Рет қаралды 195,421
November 8, 2017 mkutano wa sita wa Bunge la 11 umeendelea tena Bungeni Dodoma ambapo Wabunge walikuwa wakijadili na kushauri kuhusu mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa.
Ni mpango unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango na bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Kati ya Wabunge waliopata nafasi ya kusimama na kuzungumza ni pamoja na Mbunge wa Tarime vijijini John Heche ambae alihoji uhalali wa Serikali kuchoma moto nyumba za Wananchi wa tarime pamoja na kukamata mifugo ya wafugaji.