69able 5 ай бұрын
"Mpigania uhuru wa kiuchumi", Asante sana Mchungaji.
@ismaelmatano3571
@ismaelmatano3571 Жыл бұрын
Aslam aleikum salama hope everything well on your side, I'm from Kenya and I really enjoyed your interview with rich billionaire and the previous interviews too.. Wanna request if possible to bring him back again coz he's educate so many people in this world. And it's gives people not to give up in life.. SALAMA we love you and Allah bless you good things happen to you. xxx
@JosephJasson
@JosephJasson 7 ай бұрын
Ubarikiwe dada kwa kutuletea huyu mtumishi wa Mungu
@leahsangawe9609
@leahsangawe9609 Жыл бұрын
Huyo baba nii was aiana yake, humble, helpful and passionate. Hatuchoki ukimsikiliza. Ujumbe wa kutosha! Tutaufanyia kazi . Thanks Salama. Good work!!
@kambamazig02024
@kambamazig02024 Жыл бұрын
Salama, swali lako kuhusu imani na dini pamoja na sayansi ni zuri mno na limewagusa wengi sana, pia nashukuru kwa patience uliyonayo wakati unamuuliza maswali.
@manuelykimaro9995
@manuelykimaro9995 Жыл бұрын
Kwa kweli Aliposema kuhusu muda ameni inspire mambo mengi
@mickmadinda110
@mickmadinda110 Жыл бұрын
Hii ntarvew imenifunza na imeongeza kitu kwenye Maisha Yangu kupitia hii interview naenda kua tajiri huu Mwaka imenipa ujasir Zaid ya kutafuta ishi Sana Salama na Father apo rich billionea mchungaji
@barakakusa7606
@barakakusa7606 Жыл бұрын
Tufanye ibada ndugu zangu, Mim Huwa naumia Sana napokuta mtu wa dini fulani anamchukia wa dini nyingine,
@zaqiamhando6522
@zaqiamhando6522 Жыл бұрын
Best interview 2023🙌 nmepata majibu ya maswali
@dreusebiusjmikongoti248
@dreusebiusjmikongoti248 Жыл бұрын
"NDANI YA UJANA KUNA UTAYARI WA KUFANYA KAZI" #WALK_THE_TALK
@farajalongo4528
@farajalongo4528 Жыл бұрын
"Imani siyo kuelewa, Imani ni kukubali." 🙌🤛
@peacemuzaliwa2563
@peacemuzaliwa2563 9 ай бұрын
Uyu mzee ni Mzalendo ...i wish to meet you Mentor wa Taifa. Salama asante mzee ametufunza mengi.#One Love
@godifalsafa
@godifalsafa Жыл бұрын
Nilijihisi kuwa nipo kwenye lecture room nakula nondo ❤
@naidamwakibinga6309
@naidamwakibinga6309 6 ай бұрын
Hongera sana dada mungu akubariki na Asante sana mchungaji kwa ushauri mzuri 🙏🙏🙌🙌💯❤️❤️❤️❤️🤝
@user-ty6lr1zq7j
@user-ty6lr1zq7j Жыл бұрын
Yani natamani msimalize maana nabarikiwa sana nacheka hadi nashangaa najihisi mpya kwa maongezi ya MCH Hananja Mungu akulinde na akutunze mpendwa
@preneruth5110
@preneruth5110 Жыл бұрын
The best of the best interview..... Sisi sote ni wa Tanzania 🇹🇿 hakuna cha udini,ukabila wala rangi.. tusigombanie maini kabla mwenye ng'ombe hajachinja
@OmarOmar-cj9pn
@OmarOmar-cj9pn Жыл бұрын
Dah huyu mzee kichwani yupo vizur sana ubarikiwe
@SarahSamson-mw2xf
@SarahSamson-mw2xf Жыл бұрын
Interview Bora sana kwangu imenipa majibu mengi,good job salama kip it up.
@drisayatosiri
@drisayatosiri 6 ай бұрын
Asante Salama kwa umahiri wako ktk uandishi. Big up!
@ibramrzebra1675
@ibramrzebra1675 Жыл бұрын
Masha'Allah Tabaraka'Allah Yani mda mdogo sana, Salama tunamuhitaj tena please
@user-jw8nd4qj6n
@user-jw8nd4qj6n 7 ай бұрын
Ubarikiwe sana mchungaji,umetoa madini ya thamani sana.❤❤❤
@iduelabu4007
@iduelabu4007 Жыл бұрын
Nakupenda alafu najifunza sana kwako baba Mungu akutunze
@saidbwanakheri1471
@saidbwanakheri1471 Жыл бұрын
Funny, educational, humble, inspirational, loving, caring what an interview. Respect to you Salama and the billionaire.
@hamadysarum6862
@hamadysarum6862 Жыл бұрын
Mimi ni muisilamu Ila uyo mzee mchungaji ,nampenda sana mafundisho yake ni bora
@fredducaunt
@fredducaunt 4 ай бұрын
😂😂kwani waislamu hawapendi mafundisho yake😂
@mozasaid3869
@mozasaid3869 Жыл бұрын
Wallahi nimecheka sana, pia nimejifunza kwa nondo za Hananja
@farajalongo4528
@farajalongo4528 Жыл бұрын
"Mnajenga majengo kutega uchumi, sisi tunajenga kutega huduma." 🙌🤛
@episonfelician7670
@episonfelician7670 Жыл бұрын
Mtumish Nimekpenda Sana nimejifunza vtu we ni jasiri Mungu azidi kukupa nguvu na uishi miaka 10000000
@echolude
@echolude Жыл бұрын
This man has such fidelity to humanity; nonetheless, he speaks really fast for Kenyan ears.
@user-hf4rv7bx7s
@user-hf4rv7bx7s 5 ай бұрын
Huyu mchungaji anamjua kufundisha, ukweli huwezi kudai haki bill wajibu, wajibika na haki inakuja yenyewe. Asante kwa mauojiano Dada Salama
@Coachsamwel
@Coachsamwel Жыл бұрын
Nimeguswa sana sana sana na mchungaji huyu... Daah!! Barikiwa salama kwa exposure ya watu hawa!! We need this things to trend 📈 jaman
@peterthadeus5550
@peterthadeus5550 Жыл бұрын
Daah one of the best interviews from Bongo in recent times, Salama you are the best keep this up. Your interviewees give us relevant information and education and I'm sure I'm among many who appreciate this show.
@Pihansmo1129
@Pihansmo1129 6 ай бұрын
Huyu baba ni fighter hadi sasa anajihusisha na vinyago nafahamu vzr sana❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤
@kutokakutoka8730
@kutokakutoka8730 Жыл бұрын
Salama huu mwaka umetufungulia na mazuri sana kwa kila jambo vijana tunajioliza tumepewa majibu hongera sana salama salut kwa mzee wetu mchungaji nipo KENYA nainjoi
@farajalongo4528
@farajalongo4528 Жыл бұрын
Kule unaenda kutiwa moyo tu, muhimu FANYA KAZI. 🤛🙌
@AfiSoul103
@AfiSoul103 Жыл бұрын
Jamaniii...."Jicho lako linaona nini".. hii ni muhimu sana...
@furahadokela8633
@furahadokela8633 Жыл бұрын
Hongera sana Dada Salama, Unajua sanaaaa, interview inaubora wa hali ya juu, inavutia kusikiliza. Nimejifunza sana. SHUKRANI....
@zakariamigeto3543
@zakariamigeto3543 Жыл бұрын
Kama mmenotice salama haonekani sana atakuwa hana mbavu muda mwing sanaaa
@nicolausalex7904
@nicolausalex7904 6 ай бұрын
Hakikaaa mungu awe nawe daima mchungaji
@mussamuro752
@mussamuro752 Жыл бұрын
This will be interview of the decade.
@MarcoChali
@MarcoChali Жыл бұрын
Kabisa ✊🏾
@neemamoshi
@neemamoshi Жыл бұрын
He talks real and reality.... Nice and good thanks for this fantastic show
@noahmallango8223
@noahmallango8223 3 күн бұрын
Mchungaji Thanx ur genius
@bernadinodnawe184
@bernadinodnawe184 Жыл бұрын
I wish to meet this man one day, very humble, very intelligence man, he is third eye opened, he is just see life in a spiritual way. he see love 😍.
@__thereal_unclechibo_7953
@__thereal_unclechibo_7953 Жыл бұрын
I think he meditate
@asrasanyu
@asrasanyu 6 ай бұрын
Hata mimi nimetamaani
@khadijaymohammed4002
@khadijaymohammed4002 Жыл бұрын
ni inspire sanaaa hyu mchungaj anatoa nondooo sanaaa mungu akuweke
@tehamaacademy
@tehamaacademy Жыл бұрын
... Interview Bora kabisa kutokea kwenye ubora wako #SERMON
@athanawanjala3075
@athanawanjala3075 5 ай бұрын
Salama ni hatari. Elimu tumepata❤
@OG_20
@OG_20 Жыл бұрын
Tusisifie tu interview jamani tubonyeze na kitufe cha support ....Salama you the best Kuna mengi wenye digital media zao wana cha kujifunza kwako....keep going!
@miltonjohn9779
@miltonjohn9779 6 ай бұрын
Wew ushabonyeza?
@moshimnyeda9435
@moshimnyeda9435 Жыл бұрын
Giant wa Tanzania 🇹🇿 🤝🤝🤝👊👊
@Coachsamwel
@Coachsamwel Жыл бұрын
I love this pastor.. lazima nije kutoa chochote kwenye kituo chako kabla robo ya kwanza ya Mwaka huu kuisha.. Serious naguswa sana na mission hizi
@silverman6930
@silverman6930 6 ай бұрын
Please don’t forget if you haven’t 🇬🇧😁
@mahatakitengewamuninga1260
@mahatakitengewamuninga1260 Жыл бұрын
Best Interview 2023..MCHUNGAJI HANANJA KIBOKO
@elizabethtibenda7324
@elizabethtibenda7324 Жыл бұрын
Salama we mzur sanaaaa, na be blessed kwa kutuletea watu wa kutujenga
@salummohd4300
@salummohd4300 Жыл бұрын
Salama umemleta mtu na nusu mwenye fact za maisha.
@daffagunda-rm3hj
@daffagunda-rm3hj 8 ай бұрын
Rev, hakuna kazi bila.kumshirikisha.mungu,hata.mama anajua, lazima mwejyezi mungu asimame na kila jambo.amen.
@engfestosamson6553
@engfestosamson6553 5 ай бұрын
🎉Hongera sana maneno yako mazuri
@jumamaganga5064
@jumamaganga5064 6 ай бұрын
Maneno n mengi na hapotezi point🙌🙌
@Ramadhan.999
@Ramadhan.999 4 ай бұрын
Point inabaki imesimama
@IsraeiMwankwasya
@IsraeiMwankwasya 3 ай бұрын
Uko vema salama na mchungaji hananja Mungu awabariki
@michaelkiboya1307
@michaelkiboya1307 Жыл бұрын
Hii ni interview bora zaidi kuwahi kuitazama.
@rehemaothman2475
@rehemaothman2475 Жыл бұрын
Salama leo umepatikama hata swali Huna nafasi ya kuuliza😆😅😅🤣🤣🤣🤣🤣🤣
@ayramaa1619
@ayramaa1619 Жыл бұрын
Nakupenda sana maneno yko yananipa moyo nguvu na usabiti
@cecykaitanus7873
@cecykaitanus7873 Жыл бұрын
This is the best interview ever🙌🏽
@josephinekanju9643
@josephinekanju9643 5 ай бұрын
I'm blessed through this interview Thanks God and to U Salama and Young Rich
@nantaembanusurupia5674
@nantaembanusurupia5674 Жыл бұрын
Nimeangaliaaa nikajua Salama ndio anahojiwa!
@josephlorri431
@josephlorri431 Жыл бұрын
Salama ni mwandishi bora... umemwacha mzee aongee,nasi tumepata elimu. Kuna waandishi wengine wangemkatisha... salama ni type ya Millard ayyo
@matldakisanga9653
@matldakisanga9653 Жыл бұрын
Salama naangali Mtumishi ananipa raha mbavu zangu
@vickydan2869
@vickydan2869 Жыл бұрын
Hakika
@willykaovela5485
@willykaovela5485 Жыл бұрын
yes
@Ohhvio
@Ohhvio Жыл бұрын
Salama always the best interviewer
@jworld1480
@jworld1480 Жыл бұрын
hii mimi pia nimeliona salama is professional ever
@blandinamyinga9489
@blandinamyinga9489 Жыл бұрын
Asanteeeeeeeeee"watu huwa wanauliza mbona hunywi pombe majibu hayo"akili yangu yenyewe pombe🤣🤣🤣🤣ikinywa ni hatari
@rehemaothman2475
@rehemaothman2475 Жыл бұрын
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
@ashumohd2192
@ashumohd2192 Жыл бұрын
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
@simonrusigwa3024
@simonrusigwa3024 Жыл бұрын
Hatari sana
@filamupictures9349
@filamupictures9349 Жыл бұрын
Hata mimi. Najiona hivyo, kuwa sinywi pombe bado huwa najitafakari maamuzi na matumizi yangu naimagine ningekuwa mnywaji ningekuwa je sasa!! 😂😂
@blandinamyinga9489
@blandinamyinga9489 Жыл бұрын
@@filamupictures9349 tungekuwa wehuuu😂😂😂
@lukizatv
@lukizatv Жыл бұрын
The best lesson, utoto utumwa ,ujana maswali,uzee ugonjwa
@jacksonmacha.8613
@jacksonmacha.8613 Жыл бұрын
am rich kid..inspired by rich bilioner..lifee is good. thanks much SALAMA JABIRI for this message ..always you are at the Top ❤
@reyreh
@reyreh Жыл бұрын
In whatever he does, he sees and encourages live for one another, nampenda sana very open minded. Thanks for a great listening skill @Salama
@jeanmiruho4770
@jeanmiruho4770 6 ай бұрын
❤😂Nakupata sana billionaire Rich 5/5 från Stockholm Sweden Ubarikiwe sana
@cvanoedward3093
@cvanoedward3093 Жыл бұрын
Hongera sana Salama kwa kubuni kipindi kizuri Mungu akusimamie ufike pale unahitaji
@agatherbaluah4862
@agatherbaluah4862 Жыл бұрын
Hakuna kushindwa kweye maisha. Maisha ni kupambana jiamini.
@rasjamal9854
@rasjamal9854 Жыл бұрын
Very true maisha ni kufanya kz kupambana na Iman na subra
@mfalmekaitaba2425
@mfalmekaitaba2425 10 ай бұрын
😊😊😊 ety Imani zingine ukifa unakamuliwa hili urudi ukiwa mtupu.
@angellomarcel5677
@angellomarcel5677 Жыл бұрын
Mwamba huyu hapa..anatoa sana Elimu
@bakariomary5781
@bakariomary5781 Жыл бұрын
Yaaan mpaka nashindwa ni comments how ntacomment maana ni mgodi tena wenye kila Aina ya madini
@user-dm8oh9xe3c
@user-dm8oh9xe3c 6 ай бұрын
😅😅😅 for sure
@blandinamyinga9489
@blandinamyinga9489 Жыл бұрын
Jamani watu wa📷📸 leo nahisi wanakufa kwa kucheka🤣🤣🙌🙌🙌🙌🙌🙌 HAPANA jamani 🤣🤣🤣🤣🤣
@rehemaothman2475
@rehemaothman2475 Жыл бұрын
😅🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
@domisonrichman6499
@domisonrichman6499 Жыл бұрын
Daah mwalimu wangu kitambo sana...leo nmecheka...naomba nipate number yako ...mwanafunzi wako msasani Luther an church 2002
@erickchitumbi1308
@erickchitumbi1308 Жыл бұрын
Salama huyo mzee anayo iq kubwa sana.huchoki kumsikiliza na anachosema ukikifanyia kazi unakuwa mfano wa kuigwa kwenye maisha yako yote.
@irenemsacky5346
@irenemsacky5346 Жыл бұрын
Best interview ever
@hajiiddi2531
@hajiiddi2531 Жыл бұрын
you should be inviting smart people like these ....best pod so far💪
@nestoryremy8088
@nestoryremy8088 6 ай бұрын
Mtumishi wa mungu ubarikiwe sana na mungu akupe maisha malefu uendelee kuokoa hiki kizazi kilicho sahau kazi na kubaki kutegemea miujiza kutoka kwa watumishi wa mungu
@mbwanamtessa8607
@mbwanamtessa8607 Жыл бұрын
Dada salama pole sana leo kwa kijasho Japo leo umeyakanyaga
@jacoblaban2589
@jacoblaban2589 10 ай бұрын
BWANA YESU ASIFIWE. TUMSIFU YESU KRISTO.
@user-tt1by8ly2l
@user-tt1by8ly2l 7 ай бұрын
M. Mungu amfishe haliyakua ksmridhia
@andrewlyimo8950
@andrewlyimo8950 Жыл бұрын
Tunashukuru Sana Salama kwa kumleta Pastor hakika tumepata bonge la lesson.
@Lugongam
@Lugongam Жыл бұрын
Lifetime education from an hour interview 🙌🙌🙌,,,
@RafaelKusila-yc8iq
@RafaelKusila-yc8iq 6 ай бұрын
Asante sana salama asante hananja kwa mazungumzo wameenda vyema sana mungu awabariki nyote
@emauf
@emauf Жыл бұрын
Mchungaji wa kweli unamuona, sio kwa ubinafsi na kuahidi magar na miujiza, ila kwa kujitoa. Billionea mfano wa kuigwa.
@khadijakimana8809
@khadijakimana8809 Жыл бұрын
Mchungaji Rich is a life coach..!
@michaeljeremiah5364
@michaeljeremiah5364 Жыл бұрын
Mungu akubariki sana salama...,🙏🙏🙏🏆
@abdulbongekapunye
@abdulbongekapunye Жыл бұрын
Salama wewe leo unacheka tuu hiii tamu sana
@rehemaothman2475
@rehemaothman2475 Жыл бұрын
Na maneno mazito akimalizia eeeeeeheeeeee
@user-kp5zu2nh5n
@user-kp5zu2nh5n 4 ай бұрын
Bwana Yesu asifiwe, jamani nisaidie ni namba za mchungaji hananja wana wa Mungu
ОДИН ДЕНЬ ИЗ ДЕТСТВА❤️ #shorts
00:59
BATEK_OFFICIAL
Рет қаралды 8 МЛН
Tom & Jerry !! 😂😂
00:59
Tibo InShape
Рет қаралды 63 МЛН
UTOTO UTUMWA, UJANA MASWALI, UZEE MASWALI
46:42
CLOUDSMEDIA
Рет қаралды 254 М.
MCH.RICHARD HANANJA AWAVUNJA MBAVU WA SONGWE.
16:15
KAYUNI ONLINE TV
Рет қаралды 145 М.
Парень со странностями помог мальчику 🥺 #фильмы #сериалы
1:00
DixyFilms - Фильмы и сериалы
Рет қаралды 3,8 МЛН
THE POLICE TAKES ME! feat @PANDAGIRLOFFICIAL #shorts
0:31
PANDA BOI
Рет қаралды 23 МЛН