Mwanafunzi Umbwe 'boys' afariki dunia akifanya mazoezi

  Рет қаралды 3,001

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

Күн бұрын

Mwanafunzi wa kidato cha tano, katika shule ya wavulana ya Umbwe, iliyopo kata ya Umbwe Onana, Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Thomas Edward Kogal (19) amefariki dunia wakati akifanya mazoezi.
Mwanafunzi huyo ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Kigoma, anadaiwa kufariki jioni ya jana Agosti 13, 2024 wakati akifanya mazoezi na wenzake shuleni hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo Agosti 12, 2024 na kusema taarifa zaidi atazitoa baadaye.
"Ni kweli kumetokea kifo cha mwanafunzi wa Sekondari ya Umbwe, naandaa taarifa nitaitoa baadaye," amesema Kamanda Maigwa.
Akizungumzia kifo cha mwanafunzi huyo, Mkuu wa shule hiyo, Elirehema Mungaya, amesema mwanafunzi huyo alifariki dunia wakati akiwa uwanjani akifanya mazoezi na wenzake.
"Ni kweli mwanafunzi wetu amefariki jana jioni wakati akiwa uwanjani na wenzake wakifanya mazoezi, lakini alikuwa na changamoto ya tatizo la moyo,"amesema mkuu huyo.
Akizungumzia kuupokea mwili wa mwanafunzi huyo, Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Umbwe, Dk Danloard Nyimbi amesema mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo tayari akiwa amekwishafariki dunia.

Пікірлер: 8
Just Give me my Money!
00:18
GL Show Russian
Рет қаралды 1,1 МЛН
Mwanafunzi Shule ya Umbwe asimulia kifo cha mwenzake aliyefia mazoezini
4:01
RAPHAEL KENETH MIKONONI MWA JESHI LA POLISI TUKIO LA KIFO CHA MANDOJO.
8:02
ITAKUTOA MACHOZI: MFANYA KAZI WA NDANI AMNYONGA MTOTO WA MIEZI 6/UCHAWI
25:46
MPANDA MLIMA KILIMANJARO APEWA MILIONI 3 NA MZUNGU AKASOME
5:45
Mwanamke auawa Tabora, afichwa uvunguni
10:37
Mwananchi Digital
Рет қаралды 17 М.