Рет қаралды 11,626
Jina lake hasa ni Salim bin Bashir bin Salim Al-Harthy. Umaarufu wake ni Abushiri. Alikuwa kijana, tajiri na shujaa. Alisimama dhidi ya Waingereza kwao Zanzibar. Akasimama dhidi ya Wajarumani kwenye ardhi ya Tanganyika. Zanzibar aliwaachia alama ya Jengo la Mambo Msiige. Tanganyika aliwaachia athari ya mapambano ya ukombozi. Mjuwe Shujaa Abushiri.