Рет қаралды 32,397
Miaka tisa iliyopita Kijana Tumaini Mabula (32) alisafiri mpaka Dar es salaam kutafuta maisha lakini ikawa kinyume na alivyotarajia, akakutana na majanga yaliyomfanya aishie kukaa mahabusu kwa miaka tisa lakini sasa ameachiwa huru na kusimulia yote kwenye @ayotv_
February 2013 akiwa anaishi Mwananyamala Jijini Dar es salaam Rafiki yake alimuomba kutumia chumba alichokuwa anaishi (gheto) ili apumzike na Mpenzi wake hivyo Tumaini akaondoka kwenda Kariakoo alikokuwa anafanya shughuli za kujitafutia kipato na kuwaacha wawili hao ndani kwake na aliporudi jioni akamkuta Girlfriend wa Rafiki yake akiwa amefariki na baadaye akagundua kwamba Rafiki yake ameshatoroka hivyo kesi ya mauaji ikabaki na yeye.
Tumaini awali alisema yuko huru mtaani na ndio kwanza anataka kuanza moja akiwa hana chochote wala msaada, hana pa kulala, hana kazi na hana Ndugu wa kumsaidia na akatoamba namba ili yeyote atakayeguswa amsaidie chochote kwa Airtel money 0688580756 jina Abilahi Abdallah.
Leo amerudi tena na kuwashukuru Watanzania kwa kumchangia akapata zaidi ya Tsh. Milioni ambazo zimemuwezesha kupanga chumba Mbezi na kununua godor, jiko na vitu vingine vya kuanzia maisha, amebakiwa na Tsh. Laki 7 na sasa ana mpango wa kufungua kibanda cha kuuza matunda, bado anaomba support ili azidi kusimama zadi… simulizi yake nzima ipo kwenye KZbin ya millardayo,