Silaa awasimamisha wapima ardhi wawili Dodoma; aeleza wanavyohonga viongozi viwannja kuficha madudu

  Рет қаралды 17,558

Mwananchi Digital

Mwananchi Digital

7 ай бұрын

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amemuagiza Katibu Mkuu Wizara yake, Mhandisi Anthony Sanga kuwasimamisha kazi wapima ardhi Enock Katete na Cleoface Ngoye kwa tuhuma za kuidhinisha na kubadilisha ramani ya eneo linalomilikiwa na Kanisa la Morovian kiwanja namba 1,2 na 3 Block T mtaa wa Itega Jijini Dodoma.
Waziri Silaa amechukua hatua hiyo Jumatatu, Novemba 27, 2023 jijini Dodoma baada ya kufika eneo la tukio na kujionea hali halisi ya eneo hilo ambalo tayari baadhi ya sehemu zake tayari zimeendelezwa na kuwa na majengo ya kisasa na hivyo kumuagiza Kamishna wa Ardhi wa jiji la Dodoma, Jabiri Singano kuwapa notice ya kuhama eneo hilo wale wote waliomilikishwa eneo hilo kimakosa.
Aidha Waziri Silaa amebainisha kuwa baadhi ya watendaji sekta ya ardhi wasiokuwa wema wamekuwa wakiwahonga baadhi ya viongozi kwa kuwapa viwanja kama kinga yao mara wanapokutwa na makosa ili hali viongozi hao wanakuwa hawana taarifa kama watendaji hao wana nia ovu.

Пікірлер: 31
@angellomarcel5677
@angellomarcel5677 6 ай бұрын
Shikamoo Waziri SLAA, Shikamoo tena na tena Big up sana, Hao watu wa Aridhi kifupi ni WEZI WEZI WEZI WEZI hadi kiama
@mr.erickmwacha8575
@mr.erickmwacha8575 Ай бұрын
YANI NI WAHUNI MNOOO
@user-os6sc7is5h
@user-os6sc7is5h 3 ай бұрын
Waziri Akukupenda mungu na wazazi wako na mama wa hiyali samia kwisha Wengine wanafki hao 😂😂😂😂😂❤❤❤❤❤
@dollyjohn6811
@dollyjohn6811 7 ай бұрын
Safi sana waziri wetu MUNGU wa mbinguni akubariki kwa kazi unayoifanya
@deonatusyokta3579
@deonatusyokta3579 6 ай бұрын
Silaa una chembe chembe za magufuri mw Mungu akubali
@kilogreekachananawatuwasio4054
@kilogreekachananawatuwasio4054 4 ай бұрын
Waziri wa mama samia kazi hiendele ❤☝️🤲🙏🙏🙏🙏🙏
@user-xn8jh1yw1h
@user-xn8jh1yw1h Ай бұрын
Nyoosha Mstari Mheshimiwa! Remmy Ongara alisema..... "Barabara mrefu haikosi kona...." Duh! Sisi wanyonge tulikuwa hatuoni mbele kwa sababu Barabara ilikuwa ndefu na kona kibao!.......God is always Good.
@bennyinnocent2750
@bennyinnocent2750 4 ай бұрын
HUU MFUMO HAUWEZI KUMALIZA MATATIZO YA ARDHI KWANI MZIZI MKUU NI KUPEANA MADARAKA BILA KUZINGATIA WELEDI
@christinewomanoffaith5479
@christinewomanoffaith5479 28 күн бұрын
Mbona watu wengi wamepata haki zao Hatuwezi kusuburi mfumo ubadirike,utatukuta Tunaomba Arusha Kwa makonda nk.... Matapeli sugu wenye hela wamenyang'anywa maeneo yamerudi Kwa wahusika
@rosemuhandoofficial5676
@rosemuhandoofficial5676 7 ай бұрын
Ni kweli hata Mimi nimedhulumiwa kiwanja changu hapo itega BLOC H NO 33, tena nilinyang,anywa Kwa nguvu, na Mtu ameuziwa amejenga nilipojaribu kufuatikia nikatishiwa kupotezwa,,kuuawa, Inauma,
@angellomarcel5677
@angellomarcel5677 6 ай бұрын
Pole sana Haki ya mtu haipotei..Mungu atarudisha kila kitu...enzi za LUKUVI watu walifanya mno uhuni na wizi...SLAA ubarikiwe sana wewe LULU iliyokuwa jalalani..
@christinewomanoffaith5479
@christinewomanoffaith5479 28 күн бұрын
Ndo Muda huu ss Utapata haki yako
@user-xv2sb3ys6z
@user-xv2sb3ys6z 7 ай бұрын
Majizi Sana Hasa hao wafanyakazi dawa ni kuwafukuza ila uanze na huyo mkurugenzi
@jedidahbintidaudi8241
@jedidahbintidaudi8241 Ай бұрын
Jerry Slaa- the Magufuli way
@user-kt2mi9zy2j
@user-kt2mi9zy2j 4 ай бұрын
Ko mnaandaa uchaguz au
@bennyinnocent2750
@bennyinnocent2750 4 ай бұрын
HALAFU PIA UTENDAJI WA ONE MAN SHOW HAUNA TIJA ENDELEVU, TUTENGENEZE MIFUMO YENYE NIDHAMU ENDELEVU
@saidabdillahi8107
@saidabdillahi8107 4 ай бұрын
Utafika mbali kijana sasaki tunaona muheshimiwa Rais allikuwa sahihi kumuondowa yule Lukuvi wengi hatukumuelewa mwanzoni
@hamzakimaro3764
@hamzakimaro3764 7 ай бұрын
ILA WALIOUZIWA VIWANJA HAWANA MAKOSA!! MAKOSA NI YA SEREKALI KUWAAJIRI NA KUWA KAZI MAFISADI!!
@isaacmwaseba9972
@isaacmwaseba9972 4 ай бұрын
Kuna siku utasema kosa ni la Mungu kumuumba huyo mtu usitetee hao wezi ukaingiza serikali uwizi ni tabia ya mtu.
@RenaldaZeramula
@RenaldaZeramula 3 ай бұрын
Mafuru ana dhamana na serikali. Lazima.muwatafutie maeneo.mengine
@farhannahkulishwaburekunam5360
@farhannahkulishwaburekunam5360 2 ай бұрын
Hiyo mafuru ni mwizi sana na anapenda honga amewaibia sana huko tanga hata mimi alichukua pesa zangu
@chenyakwihela1637
@chenyakwihela1637 3 ай бұрын
Aisee huyu ndio kiongozi sasa anarithi njia za marehemu magufuli kabisa akiwa waziri wa aridhi daaah slaa piga kazii
@user-oh6pc7zd4s
@user-oh6pc7zd4s 4 ай бұрын
FIDA HUSSEIN NI MWIZI WA WANYONGE ARDHI ZAO NA NYUMDA ZAO DAR
@allykimu9716
@allykimu9716 4 ай бұрын
We ni mtu mtu mtu...
@user-oh6pc7zd4s
@user-oh6pc7zd4s 4 ай бұрын
FIDA HUSSEIN NI BEPARI WA ARDHI MWIZI MKUBWA WA WANYONGE MAJUMBA YA WATU ANADHULUMU
@tumainiellyimo4657
@tumainiellyimo4657 4 ай бұрын
Mh! Waziri u afaa na wizara ho safi wewe kuwepo
@hamzakimaro3764
@hamzakimaro3764 7 ай бұрын
KAKA SLAA HONGERA KWA KAZI NZURI MNO! LAKINI JICHUNGE NDUGU YETU,HAWA MAFISADI WANANGUVU KUBWA SANA,WASIJE WAKAKUTOA ROHO!! MUNGU AKULINDE
@farhannahkulishwaburekunam5360
@farhannahkulishwaburekunam5360 2 ай бұрын
Hiyo mafuru ni mwizi sana na anapenda honga amewaibia sana huko tanga hata mimi alichukua pesa zangu
@christinewomanoffaith5479
@christinewomanoffaith5479 28 күн бұрын
Kwisha habari yake kazi Hana tena
The child was abused by the clown#Short #Officer Rabbit #angel
00:55
兔子警官
Рет қаралды 25 МЛН
Vivaan  Tanya once again pranked Papa 🤣😇🤣
00:10
seema lamba
Рет қаралды 34 МЛН
Khó thế mà cũng làm được || How did the police do that? #shorts
01:00