Рет қаралды 4,584
Profesa Mussa Assad, ambaye amewahi kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kati ya mwaka 2014 hadi 2019, amefanya mahojiano na The Chanzo ambapo, pamoja na mambo mengine, ameeleza sababu zinazopelekea ubadhirifu Serikalini kuendelea kutokea.
Katika mahojiano haya, Profesa Assad, ambaye kwa sasa ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Kiislamu Morogoro (MUM) - Utawala na Fedha, ameeleza mbinu mbalimbali na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuleta uwajibikaji na kukomesha ubadhirifu wa fedha za umma.
Profesa Assad pia amezungumzia tukio la yeye kuondolewa ofisini mwaka 2019, uamuzi ambao Mahakama Kuu ya Tanzania hivi karibuni ilisema umefanyika kinyume na Katiba ya nchi.
Unaweza kutufuatilia kupitia;
TWITTER: / thechanzo
INSTAGRAM: / thechanzo
FACEBOOK: / thechanzo
TIKTOK: www.tiktok.com/@thechanzo?is_...
Au tembelea tovuti yetu: www.thechanzo.com
Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105
The Chanzo Initiative, 2022 © All Rights Reserved.