Рет қаралды 1,333
Bi Zainab Himidi alifahamika visiwani Zanzibar kama mwalimu, mwanaharakati wa haki za wanawake na pia mshairi bingwa. Kwenye Kongamano la 36 la Kiswahili lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Bayreuth, kusini mwa Ujerumani (17-19 Mei, 2024), Profesa Rayya Timamy wa Chuo Kikuu cha Nairobi alichambuwa jinsi kazi za ushairi za Bi Zainab zinavyoisaidia jamii ya Waswahili kurudi kwenye utamaduni wao, ambao ndiyo ngao ya kulinda utu wao.