Рет қаралды 38,914
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amemvaa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu kwa kukosoa baadhi ya mambo akkisema kkwamba mambo hayo yamefanywa na Rais Samia kwasababu ni Mzanzibari.
Waziri Nape ameyasema hayo leo Jumatatu, Aprili 29, 2024 wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo ameeleza kuwa alitegemea chama chake kimkemee.
Akizungumza Mkoani Manyara siku chache zilizopita Tundu Lissu alisema kama kusingekuwa na muungano Rais Samia Suluhu Hassan asingekuwa Rais wa Tanzania.
"Bila miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Samia Suluhu Hassan asingekuwa anafukuza Wamasai, anafukuza sababu ya kuwa na muungano" ameongeza