Рет қаралды 1,554
Ukoloni wa Wajerumani katika ardhi ya nchi zilizokuja kufahamika baadaye kama Tanganyika ulikumbana na upinzani mkali kutoka kwa wenyeji, ambao waliendesha vita vya miaka kadhaa dhidi ya dhuluma ya utawala huo katili. Miongoni mwa mashujaa walioongoza mapambano hayo ni Sultani Mkwawa wa jamii ya Wahehe. Sheikh Riadh Al Busaidi anatusimulia ushujaa wa shujaa huyo na wenzake wengine.