Рет қаралды 44,381
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi amewashauri wanamichezo kuwa na desturi ya kupima afya zao hasahasa magonjwa ya moyo ili kuepuka vifo katika michezo.
Prof. Janabi ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Hospitali hiyo na mwelekeo wa Utekelezaji wa mwaka wa fedha 2023/24.
Prof. Janabi ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo amesema kumekuwa na wanamichezo wanapoteza maisha katika mazoezi kutokana na matatizo ya moyo na hii inapelekewa na kutokuwa na utamaduni wa kutopima afya zao mara kwa mara.
“Kuna watu wanasumbuliwa na tatizo la mioyo yao kuwa mikubwa na unaweza ukashangaa mchezaji kaanguka ghafla uwanjani na kuna wengine hata wanapoteza maisha. Ni muhimu sana kupima afya hasa kwa wanaofanya michezo ya kukimbia maarufu kama Jogging au kutumia nguvu kama wanaokwenda gym,” ameshauri Prof. Janabi.
Prof Janabi pia maevishauri vilabu vikubwa hapa nchini kuwa na desturi ya kuwapima wacheza wao wapya kabla ya kuwasajili ili kuepukana na hasara wanazoweza kuingia baada ya kumsajili mchezaji huyo na akashindwa kucheza kutoka na matatizo ya kiafya kama moyo.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: / spotileo-176. .
HabariLeo: / habarileo
DailyNews: / dailynewstz
INSTAGRAM;
HabariLeo: ....
SpotiLeo: ....
TWITTER;
Twitter HabariLeo: Ha...