Dina Afunguka Chanzo Cha Kuacha Kazi Clouds : "Akufukuzaye Hakwambii Toka" | SALAMA NA DINA PART 2

  Рет қаралды 37,142

YahStoneTown

YahStoneTown

Күн бұрын

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Dina Marious ni STAR ambaye amakua akijenga jina lake kwa miaka mingi sana. Kama sote tunavyofahamu hakuna mtu ambaye anaibuka tu siku moja na kupata heshima na kuaminiwa kama hajafanya kazi ambayo itamfanya watu wamuamini na kumpenda. Dina yeye ameteka kabisa soko la Wanawake, kitu chochote kinachohusiana na wanawake na madhila, raha na mambo yao ya kijamii basi ukiangalia kushoto na kulia lazima utamkuta Dina yuko hapo akitoa mchango wake kwenye suala hilo. Iwe kuanzia maandalizi au uwepo wake tu. Hicho ndo ambacho yeye kama Mama na Dada na Binti ameamua kufanya, na anaweza haswa.
Alianzia Radio ya watu ya Clouds FM na baada ya kupata mtoto wake wa kwanza mitihani mingi aliipitia, ile maternity leave ambayo alikaa wakati anamkuza kijana wake ilileta mabadiliko makubwa kwenye maisha yake. Zion (mtoto wake) alipo zaliwa ilimbidi Dina aache kazi kwenye Taasisi ambayo alikua ameizoe mno na kutafuta ustaarabu mwengine bila ya kuwa na mipango hiyo wakati alipochukua likizo yake ya kwenda kujifungua. Mipango ilikua akitoka kwenye likizo yake hiyo ya uzazi basi arudi tu kazini kwake kama kawaida lakini Bosi wake wa wakati huo, Marehemu Ruge Mutahaba alikua na mipango mengine na Dina mipango ambayo kwa mujibu wake anaamini alikua akipigwa chenga tu na hakukua na mpango thabiti ambao ulikua umeekwa kwaajili yake.
Dina anakumbuka nenda rudi alizokua akizipata na kulipwa mshahara bila ya kufanya kazi yoyote, kwa kweli hilo lilikua likimsubua sana na anasema kila akiangalia kushoto na kulia alikua haoni dalili zozote za yeye kuanza kufanya kazi muda wowote wa karibu na kwasababu maswali yake mengi mazito yalikua yakipatiwa majibu mepesi mepesi aliona basi si vibaya kama atatafuta challenge nyengine kwenye maisha yake. Kwanza hiyo plan ambayo alikua amepewa hakua ameifurahia na pili majibu ambayo alikua anapatiwa nayo yalimfanya ajue pale hapakua sehemu sahihi kwake tena.
Kumuuma ilikua ikimuuma sana kama anavyosema mwenyewe, hakukua na sababu yoyote ya kutaka kufanya mabadiliko yale ambayo yalifanyika, ya kutaka kumpeleka yeye kwenye TV wakati tayari alikua ameshatengeneza kundi kubwa la mashabiki kwa wakati huo, na pengine approach iliyotumika pia haikua sahihi na hilo liliacha ladha mbaya kwenye moyo na kinywa chake, na baada ya hapo kwasababu kulikua na ofa nyengine hakufanya ajizi kuziskiliza na uzuri zaidi kwanza hapakua mbali na ofisi yake ya zamani hapo alipokua anatakiwa na pili ambalo ndo KUBWA kabisa, alikua anapewa muda ule ule wa hewani kama ambao alinyang’anywa baada ya kuenda likizo ya uzazi kwenye ajira yake ya zamani. Alikua na kila sababu ya kuchukua hatua nyengine na kujisogeza mbele zaidi, kama ambavyo tunafahamu, mtu huenda aitwapo. Na mengine ndo haya, yamebaki story tu.
Nafasi yake kwenye jumuia za wanawake ni ya kipekee na anaiweza kuikaimu vizuri tu, amekua akifanya shughuli mbali mbali za kutatua baadhi ya adha na pia kuwatunza wale ambao anadhani wanastahili ili kuwafanya wapate nguvu zaidi ya kuendelea kufanya wanayofanya kwa uzuri zaidi. Na amekua mfano mzuri hata kazini kwake maana kipindi chake cha Radio ni moja ya vipindi vinavyo sikilizwa zaidi kwa wakati ule. Hilo halina ubishi.
Kama binadamu wengine na yeye nae ana ushindi mwingi na kushindwa kwingi kwenye maisha yake na kwenye session hii tukiyagusia hayo na zaidi. Kuhusu mapenzi, mtoto, familia yake alitokea, elimu na malezi lakini pia muajiri wake wa zamani na jinsi ya kukabiliana na mambo mbali mbali maishani.
Yangu matumaini uta enjoy na kujifunza mambo kadhaa kuhusu kazi na jinsi na kujua kutafuta na kupata kutoka sehemu nyengine ukiachana na ile ulokua umeizoea.
Love,
Salama.
Support us through anchor.fm/yahs...
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL bit.ly/YahSton...
Listen our Podcast on
Spotify Link spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link bit.ly/GoogleP...
Audiomack Link bit.ly/YahSton...
‪KZbin Link bit.ly/KZbinS...
Soundtrack Yeah by @MarcoChali • Marco Chali Feat One T...
Follow:
Twitter: / yahstonetown
Instagram: / yahstonetown
Facebook: / yahstonetown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: slidedigitaltz

Пікірлер: 84
@hawaaman3172
@hawaaman3172 Жыл бұрын
Utu, hekima,uvumilivu Dina ❤❤❤❤ Golden heart interview imetulia na imenipa majibu mengi sana hakika Subra ina malipo
@BernadethaMihele
@BernadethaMihele 5 ай бұрын
Dina somo yangu hongera kwa kuwa jasili na mpambanaji nimependa story sana
@dr.sarahbusongo
@dr.sarahbusongo 2 жыл бұрын
Dina You're the Best.... I think this is the interview I was waiting to hear. Hongera Sana Salama
@lotilazaro8845
@lotilazaro8845 2 жыл бұрын
Dina uko real xan, i can feel ur humanity through ur words
@moshielfesty7992
@moshielfesty7992 Жыл бұрын
Dina nakupendaga Sana mpenzi
@catherinemwanga6227
@catherinemwanga6227 2 жыл бұрын
Unaweza sana Salama, big up sister....hongera sana Dina kwa kujibu maswali vizuri
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 2 жыл бұрын
Nime jifunza sana hapo kwa baba mtoto 🙏👌🏽
@rehemamakuburi8254
@rehemamakuburi8254 2 жыл бұрын
Good inrerview. Waswahili wanasema Milango ikifungwa upande mmoja Mola anakufungulia upande mwengine
@mgenikisinzah1564
@mgenikisinzah1564 2 жыл бұрын
Exclusive interview ni njia kuu ya kujifunza.Ahsante salama
@agnessjoseph9069
@agnessjoseph9069 2 жыл бұрын
Maisha ya kazi yana changamotooo sometimes!!!!! Dah 🙌🏻
@leaherasto929
@leaherasto929 2 жыл бұрын
Namkubali Sana Dina umepambna Sana Mungu akuzidishie baraka
@brainsngaugula6075
@brainsngaugula6075 6 ай бұрын
Dina since day 1
@happymilangasi5904
@happymilangasi5904 2 жыл бұрын
DINA YOU ARE THE BEST
@mc_mrope
@mc_mrope 2 жыл бұрын
Interview ni nzuri sana sana sana...! Hongereni sana
@sky-wz5zi
@sky-wz5zi 2 жыл бұрын
I love the story, and i love Dina 😘❤️
@niriacatering172
@niriacatering172 2 жыл бұрын
Penda Sana Salama na Dina Mungu awalinde
@ibrahimkibira9943
@ibrahimkibira9943 2 жыл бұрын
Super 👌 good 👍 excellent interview 👏 I love dinnar
@rehemarwanda6039
@rehemarwanda6039 2 жыл бұрын
Dina we mkaliiiii hatariiii🔥🔥🔥
@kissamwamunyange1018
@kissamwamunyange1018 2 жыл бұрын
Nakupenda Dina unajielewa Sana darling🌹
@hamidasaif4065
@hamidasaif4065 Жыл бұрын
Asante sana dina
@salmadulazi6876
@salmadulazi6876 2 жыл бұрын
Nampenda Sana Dina...kibonge mwenzangu...leo nimefarijika sana ...ila bado sijaelewa ile Salma Msangi imepotea wapi?mn pia nampenda Sana Somo.yangu
@mapekhamis3882
@mapekhamis3882 2 жыл бұрын
Alimuhoji Salma Msangi Mpnz Nae Yuko vzr Kwny Kujibu Maswali 🙌
@bntrashidi3083
@bntrashidi3083 2 жыл бұрын
Dina Marios Mimi Ni shabiki yako tangu 2006 ndio kwanza naingia mjini adi Leo japo apo katikati nilisafiri ila ckujua uko efm Mana niliachana na kusikiliza radio kipindi Cha magufuli mana radio nyingi zilibadilika na kuamua kumsifu magu tu Ila yote kwa yote nimejifunza mengi kutoka kwako wee ni shujaa . Nimeinjoy Sana kusikiliza iki kipindi
@mustaphareginald3264
@mustaphareginald3264 2 жыл бұрын
Keep it up sis...Salama!! We love u
@felixjunior4772
@felixjunior4772 2 жыл бұрын
Nilisoma gazette la udaku kipindi hicho kuhusu kuondoka clouds ni sababu alikuwa haelewani na zamaradi ambae alikuwa in relation na Boss
@ahmedaliabdallaali7946
@ahmedaliabdallaali7946 Жыл бұрын
Ilove you salama 💪🤲🙏
@khadijahali4837
@khadijahali4837 2 жыл бұрын
Kwl akufukuzae akuambii toka hy
@yurisongoro2895
@yurisongoro2895 2 жыл бұрын
Dina I love youuuu🥰🥰🥰🥰🥰😍😍🥰🥰🥰
@Annie-tt8fi
@Annie-tt8fi 2 жыл бұрын
Wana KZbin mmetusahau wiki hii Jamani ama? Salama na ya wiki hii Hamna?
@asiaasia5025
@asiaasia5025 2 жыл бұрын
Nakumbuka kipindi cha leo tena wakati ule kilikuwa 🔥 hapa Dina pale da Suzy na kule Geàh Habib balaam lilikuwa zito. Nilikuwa malini nacho sana kipindi cha leo tena.
@khaleedmakiya8892
@khaleedmakiya8892 2 жыл бұрын
best kipindi ever seen.
@annaabraham6999
@annaabraham6999 2 жыл бұрын
Natamani sana kukutana na Dina
@muniramunira9941
@muniramunira9941 2 жыл бұрын
💯💯
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 2 жыл бұрын
💜🎉
@GloryMsopa
@GloryMsopa 9 ай бұрын
Nimejifunza kitu jmn
@rosetasuleiman6799
@rosetasuleiman6799 2 жыл бұрын
Umenena vyema
@faudhiasalum7279
@faudhiasalum7279 2 жыл бұрын
Kumbe Salama ana mtoto uwiii duh
@zakiamseka9698
@zakiamseka9698 2 жыл бұрын
Cha ajabu nini
@maryshirima1234
@maryshirima1234 2 жыл бұрын
19:21....📌
@mankacharles4559
@mankacharles4559 2 жыл бұрын
Anae toa uhai ni mmoja tu aliyeumba ww umebeba tu kwa uheri ila muumba ni mmoja tu
@uwezomabava3949
@uwezomabava3949 2 жыл бұрын
Uyu mdada nilikuwa nampenda kabla sijamuona kila mtoto anakusudio lake akuna bahati mbaya
@xkingx8041
@xkingx8041 2 жыл бұрын
Kwani nani baba wa mtoto wetu dina ?
@angelajessala7633
@angelajessala7633 2 жыл бұрын
Ukijibiwa nitag tafadhali
@dianerditto
@dianerditto 2 жыл бұрын
Leo kupindi kimeanza mwisho kwenda mwanzo
@elizabethhonere2931
@elizabethhonere2931 2 жыл бұрын
Interview nzuri ila alizaa na nani sijui,umbea huu utanipeleka pabaya wooiii
@ceciliakija551
@ceciliakija551 2 жыл бұрын
Ruben Nchakali
@ceciliakija551
@ceciliakija551 2 жыл бұрын
Nae ni mtangazaji
@tonyriziki37
@tonyriziki37 2 жыл бұрын
Huyo ex ni Ruben Ndege"Ncha Kali!
@happyiskra7484
@happyiskra7484 2 жыл бұрын
Ohkay!!!
@husseinibnuhassan1272
@husseinibnuhassan1272 2 жыл бұрын
unajua understand zinakuja baadaye baada ya why nyingi...dina marios bonge 1 la mtu mwanamke na nusu
@nickolatharwelamila776
@nickolatharwelamila776 2 жыл бұрын
Kwani aliza nanani???
@aneththeodory8518
@aneththeodory8518 2 жыл бұрын
Ncha kali (Ruben Ndege)
@RamazaniMulongeca
@RamazaniMulongeca 2 жыл бұрын
UMEKOSEA SALAM, hii ndo Part2, but umeadika part1, Na part 1 umesema Part2 Of course wapili mimi #2
@masalakulwa7601
@masalakulwa7601 2 жыл бұрын
hata mm.naiona kama 2
@emmamatemu8225
@emmamatemu8225 2 жыл бұрын
Ndio
@ebenezanatse9436
@ebenezanatse9436 2 жыл бұрын
Soma vizuri alivyoandika.....
@RamazaniMulongeca
@RamazaniMulongeca 2 жыл бұрын
@@ebenezanatse9436 Got you son
@roseurio9600
@roseurio9600 2 жыл бұрын
Dina anajielewa sana kwakweli hana ushamba wa mabifu ila swali alivyolazwa hosptl mwez ilikuwa ni haya matatizo ya baba mtt wake??
@abdallahmdangadachi7030
@abdallahmdangadachi7030 2 жыл бұрын
Mualike mwaisa siku moja
@Jassmin-media-official
@Jassmin-media-official 2 жыл бұрын
Kwani Dina alizaa nani?natamani kujua mzazi mwenzake msahada please
@kelvinfrank8881
@kelvinfrank8881 2 жыл бұрын
Ncha kali mzee wa ubunifu pale mawinguni
@edwinmbugua7738
@edwinmbugua7738 2 жыл бұрын
Nchakali hatari sana
@zakiamseka9698
@zakiamseka9698 2 жыл бұрын
Nani huyo ncha kali?
@edwarddaniel5683
@edwarddaniel5683 2 жыл бұрын
Sebastian Maganga
@zuenahamoud1532
@zuenahamoud1532 2 жыл бұрын
Reuben ndege a k a ncha Kaliiiii
@hamadgakwaya3466
@hamadgakwaya3466 2 жыл бұрын
Kumbukumbu zangu dina Mario's aliwahikumohoji mond kipindi kile bando mdogo kweny gemu mlete tenabando anamadini mengi sana
@josephk90
@josephk90 2 жыл бұрын
Huyu dada nmempenda zaidi, mkweli mno.
@mapekhamis3882
@mapekhamis3882 2 жыл бұрын
Apo baadh ya watu maarufu(co woote) watizame waone vile majibu yanatakiwa co kujibu swali km umevurugwa au unajickiiiia kujibu swali 😀😀😀
@Hashdough
@Hashdough 2 жыл бұрын
HII MBONA IMEANZA TUU 🤣🤣🤣
@muna1744
@muna1744 2 жыл бұрын
Hata mimi nimeshangaa nilijua part 2
@Hashdough
@Hashdough 2 жыл бұрын
@@muna1744 aah kumbe wamekosea heading tuu.. part one ndio 2 na two ndio 1
@Hashdough
@Hashdough 2 жыл бұрын
@@mkaapwekekariakoo6417 wewe ndio hujaelewa, kaa kimya
@mkaapwekekariakoo6417
@mkaapwekekariakoo6417 2 жыл бұрын
@@Hashdough 🙏🙏
@mkaapwekekariakoo6417
@mkaapwekekariakoo6417 2 жыл бұрын
@@Hashdough sijaelewa nini sasa mbona unanitaja biala sababu????
@yurisongoro2895
@yurisongoro2895 2 жыл бұрын
🥰🥰🥰🥰🥰🥰
@muna1744
@muna1744 2 жыл бұрын
Na walifanyana nini na Zamaradi
@kazkaz1943
@kazkaz1943 2 жыл бұрын
Hhhhhhhh
@ilovejesus9303
@ilovejesus9303 2 жыл бұрын
Mbona hatumjui huyo ex wa dada Dina? Natamani kumjua. Ila hongera sana dada kukuza mtoto wako
@gracemushi1283
@gracemushi1283 2 жыл бұрын
Anaitwa nncha kali yuko pale clauds
@asiaasia5025
@asiaasia5025 2 жыл бұрын
Nakumbuka kipindi cha leo tena wakati ule kilikuwa 🔥 hapa Dina pale da Suzy na kule Geàh Habib balaam lilikuwa zito. Nilikuwa malini nacho sana kipindi cha leo tena.
To Brawl AND BEYOND!
00:51
Brawl Stars
Рет қаралды 17 МЛН
Salama Na Jokate Ep 3 | KAMISHNA Part 2
29:49
YahStoneTown
Рет қаралды 150 М.
Timbulo Awasaidia Wazee Wasiojiweza
19:00
Timbulo
Рет қаралды 19 М.
To Brawl AND BEYOND!
00:51
Brawl Stars
Рет қаралды 17 МЛН