WAZIRI SILAA USO KWA USO NA MUSHI ALIE JENGA GHOROFA ENEO LA WATU | WEWE NI TAPELI NA.......

  Рет қаралды 64,667

RAI TV

RAI TV

Ай бұрын

MUSHI ATUHUMIWA KUJENGA GHOROFA KWA MTU
•WAZIRI SILAA AELEKEZA ARUDISHIWE MWENYEWE
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema ghorofa lililojengwa katika kiwanja namba 487 Mikocheni jijini Dar es salaam litarudishwa kwa mwenyewe Bw. Fatael Anderson baada ya uchunguzi wa nyaraka uliofanyika kubaini kuwa limejengwa na Kampuni ya Jued Homes Limited inayomilikiwa na Bw. Paul Meenda Mushi ambaye awali alitajwa kama tapeli namba moja wa viwanja jijini Dar es salaam.
Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara katika eneo hilo akiambatana na mmiliki halali wa eneo hilo Bw. Fatael Anderson ambapo amekuta kiwanja hicho kimejengwa Ghorofa na limekuwa likitumika kwa biashara na ofisi mbalimbali.
Amesema Kiwanja hicho kiliandaliwa hati namba 52250 ya miliki ya miaka 33 kuanzia tarehe 01/01/1984. Hata hivyo Fatael Anderson hakuwahi kusaini rasimu ya hati wala kuchukua hati hiyo ambapo tarehe 12 Machi 2004 Mushi alighushi nyaraka zote kwa kutayarisha hati na kisha kufanya uhamisho wa miliki hiyo kutoka jina la Ndg Fatael Anderson kwenda Kampuni ya Jued Homes Limited.
Silaa amesema tarehe 15/02/2010 kampuni ya Jued Homes Limited walitoa tangazo la kuomba kubadilisha matumizi ya kiwanja kutoka Makazi Kwenda Makazi na Biashara. Mabadiliko hayo yaliidhinishwa na Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji tarehe 20/07/2012.
Katika uchunguzi wa nyaraka imebainika kuwa Kampuni ya Jued Homes Limited (inayomilikiwa na Bw. Paul Meenda Mushi) ilighushi nyaraka zote kwa kutayarisha hati kwa jina la mmiliki Ndg Fatael Anderson na kisha kufanya uhamisho wa miliki hiyo.

Пікірлер: 136
@user-qh2bx5em6j
@user-qh2bx5em6j Ай бұрын
Silaa napenda tu unavyoongea unamwelewesha Mtu jambo mpaka anaelewa Mungu akubariki Sana
@imraniqbal00765
@imraniqbal00765 Ай бұрын
Ktk serikali ya mama samia kuna vijana watatu mimi nawakubali sanaa Mama hakukosea kabisa kuwa chagua Jery slaa,bashe,makonda
@kristofuraha3369
@kristofuraha3369 Ай бұрын
Yani nimegundua hata Lukuvi wakati akiwa waziri wa ardhi hakuwahi kufikoa viwango vya utendaji wa JERY SLAA.
@user-yu1xi7dh4o
@user-yu1xi7dh4o Ай бұрын
Mtoe bashe kabisa ni msanii ni kwa vile humjui tu ni fundi kujieleza na kupangilia hoja zake ndo pale anawachanganya watu ila ni mwizi mzoefu na mwizi fundi timu mwiguru nchemba.
@paschalpaul3862
@paschalpaul3862 Ай бұрын
Kwa upande wa bashe kuna ukakasi wa tuhuma mbalimbali kwenye tenda za kilimo na hivyo ipo siku Bashe atapigwa spana japo kwa macho ya nyama anaonekana mtendaji mzuri lakini kuna harufu za ubadhirifu zinamzunguka
@mohammedibrahim1629
@mohammedibrahim1629 Ай бұрын
Awesu waziri wa maji
@gandeone1585
@gandeone1585 Ай бұрын
Waziri wa Ujenzi Umemsahau
@femidayahaya4882
@femidayahaya4882 28 күн бұрын
Kabla hata cjazaliwa Mzee kadhulumiwa😢😢 Ndo haki yake anaipata Leo...Nimeamini riziki ya Mtu haipotei hata kama ikichelewa ila itarudi kwake...Mungu ni mwenye Nguvu.
@RobertCollinskc
@RobertCollinskc Ай бұрын
Haki siku zote huzunguka na kumtafuta mwenye haki, hatimaye kapata haki yake, miaka 40 ya subra na maombi, mungu kamjibu.
@johnmalembo6464
@johnmalembo6464 Ай бұрын
Umekula bonasi ya jumba Bure baba....haki ya mwenye haki Huwa haki
@froma3732
@froma3732 Ай бұрын
Na kodi alokuwa akichukuwa alipe
@zillytash693
@zillytash693 Ай бұрын
Mshamba mkubwa unapaswa kupigwa Risas tisa kichwani ufe miaka yote hiyo Bado wasema amepata jumba Bure stupid u
@Josephineexsuper
@Josephineexsuper Ай бұрын
Mungu akulinde waziri wetu... Wananchi waone sasa huyu Paul Mushi ni tapeli kweli...watu waliona anaonewa lkn sasa ndo muone...wezi wa ardhi wana roho ngumu sana na wakavu kweli wakichukua mali ya mtu
@christinewomanoffaith5479
@christinewomanoffaith5479 Ай бұрын
Yaani wezi wa ardhi wengi kwann ni wa kasikazini? Ht yule wa Tanga the same. Huko Arusha nako makonda anawanyoosha ila wengi ni walewale
@thomastemu3332
@thomastemu3332 Ай бұрын
Hongera sana waziri wangu Jerry slaa..mama samia alichagua jembe
@gideonchilongani3421
@gideonchilongani3421 Ай бұрын
p😊0nl9
@gideonchilongani3421
@gideonchilongani3421 Ай бұрын
😊
@user-uh7to2kw2z
@user-uh7to2kw2z Ай бұрын
Huyo Moshi kila sehemu anatajwa laana mkubwa huyo Ila mwisho wake umefika amewatapeli wengi Sana muheshimiwa Slaha tunakupenda tunakuombea 🙏♥️mtetezi WA wanyonge🎉🎉
@ezehabari947
@ezehabari947 Ай бұрын
Huyu waziri Mh Rais Samia amuwekee Ulinzi vinginevyo atauwawa
@user-ii6gs2jg4g
@user-ii6gs2jg4g Ай бұрын
Mi naona serikalin kuna wachapa kazi ni wawili tu. Makonda na wewe silaa mungu awaongoze kwa mno
@angellomarcel5677
@angellomarcel5677 Ай бұрын
Makonda Bashe na Silaa waache tu hawa watu ni Noma akili nyingi alafu no Longo longo..Big up sana kwaoo
@j6sitta
@j6sitta Ай бұрын
Amen
@hamisJuma-lx2cc
@hamisJuma-lx2cc Ай бұрын
Ndug waziri tunaonewa sana na watendaji wako wa Aridhi tunanyaganywa haki zetu hivi hivi kwa7butu niusomi wa kijanja
@christinewomanoffaith5479
@christinewomanoffaith5479 Ай бұрын
Mtafute makonda
@OmanOman-dn6dj
@OmanOman-dn6dj Ай бұрын
Jery slaa Yeye kazini ni mashati meupe tu
@mwanaidimussa
@mwanaidimussa Ай бұрын
Iviii anayo mangapiiii jmn !!! Havaiiiii rangiii nyingneee y????
@OmanOman-dn6dj
@OmanOman-dn6dj Ай бұрын
@@mwanaidimussa Itakuwa Anayo Mengi..Anakuwa Anabadilisha tu
@zuwenasalim2794
@zuwenasalim2794 Ай бұрын
Huvaa mashat meupe huamaanisha yeye nimsafi wa roho mpk kwenye kazi
@ramadhanimtetu3656
@ramadhanimtetu3656 Ай бұрын
Mashati meupe Yana maanisha hataki rushwa kabisa
@user-kz7ys5qw2h
@user-kz7ys5qw2h Ай бұрын
Ni msafi Jamn huyo Mwirag
@walinaziontime7300
@walinaziontime7300 Ай бұрын
Samia Mama kwa karata bya ya Makonda na Silaa Sina Ubaya na Wewe
@emanuelmaraki9758
@emanuelmaraki9758 Ай бұрын
Duuu Mzee umelambaaa nyumbaa
@sudymgeni701
@sudymgeni701 Ай бұрын
Yani waziri kunanafasi yako kwa mungu amini usiamini.mungu akulinde maisha yako yote
@geey7893
@geey7893 Ай бұрын
Nenda Morogoro eneo la Mkundi kwa Masister kuna Mtu anajiita Almas Mvungi, ameshatesa sana Watu. Ni ziaid ya Paul Mushi
@christinewomanoffaith5479
@christinewomanoffaith5479 Ай бұрын
Yaani Majina yaleyale🙌 Ni mushi,mvungi,kimaro nk Hawa watu Wana roho ngumu jmn Hebu basi tafuteni namna ya kufikisha hizi taarifa Kwa waziri au makonda hapa sio rahisi kusoma sbb acc zinazorusha taarifa ni nyingi! au kwa AYO
@deusdeditswebe8930
@deusdeditswebe8930 Ай бұрын
Uje na Mwanza ...
@neemareuben311
@neemareuben311 Ай бұрын
Jery nakupendaaaaa wallah ww na makonda ❤❤❤❤❤❤
@user-ry8xf1no2s
@user-ry8xf1no2s Ай бұрын
Mueshimiwa laisi wangu mpendwa Samia suluhuhasani Kwa kutupa wazili Bomba sana jeli silaa Brother na kupenda sana Alha akufanyiewepesi inshallah kwenye uongoziwako
@user-nn3py9nj8l
@user-nn3py9nj8l Ай бұрын
Duuuuh....... Kwaiyo mzee anapata kiwanja na bonus ya gorofa....🤔😆 Uyo Mushi amekwishaa🙌🙌
@mwanaidimussa
@mwanaidimussa Ай бұрын
Yaan apooo kaz anayoooo ,, huyooo mzeee ni boss anatakiwaaa amuoneee kam mungu wakee ili wakaeee wayajengeee bila ivo abomoeee
@user-nn3py9nj8l
@user-nn3py9nj8l Ай бұрын
@@mwanaidimussa .... Yaa wake wakubaliane.... Atlist ampe pesa ya kufidia kiwanja chake....
@chumamasunga8855
@chumamasunga8855 Ай бұрын
​@@mwanaidimussakumbuka amefanya biashara hapo kwa miaka 40, bila kulipa chochote
@user-ex9sd8wm4l
@user-ex9sd8wm4l Ай бұрын
Allah aqbaru jamaani mbona watu wengine wanaroho mbaya hivi kweli unakuwa unakiwanja halafu mtu mwongine anajenga dah!!!
@user-qt5tx7xu8f
@user-qt5tx7xu8f Ай бұрын
MAMA.samia umechanguwa majembe.matatu.wakwanzajery Sarah wailing nimakonda.watatu.nichalamila.hao nimajembe wa tanzania
@user-eu6ql9zl7n
@user-eu6ql9zl7n 9 күн бұрын
Nampenda utulivu wake hana papara hapayuki na anakuelewesha kwa utaratibu
@dignakanje4508
@dignakanje4508 Ай бұрын
Yaani mungu àkubariki sana waziri
@HanifaOman-oo4pl
@HanifaOman-oo4pl Ай бұрын
Allhamdulillah. BBa unmepataakiyako. Silaa,Allahakupe itajiola moyowako❤❤
@jimmyfrankie8301
@jimmyfrankie8301 Ай бұрын
Huyu mzee wangu wa kilimanjaro za chini ya kapeti naskia ni balaa kwenye haya mambo ya viwanja na ardhi kwa ujumla ni nomaa hongera mh kwa kurudisha furaha ya huyo baba😂
@TitoRufizi-xb2ub
@TitoRufizi-xb2ub Ай бұрын
Nchi hii Makonda akiwa Rais na Jery waziri mkuu nchi itaenda vizuri sana
@user-yu1xi7dh4o
@user-yu1xi7dh4o Ай бұрын
Waziri mkuu tulienae Majaliwa ni mzuri mno ila walioko juu yake akitaka kufanya kitu anaambiwa shatap ndo maana wakaamua kumpa msaidizi wa kukoroga mambo
@adamapollo9859
@adamapollo9859 Ай бұрын
Kweli ila amiamuwa kuwa raisi atapita bila vikwazo maana tuna mpenda makonda awe makamo wake❤
@afraeliazaelayo
@afraeliazaelayo Ай бұрын
Asante Mungu Wetu,Kutupa Uongozi wa Nchi yetu yenye Baraka zako,wenye Roho Mtakatifu wako,wa kutenda na Kusimamia Haki. Mungu Tunakuomba,Ummbariki Rais wetu na Viongozi wote waliyo chini yake kwenye nafasi mbalimbali,aidha kwa Uteuzi wake au kwa kuchaguliwa ,Waweze kuendelea kutenda na kusimamia Haki,hasa kwa wanyonge na hata wengine wowote waliodhulumika katika kupata haki zao. Hakika Mungu Atatubariki Wa-Tanzania. Utawala wowote Ukishajali kutendea Wananchi wake haki,na kusimamia sheria ki-haki, Mungu Atatulinda nayote mabaya. Mpe Rais Wetu Timu ya kufanya kazi naye wenye hofu ya Mungu,wapende kutenda haki,na Mungu Atawabariki tu, wasiwe naharaka ya kutamani maisha ya kudhulumu. Mungu Atawahangaikia,na wao wahangaikie haki za Wa-Tanzania. Mungu Muongoze Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Muinulie Timu ya Kusaidiana na Wateule wake wakazidi kuteda na kusimamia haki. Mungu Ibariki Tanzania. Hofu Ya Mungu Ikatawale. Amen.
@RubenMtuwaMungu-bz8ee
@RubenMtuwaMungu-bz8ee Ай бұрын
Mbona nchi kubwa kwanini upore eneo la mwingine?
@lusticabernad9982
@lusticabernad9982 Ай бұрын
Nakufuatilia sana mh, ila uko vizuri sana, Mungu akutangulie Jerry❤
@SHARIFF799
@SHARIFF799 Ай бұрын
This guy should be next president of Tanzania....SILAA
@polycarpykavishe9001
@polycarpykavishe9001 Ай бұрын
Kuna watu wanajua kuchezesha balaa huyu mushi ni nuksi
@mishiabdu7478
@mishiabdu7478 Ай бұрын
Mweshimiwa mungu akuweke.nina imani na mm iko siku nitakuona utanisadia
@johnchuwa2888
@johnchuwa2888 Ай бұрын
Ndugu yangu silaa naomba usitishe zoezi linaloendelea bagamoyo.kwani kuna wahuni wakishirikiana na mahakama wavunja nyumba za watu ovyoovyo tuu kana kwamba hakuna serekali huku?naomba mtumie busara kutatua mgogoro hiyo ya aridhi mapinga.
@MrKhatibu
@MrKhatibu Ай бұрын
Paul Moshi inabidi watu wa film industry wanunue story yake na kufanya movie. Jamaa ni gangster anawaibia mpaka watu wasioibika
@shariffsagaf2305
@shariffsagaf2305 Ай бұрын
Mungu akulendi nasema ndani ya moyo
@kivuswahilitv6833
@kivuswahilitv6833 Ай бұрын
Kisha utasikia watu fulani eti CCM haifanyi kazi ila wanampongeza waziri wa CCM Nawahakikishia hakuna Tanzania bila CCM
@comfortmunuo5545
@comfortmunuo5545 Ай бұрын
Kwani Kuna chama kingine kilishaongoza hii nchi Kwa hiyo nyie Ma ccm ndio mmeharibu nchi hii kwa kuhifanya maskini na ularushwa kila mahali. Mkishafikia uchaguzi tuu mnajua jinsi ya kuwatapeli wananchi. Ila Slaa,Makonda,Bashe ,Chalamila na Mpina hawastahili kuwa ndani CCM
@MrishoHussein-oz9nr
@MrishoHussein-oz9nr Ай бұрын
Mmungu atakulinda maana kupambana na manyangau sio kazi ndogo usirudi nyuma mh mmungu yupo pamoja na ww na ss zulmiwa tupo nyuma Yako utashinda hivi vita ishaall
@MichaelmotikaLaiser-dl6wm
@MichaelmotikaLaiser-dl6wm Ай бұрын
Waziri hongera sana mungu atakulinda
@selemankishema5780
@selemankishema5780 Ай бұрын
Do!!! Injii hii hii kali
@user-nm2jq7xo5f
@user-nm2jq7xo5f Ай бұрын
Mheshimiwa siomachozi ya andason yatakulinda sio hivyo nimachozi ya wstanzania wengi wslipo dhulumiwa yatakulinda mheshimiwa waziri tetra hakiya wanyonge wapate hakizao mungu akulinde daima
@NeemaElisante-zd2dt
@NeemaElisante-zd2dt Ай бұрын
Mheshimiwa ubarikiwe sana tunaomba uje na kimara
@erickwanjarajr5707
@erickwanjarajr5707 Ай бұрын
Mzee alikuwa anapita kwa miguu jirani na kiwanja chake duu! Maisha haya.
@Theironrod9373
@Theironrod9373 Ай бұрын
Good job 👍
@batapoint
@batapoint Ай бұрын
This movie will change my life
@grationkato7658
@grationkato7658 Ай бұрын
Tanzania 🇹🇿 Tanzania 🇹🇿 tuna watu bwana
@user-ex9sd8wm4l
@user-ex9sd8wm4l Ай бұрын
Lakini hakiyako lazima utaipata tu sasa mzee wawatu leo amekipata kiwanja chake
@kleofacejerome
@kleofacejerome Ай бұрын
Watu n majasiri Asee Mushi shikamoo
@thomastemu3332
@thomastemu3332 Ай бұрын
😅mushi amekuja moshi
@thomastemu3332
@thomastemu3332 Ай бұрын
Mushi amekua moshi 😅
@MrKhatibu
@MrKhatibu Ай бұрын
Paul Mushi wewe sio tapeli ila ni mwizi jambazi wa ardhi.ona sasa unaiabisha family yako na wapendwa wako
@user-xn8jh1yw1h
@user-xn8jh1yw1h Ай бұрын
Lila ma Fila havitengamani! Walisema za Mwizi ni Harobaini! 1984 - 2024...... ni miaka 40! A m e n.
@user-iw5hu3mc7l
@user-iw5hu3mc7l Ай бұрын
Wachaga wameibiana hahaha haha na slaa mwenyewe mchaga
@MiriamAbdallah
@MiriamAbdallah Ай бұрын
😂😂😂😂 washenzi sana 😂😂😂😂😂
@albertjames6845
@albertjames6845 Ай бұрын
Acha ukabila wewe
@Mpakauseme
@Mpakauseme Ай бұрын
Si ukabila wapo wengi ni wezi katika kabila ilo wanatabia za tamaa tamaa sana ​@@albertjames6845
@vankumw3ndatalk2friends29
@vankumw3ndatalk2friends29 Ай бұрын
Hivi ni mimi tuu ndo nasikia hiyo engine ya LC300 huko nyuma 😅
@BIGBOSS-hl3bu
@BIGBOSS-hl3bu Ай бұрын
P MUSHI ANAMENGI MABAYA KAWAFANYIA WATU
@salamasefu5494
@salamasefu5494 Ай бұрын
Wachaga noma wameibiana hahaha.hawa watu sio wote wengi ni mhhhjh
@salomejohn7963
@salomejohn7963 Ай бұрын
hakika haki yamtu haipotei
@AngerusLijuja-bg6sb
@AngerusLijuja-bg6sb Ай бұрын
RAISI SAMIA UKUKOSEA KWA VIJANA HAWA MAKONDA JERY SILAA HALI API BASHE NA APA IRINA MJINI KUNA ASIKARI MMOJA YUPO UPELELEZI ANATENDA HAKI SANA JINA TU LINANITOKA YEYE NI MFUPI KIDOGO MNENE IVI KAJAZIA UKWELI NI MTENDA HAKI UYU KIJANA MPANDISHE JUU
@abbashussein-hz4dr
@abbashussein-hz4dr Ай бұрын
Jamani tunateseka weng naomben conection ya kumpata muheshimiwa namba yke anisaidie aliye nayo maana nahis kunywa sumu mm
@hajjiomary2383
@hajjiomary2383 Ай бұрын
Narudia kuomba mheshimiwa fanya mpango sech zetu ziwe na picha tumepigwa uku mtaani coz of sech
@dayana5513story
@dayana5513story Ай бұрын
Hakika Mungu nimwema
@wadeelegbogun3015
@wadeelegbogun3015 Ай бұрын
Mushi ndo jambazi wa kutupwa, hata viwanja vya NYERERE kaviiba, hata nyerere imetishiwa ni mwizi na muuji
@hatibumohamedi3471
@hatibumohamedi3471 Ай бұрын
Uyo mzee awekewe ulinzi wakutosha
@JayJay-qc1ky
@JayJay-qc1ky Ай бұрын
Nina kesi kama hii hii mwanza, watu wa aridhi walimpora mzee wgu kiwanja chake, ila wameshindwa kuchange umiliki mpk sasa, ukienda kulipia kiwanja jina la mzee lina appear kama ana viwanja wi2 kimoja ni hicho tunacho ishi na kingine ndio hicho walicho mpora, mara ya mwisho tumemtuma mtu akalipe akapewa control number ya kulipia ila wakampa control number ya kiwanja kilichopolwa na akalipia ndio sisi kujua kama bdo kipo na mpk kesho kina jina cha mzee. Nimejaribu kuntumia msg sana waziri slaa ila ajajibu wala ku acknowledge kama anapata msg , nadhani ni kwa sababu ana kazi nyingi ila nntaendelea kupambana mpk kieleweka. Yani nchi hii ni kama hakuwahi kua na waziri wa aridhi aisee.. bwana jerry anapambana mmno kuwarudishia watu furaha.
@JayJay-qc1ky
@JayJay-qc1ky Ай бұрын
Mm kama nntakipata hicho kiwanja maana jamaa kashajenga, nntataka tuelewane tu na tumalizane wala sio kumpola nyumba aliyojenga kwenye kiwanja chetu.. ila pia itategemea na yeye uelewa wake akizengua nntamwmabia aivunje nyumba atuachie kiwanja chetu.
@user-sj3wf5vz7l
@user-sj3wf5vz7l Ай бұрын
Gorofaa hilo baba Analipata
@user-nm2jq7xo5f
@user-nm2jq7xo5f Ай бұрын
Mheshimiwa tegua mitego yate yawazulumaji waende mahakamani
@chizcom4229
@chizcom4229 Ай бұрын
KICHWA CHA HABARI MBONA KAMA MMKURUPUKA "WAZIRI SILAA USO KWA USO NA MUSHI ALIE JENGA GHOROFA ENEO LA WATU | WEWE NI TAPELI "
@msafirimaulidi5054
@msafirimaulidi5054 Ай бұрын
Uyu jamaa anaitaj ulinz mkubwa sana maama majail ao lazm wanamuwinda
@angellomarcel5677
@angellomarcel5677 Ай бұрын
Sana huyu na Makonda wasipolindwa itakuwa Shida dhidi yao
@JosephHaule-yg1cf
@JosephHaule-yg1cf 23 күн бұрын
Achauhuni mahakama hutumika ndonini
@katabaroonlinetv9688
@katabaroonlinetv9688 Ай бұрын
Mwamba kapata ghorofa😅😅😅mali ya mkosaji
@wadeelegbogun3015
@wadeelegbogun3015 Ай бұрын
WAZIRI slaa mkatae mushi ni jambazi
@njeyabox7788
@njeyabox7788 Ай бұрын
Sawa ila chuma inaunguruma muda mrefu..
@ismailmasoud6001
@ismailmasoud6001 Ай бұрын
Ndio maana hakuna kitu kibaya kama RUSHWA, yaani huyo mushi ni pesa yake imemfanya apoke kiwanja cha mtu Kwa miaka 40..! Ndugu Zangu tupige vita sana RUSHWA, Kwa sababu RUSHWA ni ADUI wa HAKI ,Tena Kwa watu MASKINI
@Charlzlomo
@Charlzlomo Ай бұрын
Mwisho wa matapeli umefika
@HBI-TV
@HBI-TV Ай бұрын
Tenda haki
@azizamvungi1871
@azizamvungi1871 Ай бұрын
Ila mushi jamani unataka utajiri kwa kudhulumu.ili wiitwe tajiri?
@jeremiahngoka4980
@jeremiahngoka4980 Ай бұрын
Maigizo
@hasaabdi7199
@hasaabdi7199 Ай бұрын
Haki haizami
@abdullayahya8717
@abdullayahya8717 Ай бұрын
Huyu pacha wa Hashim Rogwe
@rayisadesigns2646
@rayisadesigns2646 Ай бұрын
HASHIM RUNGWE
@hollymore4904
@hollymore4904 Ай бұрын
​@@rayisadesigns2646ni yeye
@rehemakanyere4188
@rehemakanyere4188 Ай бұрын
Kbsaa
@digitalworld5577
@digitalworld5577 Ай бұрын
Ni kweli kabisa😅....wakati naiona picha ya clip hii nilidhani Mzee Hashum Rungwe
@user-iw5hu3mc7l
@user-iw5hu3mc7l Ай бұрын
Kwahiyo atabomoa au gorofa lake?
@KyandoSpareparts
@KyandoSpareparts Ай бұрын
ILO lake
@FredMwamgogwa-td6ni
@FredMwamgogwa-td6ni Ай бұрын
Akiamua anabomoa ni pake
@digitalworld5577
@digitalworld5577 Ай бұрын
Hii kesi yake ni complex sana, kwa sababu inahusisha utapeli na rushwa ndani yake. Inaweza ikawa ikaamuliwa mzee atakuwa anakula % fulani na mtu aliyejenga nae anakula % fulani. Huyo mwizi Paul mushi angeweza kuwa smart kabla ya kufanya huo wizi angeweza kupata lease agreement na mmiliki halisi kwa miaka ambayo wangekubaliana then mwisho wa siku jengo linarudi kwa huyu mzee mmiliki halali.
@nickylyanga2139
@nickylyanga2139 Ай бұрын
asee
@user-iw5hu3mc7l
@user-iw5hu3mc7l Ай бұрын
Huyu waziri atakua na bifu na mushi
@emmanuelbernard9552
@emmanuelbernard9552 Ай бұрын
Bifu gani hapo ? Hivi ww unafahamu kweli maana ya haki,haki ya mtu.
@ruhindacostantine2092
@ruhindacostantine2092 Ай бұрын
Kwahiyo wewe hujaona makosa ya paul
@rehemakanyere4188
@rehemakanyere4188 Ай бұрын
@@emmanuelbernard9552 hafahamu
@niffonlinetz7214
@niffonlinetz7214 Ай бұрын
ITAKUWA JERRY UMEANZA KUMFATILIA JANA KAKA POLE SANA
@salimmalaka256
@salimmalaka256 Ай бұрын
MPUMBAVU MKUBWA USI ONGEE PUMBA KWA HIYO NA HAKIMU PIYA ANA BIFU NA MUSHI???
@edwardmkwelele
@edwardmkwelele Ай бұрын
apewe tu kiwanja KINGIne sheria nazo
@Elllllllllllly
@Elllllllllllly 7 күн бұрын
Yani hapo akirudishiwa mali yake,akipige mnada chaap mambo yasije kuwa mengi
@sss3s867
@sss3s867 Ай бұрын
kwa hio unaenda kujenga rasili mali fedha kuzika kwenye nyumba ba kiwanja sio cha kwako. hii akili au matope. hebu tujalidiane hapa. yaani mzee ameramba dume kiwanja plus majengo ndio fidia yake
Now THIS is entertainment! 🤣
00:59
America's Got Talent
Рет қаралды 40 МЛН
50 YouTubers Fight For $1,000,000
41:27
MrBeast
Рет қаралды 199 МЛН
DEFINITELY NOT HAPPENING ON MY WATCH! 😒
00:12
Laro Benz
Рет қаралды 61 МЛН
Опасность фирменной зарядки Apple
00:57
SuperCrastan
Рет қаралды 7 МЛН
All creatures are from God #jesus #jesuschrist #jesuslovesyou
0:19
Jesus By Your Side
Рет қаралды 6 МЛН
MISS CIRCLE STUDENTS BULLY ME!
0:12
Andreas Eskander
Рет қаралды 16 МЛН
Summer shower by Secret Vlog
0:17
Secret Vlog
Рет қаралды 8 МЛН
НРАВИТСЯ ЭТОТ ФОРМАТ??
0:37
МЯТНАЯ ФАНТА
Рет қаралды 6 МЛН
Rang Pi Liya Mama 😂 #shorts #tiktokvideo #funnyshorts #comedy #ytshorts
0:46
Sukhasan Ka Rahman Bhai
Рет қаралды 20 МЛН